Kuna mbinu mpya ya matapeli kuwalaghai watu inayoitwa 'IMERUKA'

Kuna mbinu mpya ya matapeli kuwalaghai watu inayoitwa 'IMERUKA'

Weka ufafanuzi yakinifu tukuelewe.

Kuna link gani ya mimi kuweka namba ya siri kuangalia salio na kumpa mtu mwingine access ya kuijua namba ya siri?

Kuna uhusiano gani wa ule muhamala wake na nafasi ya yeye kuweza kuijua namba yangu ya siri iwapo tu nitaamua kuangalia salio?

Kwamba ule muhamala unakuwa ni trojan au BAT kuwa jaribio lako lolote la kuweka namba ya siri litakuwa recorded na kutumwa kwa huyo spy ambaye ana monitor hizo viruses?

Kwasababu navyojua mimi hata mtu ajue namba yangu ya siri hawezi kutoa hela iliyopo kwenye account yangu remotely bila kushika simu yangu au line yangu.

Mtu yupo Tanga mimi nipo Mbeya na hiyo line yangu, sawa huyo mtu wa Tanga anaijua namba yangu ya siri lakini line ninayo mimi....anatoaje pesa kwenye account yangu pasipo kuwa na sim card yangu?

Otherwise niwe nimetumia let say Tigo app kwenye simu yake bila ku log out, hiyo tu ndio njia pekee inayoweza kumuwezesha kutoa pesa kwenye account yangu.

Vinginevyo tuambie kivipi jambo hilo liwezekane?
 
⚠️ 🎭`
WIZI MPYA
Kuna mbinu mpya ya matapeli wamekuja na kuwalaghai watu inaoitwa 'IMERUKA'.

Tapeli hukutumia pesa kwenye simu yako akitumia namba yake.

Hii si pesa fake, ni ya kweli kabisa anakutumia pesa kidogo kama laki 100000 au elf 50000 na hata hana shaka.

Baada ya kutuma pesa hizi kisha anaanzisha muamala wa kutoa pesa kwenye account yako yako. kuna menyu ya kurequest muamala kutoka kwenye namba ya mtu mwingine ambae yupo mbali. Ila yule mtu atatakiwa aweke namba yake ya siri ili kuruhusu muamala huo.

Sasa tapeli anafanya hivyo kwa sababu anajua Unapopokea ujumbe kwenye simu yako kuwa umepokea pesa jambo la kawaida ni kufurahia na kisha kutaka kuangalia salio lako.

Ili kuangalia salio utahitaji kuweka Nambari yako ya siri (Msimbo).

Mara tu utakapofanya hivi utakuwa umethibitisha ombi lake la kutoa pesa kwenye akaunti yako.

Akaunti yako itaruhusu ombi lake la kutoa hela kiotomatiki na kuchukua pesa zako.

Ujanja ni kukurubuni tu kwa kiasi kidogo ili kukuibia.

Ili kujilinda dhidi ya ulaghai huu wakati wowote ulipopokea amana hiyo isiyotarajiwa, ili kuangalia salio lako kwanza weka Nambari ya Msimbo isiyo sahihi makusudi.

Kitendo cha wewe kuweka Msimbo wa uongo itafuta maombi yoyote ya tapeli kiutoa fedha toka akaunti yako. Kisha angalia salio lako kwa Nambari yako halisi ya Msimbo.

Kwa uhamisho huu mpya wa pesa za kielektroniki na Artificial Intelligence (AI) tufanye hivyo kila wakati ili kuepuka kudanganywa na matapeli hawa ambao kila mara wanakuja na mbinu mpya za kujaribu kutuibia.

Shiriki habari kama hizi kila wakati na familia na wafanyikazi wenza pia ili kuwafahamisha na kuwa macho.

KAA MACHO!
 
View attachment 3150505


Kuna mbinu mpya ya utapeli ambayo matapeli wamekuja nayo kuweza kuwalaghai watu na kuwaibia inaitwa "𝗜𝗠𝗘𝗥𝗨𝗞𝗔".

matapeli hao wanafanya kazi ya kukutumia pesa kupitia simu yako Yani wanabuni namba ya mtu kisha wanawatumia kiasi kadhaa cha pesa kupitia namba yake ambayo ni private namba.

View attachment 3150506

Pesa unayotumiwa ni ya kweli sio Feki!! Wala nini, anaweza kukutumia kuanzia kiasi cha Shilingi Elfu ishirini kushuka chini kwaiyo inaweza kuwa 20k , 15k , 10k au 5k bila kuwa na shaka yoyote.

Baada ya hapo atakupigia simu kuomba kurudishiwa muhamala ambao ametuma kimakosa , hivyo Kuna menu ya kuomba kurudisha muhamala uliotuma toka kwenye namba ya mtu mwingine ambaye Yuko mbali ila wewe inabidi Uweke namba yako ya Siri inawezekana ikawa
• Airtel
• Tigo
• Vodacom
• Halotel
• TTcl
• Zantel nk

View attachment 3150509

View attachment 3150515

Tapeli anajua unaweza kuangalia Salio lako kujua Kama kweli pesa hii imeingia au lah wakati unaingalia Salio si utaweka NAMBA YAKO YA SIRI NDO KOSA lenyewe sasa 😌.

Kwani ukifanya hivyo tu utaweza kuruhusu pesa zako zote zilizopo kwenye akaunti kuhamishwa kwa kugawa password yako bila kujua.

🧿 𝗞𝗨𝗠𝗕𝗨𝗞𝗔
ukiona ujumbe wowote wa utapeli au namba ya utapeli kwenye simu yako jitahidi kuweza kuripoti kupi
tia namba hii 15040.
Hueleweki. Yani niangalie salio langu kisha hela ziende kwa tapeli...hakuna kampuni ya simu yenye mfumo wa kibwege ivo...!Acha kuokoteza taarifa mtandaoni ambazo wewe mwenyewe huna uhakika nazo
 
Mimi mtu akikosea kutuma hela kwangu atafanya yeye juhudi arudishiwe,huwa namshauri awasiliane na mtandao wangu wao watajua namna ya kufanya hela irudishwe na nadhani ndiyo sheria inavyotaka.

Ishu ya kujua salio huwa naangalia kupitia text ya mwisho kutoka muamala wa mwisho kuufanya tujifunze kuhifadhi jumbe za muhimu kama hizo then # ya siri itumike pale unataka kufanya muamala tu na tena ukiwa timamu kiakili mtaani hali ni mbaya sana watu kila siku wanabuni wafanye nini ili waishi
 
Ni jukumu la makampuni ya simu kuhakikisha usalama wa amana za wateja. How comes tapeli aweze kuni-control remotely mimi naingiza msimbo hela inaenda kwake without my knowledge? Makampuni husika yawajibike haraka sana else watangaze kushindwa ulinzi wa amana za wateja tuachane nao.
 
Back
Top Bottom