Maserati
JF-Expert Member
- Jun 15, 2014
- 11,602
- 20,101
chikundi this is what tulio na uelewa wetu tunajiuliza. Sio kushangilia tu tunaibiwa na kumtoa kafara muhongo.Pia ninahoji,je wakati makontena yanawekwa chini ya vyombo vyetu vya dola,watu wa migodi walishirikishwa kwa maana kuwe kuna SEAL/lakiri ya pande zote mbili,serikali na mgodi ili yeyote asije akacheza na ushahidi kwa kujaza mchanga ionekane kwamba Dhahabu ni nyingi au kidogo?
Na je, kulikuwa na ulinzi wa pande mbili serikali na migodi katika hayo makontena? Isijekuwa askari wa mgodi walitimuliwa?
Je wakati timu ya rais inachukua sample,lakiri/seal zilifunguliwa nani akiwepo? Na wakati zinafungwa,je ziliwekwa seal/lakiri za mgodi na serikali au za serikali tu? Kama za serikali tu ndio zipo,je mgodi hawawezi kujenga hoja mahakamani kwamba serikali ilikuwa na kudhibiti wa kontena hivyo inaweza kuwa imecheza na kilichomo kwa kuongeza ili kuukandamiza mgodi?
Je taratibu za kutatua mgogoro kati ya mwekezaji na serikali zinamtaja rais? Au kamishna wa madini? Au Mkuu wa TMAA? Au TRA? Kama taratibu hazimtaji rais,je zuio lililotoka ni halali? Je kwa nini ripoti ya kamati ime-condemn migodi bila kuwapa haki ya kusikilizwa mpaka imebidi waombe nakala ya ripoti kupitia mitandaoni?
Kwa nini tumewachafua kabla ya kuwaita na kusikiliza upande wao? Mwanasheria Mkuu kwa nini hakutoa simple procedure kwamba kila mtu ana haki ya kusikilizwa kabla ya kuchafuliwa? Kwa hili tu,lazima tutalipia gharama kurudisha heshima yao,tumewachafua vilivyo!
Punguza ukibendera,elewa mambo kwa upana.