Kuna methali na misemo tulifichwa maana

Kuna methali na misemo tulifichwa maana

Weledi wa wahenga wa kuondoa ukakasi kwenye kila kitu ulipelekea usanifu wa sanaa kwenye lugha, lahaja, na vitenzi... Mathalani lugha ngumu iliyovalishwa koti iliweza kupeleka ujumbe tarajiwa bila kupotosha maana wala kuleta ukakasi kwa rika zote...!

Lugha picha ilitumika kuficha maneno ambayo ni magumu kutamkika mbele ya hadhira ama kwenye kundi lenye rika tofauti na jinsia pia.. Siku hizi hakuna ubunifu tena.. Vijana wanafyatua tuu..! Dhima ya BARAZA LA SANAA LA TAIFA NA BAKITA Imetweza na kupotoshwa na wanasiasa barobaro na kuyafanya hayo mabaraza sasa yatumike kisiasa zaidi kuliko kijamii.

Msemo wa TABASAMU LA KUMTOA NYOKA PANGONI..Wengi wanajenga picha halisi.. Lakini kiuhalisia si tabasamu la mwanaume bali ni tabasamu la kike na nyoka anayetoka pangoni ni kile kiungo kinachotambulisha jinsia ya kiumeni.. Sasa hiki kinatokaje pangoni! Wanawake wana tabasamu zao very amazing ambazo akikupa moja tu na jicho lake la huba na mahaba mazito utajikuta janaume mwili wote unasisimka na nyoka wako kuanza kujiviringua toka mafichoni akitamani vinavyopoza mtima wa kumoyo..!

Lakini pia kuna baadhi ya misemo nahau na mithali zinapoteza maana kwakuwa matukio yake halisi hayapo tena.. Kwa mfano kwa kizazi hiki utatumia maneno gani kuelezea ugonjwa mbaya kabisa wa ukoma wa enzi hizo na ulivyoogopeka mpaka kupelekea usemi wa MUOGOPE KAMA UKOMA.. Ugonjwa huu haukuwa na tiba na ulishambulia ngozi na vidole na hata midomo.. Waathirika wengi walikatika hivyo viungo na ilikuwa ukipata huu ugonjwa unatengwa kwenye sehemu maalum.. Hospital nyingi zilikuwa na wodi maalum za wagonjwa wa ukoma.

Shimo la tewa! Hili ni gereza moja hatari sana mjini Mombasa Kenya ukipelekwa huko na ukafanikiwa kutoroka wewe ni jini.... Sehemu za siri za mwanamke zinafananishwa na shimo la Tewa kwakuwa zimeangamiza wengi sana Pengine hata wewe pia unayesoma hapa.

Sasa imagine nyoka atoke pangoni kisha aingie shimo la tewa! Unapata picha gani hapo?
Mshana hiviii!!! una miaka mingapi kwani!!
 
Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani!.....sasa hapo umenipongeza tu nakuuliza tena umri wako ganiuii?/
 
Mwenda tezi na omo marejeo ni ngamani!.....sasa hapo umenipongeza tu nakuuliza tena umri wako ganiuii?/
Mwaka 1984 ndio niliachana na CCM rasmi!?
 
ebanae !!! enzi za mchonga??? uliwahi sema humu ulikuwa form one palee bukoba nyakato sec. school miaka hiyo!! ccm utarudipo lkn!
Nikirudi chama chawala niite chawa
 
Ukiona vyaelea vimeundwa...... Siku vitu vinajiunda vyenyewe na havielei tena....
Wajuu mgoje chini...... Siku hizi hawarudi chini ndy kwanza wanazidi kuvutana ili waende juu zaidi.... Wa chini utasubiri sanaa.
 
Ukiona vyaelea vimeundwa...... Siku vitu vinajiunda vyenyewe na havielei tena....
Wajuu mgoje chini...... Siku hizi hawarudi chini ndy kwanza wanazidi kuvutana ili waende juu zaidi.... Wa chini utasubiri sanaa.
Wa chini utasubiri sanaa.
 
"Huwezi kuwatumikia mabwana wawili"

Huko Kenya kuna mwanamke mmoja ameolewa na wanaume wawili na anasema anawapenda sana analala lao kitanda kimoja.

Dunia inaenda kasi sana mama katengua kauli ya Bwana Yesu.
 
Back
Top Bottom