Kuna kitu tunafichwa TRA

Kuna kitu tunafichwa TRA

naona kama kuna baadhi ya watu wanataka wamkwamishe tu wallahi hii sio poa
 
Soma tangazo vizuri la serikali. Uliotenguliwa ni uteuzi wa mwenyekiti wa bodi siyo bodi nzima. Pia ufahamishwe kuwa Bodi ya TRA inaundwa na ex-official members kama ifuatavyo; Gavana wa BOT, Katibu Mkuu wizara ya fedha, Katibu Mkuu wizara ya fedha Zanzibar, Mwenyekiti Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB), Katibu Mkuu Tume ya Mipango, Mkuu wa Chuo cha IFM, Kamishna Mkuu wa TRA na Company Secretary wa TRA. Hawateuliwi kwa majina bali nyazifa zao.
Ivi ni kweli ujui kusoma au ndo kujitia kujua sana sasa ni ivi mkuu wa nchi ametengua na kuvunja bodi nzima
 
Jpm hakurupuki aisee ukiona kafumua sehemu ujue anajua kuliko tunavyojua tatizo ni moja spidi yake ni Kali kuliko mazoea ya watz ndio maana ni kama hatumwelewi ila anajua anachokifanya kumbuka urais ni taasisi
Sasa akili ndogo kama ya kwako itaweza kupambanua maswala kama haya? Si ni sawa na mtoto wa mwezi mmoja kumpa ugali?
 
Kilichoongezeka ni pesa hazina baada ya kuamuru pesa zote zilizokuwa zinawekwa kwenye akaunti za benki za idara, mashirika na taasisi za serikali zipelekwe BOT.

Ni sawa na baba aliyewaruhusu wanafamilia wake kila mmoja atunze pesa zake halafu siku moja akaamuru pesa za wanafamilia wote atakuwa anatunza yeye. Baada ya hapo akatangaza kipato chake kimeongezeka!
Mfano sawia
 
Uwakala wa forodha ni moja ya sekta nyeti katika moyo wa uchumi wa Taifa letu.Kuongezeka kwa mapato ya nchi kuanzia katika bandari,Viwanja vya ndege,Mipaka ya nchi na biashara ya kimataifa kwa ujumla kunahusisha unyeti wa shughuri za forodha.

Mawakala wa forodha ni wawakirishi wa Mamlaka ya Mapato katika tathmini,ukaguzi,uwasirishwaji,ukokotoaji mapato ya serikali,ushawishi,Ukusanyaji Kodi stahiki,Ukaguzi na ufanikishaji wa biashara baina ya pande kuu kibiashara {Suppliers,Manufacturers,Shippers,Consignee,Importers,exporters,Consumers}.Hivyo mlolongo wa majukumu tajwa ya mawakala husika ni nyeti mno hivyo viwango vyao vya uadirifu,uaminifu,ukweli,uzalendo,uwazi kiutendaji,uelewa na mengineo vyapaswa kuwa juu kana kwamba ni watumishi wa mamlaka ya mapato ama umma.

Kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wasio waaminifu,wageni wenye mitandao ya kimataifa kibiashara,wenye viwanda kumiriki makampuni ama kutaka kumiriki makampuni ya uwakala wa forodha kwa kusudi la kuyatumia kuhujumu taifa {uagizaji bidhaa chini ya viwango,usafirishaji nyara,Usafirishaji mafuta yasiolipiwa kodi {Transit},Usafirishaji magogo,yasiyoruhusiwa-kwa kutengeneza nyaraka za bandia,kufanya udanganyifu kiforodha kwa kukwepa kodi/tozo stahiki kwa namna moja au nyingine.

Kwa sasa wamiriki wageni {wachina,wahindi,wasomali,waarabu} na wengine wengi wa makapuni yaliofungiwa kwa makosa mbalimbali ya ukiukaji wa taratibu za kiforodha yamekuwa yakitumia wamiriki vimvuri kufanikisha upatikanaji wa leseni kisha kuendelea kufanya biashara kwa makusudio ovu kwa nchi.Wapo wamiriki wenye kampuni mbili,tatu na zaidi kwa maana ya moja ikikutwa na maswahibu,wanakuwa na wigo wa kutumia nyingine.

Ni rai yangu kwa Mamlaka ya Mapato na Sumatra kuwachunguza kwa kina wamiriki na waendeshaji wa haya makampuni ya forodha ya zamani na yanayomba leseni sasa ili kubaini wahusika wenye kiu/uchu/dhamira ovu kuepusha kuwa maficho ya wezi,waroho wa utajiri kwa njia zisizo halali,upigaji dili n.k..

Pia baadhi ya makampuni yenye vinasaba na maafisa au wafanyakazi wa TRA,TPA yasimamishwe kufanya shughuri na mapya yasipewe leseni sababu ya migongano ya kimaslahi.Ninayo imani yanajulikana na yapo.Viongozi wenye dhamana katika hili msisubiri kutumbuliwa,chukueni hatua stahiki kwa maslahi ya taifa.Pia sifa za ziada ziongezwe kwa wafanyabiashara wenye nia ya kuwa mawakala wa Mamlaka ya mapato.Intergrity,Credibility,Weredi wa biashara ya kimataifa,Shipping na uzalendo vipewe kipaumbele.
 
Jpm hakurupuki aisee ukiona kafumua sehemu ujue anajua kuliko tunavyojua tatizo ni moja spidi yake ni Kali kuliko mazoea ya watz ndio maana ni kama hatumwelewi ila anajua anachokifanya kumbuka urais ni taasisi
Ni wazi kuwa wewe hujui anachokifanya JPM [emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Habari zenu wana jamvi ndugu zangu akili yangu inanituma kuamini kuwa watanzania kuna kitu tunafichwa pale TRA.

Najiuliza iweje mkuu apangue bodi iliyowezesha mapato kupanda hadi trilion 1.2 kwa mwezi. Baada ya kufuta bodi hapo hapo mkuu wa nchi anamteuwa Naibu Kamishna nafasi iliyoku wazi kwa mwaka mzima wakuu hapa kuna kitu.

Huenda kuwa makusanyo tuliyokuwa tunatangaziwa na TRA ni figure feki labda mzee kashtuka. Kiukweli hainiingii akilini eti mzee kaamua kupiga bodi nzima chini na kuteuwa mkusanya kodi mkuu namba mbili bila kuwa na tatizo mzee atakuwa kachoka na figure izi feki bodo tuna safari ndefu.
Hapo ndio ujue ccm ni ileole
 
Ccm ilipoanzisha maisha ya kipropaganda,watumishi nao wakaiga,ngoja namba zisome
 
ngoja nigoogle nione raisi yupi anashikilia record ya kufukuza viongozi wengi ndani ya mwaka. may b baba kashatembea na hiyo record
 
Mimi nadhani walikuwa wanalazimishwa kutangaza mapato makubwa kuliko wanayokusanya, walipoamua kutaka kuwa wakweli ndiyo wakapigwa chini. kumbuka ni awamu ya kusifiwa tu!
Au namna sahihi ya kudai tax arrears bila ya kufungia biashara maana body ndio inatoa maelekezo ya approaches jinsi ya kufanya mambo ndani ya taasisi kwa mujibu wa sheria.
 
Back
Top Bottom