kuna madhara gani kuishi mbali na mume?

kuna madhara gani kuishi mbali na mume?

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,999
hali zenu wanaMMU,
Joy na mumewe wamefunga ndoa mwaka jana,baada ya mwaka wakabahatika kupata mtoto. sasa Joy kanambia ana mpango wa kuhamia Arusha (kwani wanaishi Moshi) na kumuacha muwewe kisa Moshi watu wanamfatilia sana maisha yake na mumewe asionekane na mumewe akifurahia ndoa,washasema maneno kwamba anajisikia, wadada wa mjini walishamtisha kuwa wanatoka na mumewe,mara mumewe ni mwathirika,in short hana raha kuishi hapo anapofanyia kazi mumewe. kaamua kuhama ili kuepuka hizo karaha.je ni sahihi?
 
Akija Arusha anitafute nitajitahidi kuziba pengo ila awe tayari kupima ngoma .Hapa kukaa mbali na mumeo unaweza kupata vishawishi ukajikuta umeongeza idadi ya kumsaliti na yeye pia.Hivyo ndio maana watu wanaaishi pamoja kama kulikua hamna haja ya kuishi na mumeo ungeendelea kukaa kwenu ukawa unampelekea wikiendi tu
 
Hilo jambo si sahihi kabisa, huyo mke amekosa subra na uvumilivu.
Avute subra na avumilie mambo yote anayofanyiwa na wanajamii especially madada wenzake, kwani mwisho wa siku nao watachoka na kumuacha akila bata na mumewe.
Mambo haya yapo mengi sana, kuna wanawake huwa wanaona wenzao walio kwenye maisha mazuri na ya furaha kwenye ndoa wanazani hawajafanya bidii zozote zile za kuyaweka hapo maisha.
Nawashauri wawaachie walio kwenye ndoa ya furaha waendelee kufaidi.
 
si sahihi waondoke wote au avumilie
 
Kwanini wasihame pamoja, kama imekuwa unbearable?

By the way, anajuaje kama watu wanamsema au anayatafuta maneno mwenyewe? Maana mimi huwa sijui kama hata nasemwa kwani hakuna anayeweza kuja kunieleza fulani ana sema nini juu yangu. Muda ni mchache lakini siruhu vitu kama hivyo.

Ajaribu kubadili life style yake, kama anaentertain maneno na umbea basi huo muda autumie kwa something productive au ni mara mia hata apande kitandani asome biblia kuliko kuruhusu maneno ya mitaani.

Kumkimbia mumewe wakati mumewe hajamkosea ni ujinga, unless anayaamini hayo mambo. Na kama anaweza akapime na amuombe mumewe wakapime wote ili kujitoa wasiwasi kuhusu uathirika.
 
Syo sahihi coz' hakuna sehemu ambayo hakuna maneno kawaida kuishi na mwanadamu mwenzako yataka moyo maneno yanakuhamisha wewe !
 
Ivi mtu utaharibu ndoa yako kisa maneno ya watu,,embu wanawake tuwe wavumilivu je atakapohamia wakimsema atahama tena?
amuache mumewe halafu akipatiwa mke mwenzake atalalamika?
Joy alikiri kua ye na mumewe kwa shida na raha au alijua ni maigizo afanya?
 
si sahihi waondoke wote au avumilie

Nimekubaliana na wewe ktk kipengele cha kuvumilia ila issue ya kuondoka wote cdhani kwan m2 unapaswa kukabiliana na matatizo upambane ili kuyamaliza na co kukimbia
utakimbia matatizo mpaka lini?
 
he he he heeee! yaani ndio kawapa nafasi sasa ameogopa kusemwasemwa matokeo yake kaamua kuwaachia mume thubutuu mimi sifanyi ujinga huo hata kidogo.
 
ni kweli usemayo Marga, Joy anadai kashatafuta kazi Moshi lakini hajapata, hivyo anahamia Arusha ili afanye biashara kwani Arusha kuna opportunity nyingi.. . .
 
Last edited by a moderator:
yaani nitoke kwangu kisa maneno!!! watahama wao kwa jinsi nitakavyoapply U-MATONYA, NA U-STEVE WONDER! lol.
 
yaani nitoke kwangu kisa maneno!!! watahama wao kwa jinsi nitakavyoapply U-MATONYA, NA U-STEVE WONDER! lol.

asante kwa ushauri shostito, kesho nita-meet na Joy namueleza ushauri wote wa hapa jamvini then ataamua kusuka ama kunyoa!
 
mods tafadhalini, nipo mahali ambapo mtandao unasumbua na nimejikuta na-double post. nawaomba muiunganine hii post. . . samahani kwa usumbufu. Paw, Invisible na Fang naomba msaada wenu!
 
Last edited by a moderator:
Akija Arusha anitafute nitajitahidi kuziba pengo ila awe tayari kupima ngoma .Hapa kukaa mbali na mumeo unaweza kupata vishawishi ukajikuta umeongeza idadi ya kumsaliti na yeye pia.Hivyo ndio maana watu wanaaishi pamoja kama kulikua hamna haja ya kuishi na mumeo ungeendelea kukaa kwenu ukawa unampelekea wikiendi tu

mkuu samahani, nimetumia majina yasiyo sahihi ilimradi ujumbe uwafikie wanammu, yawezekana mumeme,rafikize joy wapo humu.ndo mana sijatumia majina halisi
 
Aache Upuuzi Kwani huyo Mumewe au Bwana Ake...na Akichanganya watampa uchi Kweli Mumewe ...

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
usemayo ni kweli Mahmetkid kwani mtu unapaswa kutatua tatizo na si kulikimbia. asante kwa ushauri!
 
Last edited by a moderator:
Yani anautelekeza mji wake kwasababu ya maneno ya watu?na mmewe si hana tatizo kwa hayo maneno so kwanini yy anapay attention huko nje?kama kuna tatizo alirekebishe otherwize mi sijaona point ya huyo dada kuondoka unless she has more in mind.

Ama kwel mwanamke mpumbavu huivunja ndoa yake mwenyewe na mwerevu huijenga.
 
Kaunga, ilikuwa hivi. alitumiwa message na mdada kuwa "mimi nimetembea na mumeo na nimemwambukiza HIV hivyo mjiandae kutumia ARV. issue nyingine aliipata live akiwa saloon. wadada wa saloon walikuwa wakimuongelea mumewe na ilionesha kuna mdada mmojawapo alikuwa anatoka na mumewe. yan sio habari za kuambiwa. kuhusu kuhama ni ngumu make ni miaka miwili tu tangu mumewe ahamishwe toka Arusha kwenda Moshi. si rahisi kurudi tena Arusha bila sababu za msingi.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom