Kuna maana yoyote ya kutamba kuwa wewe ni mtoto wa mkulima bila kuwasaidia wakulima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuna maana yoyote ya kutamba kuwa wewe ni mtoto wa mkulima bila kuwasaidia wakulima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Nov 17, 2010.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wakati akitoa hotuba yake fupi ya kuwashukuru wabunge kwa kumpitisha kuwa Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda aliendeleza kauli yake maarufu kwamba yeye ni mtoto wa mkulima. Nimekuwa nijiuliza mara kwa mara mantiki ya kauli hiyo. Lakini naona kama imekaa kisiasa zaidi. Binafsi ningeona kuwa ni kauli ya maana kama tungeona 'impact' ya uongozi wake katika kuwakomboa wakulima wa nchi hii. Lakini sioni mabadiliko yoyote. Wakulima wanaendelea kuwa ndiyo mafukara siku hadi siku. Sijui mnasemaje wanajamvi?
   
 2. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Sawa kabisa. Kinachotakiwa ni kuleta maendeleo. Asili ya mtu haijalishi.
   
 3. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #3
  Nov 17, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Yeye ni mtoto wa mkulima sio wakulima!, so akiwa kama mtoto wa mkulima huu ndio wakati wa kuwa mtoto wa kigogo (FISADI).
   
 4. Mo-TOWN

  Mo-TOWN JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,626
  Likes Received: 138
  Trophy Points: 160
  Nakubalina nawe 100% Ni siasa tu na kutaka kukubalika na wananchi wa kipato cha chini zaidi ya hapo hakuna utashi hata kidogo.

  Ofisi yake ya TAMISEMI chini ya kauli mbiu ya Kilimo kwa kushiriana na wananyabiashra wanaratibu nunuzi wa power tillers kwa Halmashauri zote TZ bara. WM na timu yake wanafahamu fika kuwa power tillers zina ufanisi kwa maeneo machache hapa TZ kwa maana ya kufanya kazi. Pamoja kujua hilo na kutokuwa makini na ama kwa kujua wafaidika wakuu ni wafanyabiashara jambo hilo limeachwa tu na mbaya zadi Halmshauri zikaagizwa kununua hizo power tillers. Nasema zikaagizwa yaani si ombi. Mtoto wa mkulima? Yeah kwa kuzaliwa na mkulima sio kwa maana kuwasaidio wakulima kisera na utekelezaji na ufuatiliaji maslahi ya wakulima kama ilivyo kwa wachimba madini.
   
 5. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Hivi wakulima wanahitaji pembejeo na masoko pekee? Ney i think they deserve basic social services kama elimu,afya na miundo mbinu bora.to me sera isiwe "kilimo kwanza" bali "uadilifu kwanza" au "uwajibikaji kwanza" hiki ndicho kilichokosekana hapa Tanzania.there is no a difference btn mtoto wa mkulima na mtoto wa mfanyakazi(e.g mwalimu) wote wanalalamikia njaa.let me say mimi ni mtoto wa mfanyakazi.
   
 6. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 818
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Sawa na yale kujiita Mwalimu, wakati unapanda Cidiz na msafara kwenda kazini, ndege first class,kila unapopita wewe ni V.I.P . Walinzi kibao, ,msosi wa kueleweka , baadhi ya watoto wanasoma Cuba na Russia na unafia London tena kwenye Five star Hospital.
   
 7. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Mbona siuelewi!!! Au ni hangover ya pombe za mafisadi kusherehekea ushindi wa jana mjengoni wa kuingiza vibaraka wa mafisadi!! Unaonaje ukipunguza maji kidogo na kuendelea kulala?
   
 8. s

  sombyo Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 19, 2009
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumpe muda, kipindi chake cha kwanza kilikuwa kidogo ukicompare na uzito wa kuwasaidia wakulima wote kwa wakati mmoja (katika kilimo ambacho infact kilikuwa kimekufa). He sounds serious, hence let us wait and see
   
 9. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #9
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,555
  Likes Received: 18,257
  Trophy Points: 280
  Pinda kweli ni mtoto wa mkulima, kwanza hajisikii, walinzi wake wako relaxed sio makauzibe, gari ni mujibu wa kanuni na taratibu, akiongeo yuko humble, wakati wa kampeni baada ya kuona uchafu wa kampeni za chama chake, alijinyamazia na kujikalia kando etc, etc.
   
 10. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2010
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Ni mtanzania gania ambaye babu yake au baba yake sio mkulima, mfugaji, au mvuvi? Hiyo ya kujiita yeye ni mtoto wa mkulima ni sawa na kusema kuwa yeye ni mtoto wa mla ugali.
   
 11. Questt

  Questt JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2010
  Joined: Oct 8, 2009
  Messages: 3,013
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa ni mtu wa sound (siasa mingi sana) kuliko utendaji...Cheo chake ni cha kitendaji zaidi.....Ila yeye ni mtu wa kujidai ni wa hali ya chini kila siku....What am sure of ni kuwa wanasiasa wengi wakongwe wanatokea vijijini....so kilimo ndo kiliwapa kula koz kusoma walisoma BURE.(免费)

  Jana karudia kauli yake kuwa yeye ni mtoto wa mkulima lakini for two n half years tulitegemea kuona japo tunda mabalo liwe hata halijaiva kutoka kwake.....Kuna kitu ambacho Pinda alikisahau katika kuwakomboa wakulima, wavuvi, wafugaji na Warina asali.....ELIMU I repeat ELIMU...Huwezi kuwapa watu uwezo wa kuwa na zana za Kisasa hali ya kuwa hawana elimu, hawana shule bora, hawana Walimu, hawana mazingira stahili kwa walimu....Kama anataka kuwakomboa wakulima awape elimu then the rest will follow......

  Sasa unataka wawe na matrector na power Tillers while kichwani hakuna kitu??? Ili iweje?? Wakusikilize wewe tu??? Ukisema chagua flani wachague hata kama huyo mtu ni hamnazo wamchague tu???? UKIFA????? PINDA am asking you....While ukiwasaidia katika kilimo bora, uvuvi Bora, Kurina asali Bora, Ufugaji Bora then uwape elimu kwa speed zaidi...hapo utakua umewasaidia.......
   
Loading...