ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Mimi ni mfanyakazi katika moja ya ofisi hapa mkoa wa Arusha. Tunafanya kazi ambayo siyo ngumu sana, mara nyingi ni kutumia kompyuta na kushughulikia majukumu ya kila siku ya ofisi. Ndani ya mazingira haya ya kazi, kuna mdada mmoja ambaye tumekuwa tukifanya kazi pamoja kwa muda sasa.
Kwa mwanzo, mahusiano yetu yalikuwa ya kikazi tu salamu za asubuhi, kuulizana hali, na mazungumzo ya kawaida kuhusu kazi. Lakini kadri siku zilivyoendelea, nilijikuta nikianza kumfikiria zaidi ya mwenzangu wa kazi. Kila tunapokutana, napata furaha ya kipekee, na muda mwingine hata nasahau kabisa msongo wa kazi.
Changamoto yangu kubwa ni hofu. Naogopa kumwambia hisia zangu kwa sababu tunaendelea kufanya kazi ofisi moja. Najiuliza, vipi kama atanielewa vibaya? Je, hali ya kikazi itabaki kuwa ya kawaida au itabadilika? Sitaki kuvuruga mazingira ya kazi wala kumuweka katika hali ya kutokuwa na uhuru.
Je, nifanye nini katika hali kama hii? Niendelee kuficha hisia zangu na kulinda kazi yangu, au nichukue ujasiri nimwambie kwa heshima na utulivu, nikikubali matokeo yatakavyo