GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,281
- 6,697
Niweke wazi kuwa mimi si mtaalamu wa Madini wala hiyo inayoitwa Sheria ya madini, kinachonishangaza ni hili la msururu wa wasomi ambao umeibuka na kuanza kuponda kile kilicho au kinachofanywa na Rais Magufuli.
Kinachonishangaza zaidi ni kuwa wengi wa Watanzania wa kawaida tulikuwa hatujui chochote kuhusu hili lakini hawa wasomi walikuwa kimya hivyo kutunyima fursa ya kufahamu kinachoendelea.
Hawakuzungumza chochote na wala kushauri kama wanavyofanya sasa mitandaoni na kwenye
vyombo mbalimbali vya habari kwa nguvu kubwa ajabu.
Kinachonishangaza zaidi ni kuona hawa wasomi wakiwa wameegemea wazi upande wa hawa maadui zetu, badala ya kusaidiana kama taifa kuangalia ni namna gani tutapambana nao.
Niseme wazi kuwa mimi kama Mtanzania niko bega kwa bega na Raisi JPM ingawa
katika uchaguzi kura yangu iliangukia kwa Hashim Rungwe.