Karma: Aliyemsukumiza kijana barabarani, leo mwanae amekatwa mguu baada ya ajali ya bodaboda

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Inasikitisha sana ndugu zanguni. Nawaombeni wazazi wote tujifunze kupitia huyu mtu

Mimi ni mfanyabiashara wa duka la jumla la nafaka, mwenye frame inayofuata na yeye ni hivyo hivyo. Mwezi ulioisha kuna gari lilikwama mbele ya frame zetu. Sasa kukawa na Bajaj iliyokuwa inajaribu kupenyeza kurudi nyuma, muda huo huo kuna kijana alibebelea gunia la mchele akikatiza kwenye upenyo huo huo.

Wakati anaikaribia ile Bajaj, aliamua kujibana kuelekea upande ambao wa frame ya jirani yangu, huyu jirani yangu alimsukumiza kijana kwa mgongo, yule kijana katika hali ya kuyumba yumba, alishtukia mguu wake umekanyagwa na Bajaj ile iliyokuwa na magunia kadhaa ya unga kwenye bodi

Kijana aliangua kilio kisicho na kifani, huku mifupa ya kikanyagio chake cha mguu ikiwa nyang'a nyag'a. Jirani yangu alijibu kwa jeuri kuwa kwani alikuwa anawahi nini. Tukio ni la mwezi ulioisha

Juzi kati, mtoto wa kike wa huyo jirani yangu alipakizwa kwenye bodaboda kama ilivyo ada ya kupelekwa shuleni kwa usafiri wa kitajiri. Taarifa mbaya zilitufikia kuwa bodaboda imepata ajali ilipokuwa inafanya juhudi ya kukwepa tandam ya Mahindi. Cha kushangaza bodaboda alichubuka vibaya sana na asivunjike, lakini mtoto alivunjika miguu yote na kuwa pingili pingili. Tulimbeba mgonjwa wetu na kumpeleka hospitali

Leo asubuhi wakati nafungua kijiduka changu cha kimaskini, ndipo kupata taarifa kuwa mguu mmoja wanaunofoa kabisa

Funzo: Malipo yote ni hapahapa duniani. Tenda yale unayopenda kutendewa na wenzio. Epuka matendo maovu ili usije kuingiza wasiohusika kwenye karma yako

Kosa lake yeye, karma kwa mtoto. Inasikitisha sana aisee. Nani atamuoa?

Pia soma: Kama mwenyezi Mungu atatupilia mbali suala la laana na karma, watakaoingia kwenye adhabu ya milele watakuwa wameonewa bure
 
Kuna siku nikiwa nna miaka 15 natokea ddc keko naelekea keko machungwa kile kibonde chakutoka magereza kuelekea kwakina mbwana matumla nikaskia kelele za mayowe yamwizi yule mwizi alikuwa anakuja kwakukimbia anapandisha mimi nashuka yule mwizi alikuwa kawaacha wananchi hatua zakutosha nanajua alikuwa anakimbilia kujisalimisha juu pale magereza sasa ile ananikatibia tu mi nikajifanya kama nimemkwepa akajua dogo ananiogopa

Ile kunivuka hatua moja tu nikaingiza mguu wangu kwenye mguu wake mmoja aliounyanyua hivyo mguu wangu ukawa kati kati yamiguu yake akajigonga pale pale akadondoka nikawa kama nimempotezea dk kazaa naile ananyanyuka tu wananchi wakawa wamefika dah ili tukio huwa linaniumaga sana kwenye maisha yangu naumia huwa naomba msamaa kila niendapo nyumba ya ibada huwa naamini mimi ndio sos yayule mwizi kufa
 
Usiogope maana imeandikwaa hata wabaya na wema wanahaki ya kuishi na kutumia mema ya inchiiii
 
Karma kitu gan na wewe, watanzania na Iman za kijinga jinga.

Kwani huyo mtoto anahusikaje?
Kwanini huyo mzee aisumie yeye...

Life is a game of chance.... yeyote anaweza pata lolote..

Waamini wa nchi hii huwa wanatafuta excuse ya ku justify Imani potofu.

Karma would have sound better if at all it was a coin for a coin, sio hii unayosema wewe.

Adios.
 
Kuna siku nikiwa nna miaka 15 natokea ddc keko naelekea keko machungwa kile kibonde chakutoka magereza kuelekea kwakina mbwana matumla nikaskia kelele za mayowe yamwizi yule mwizi alikuwa anakuja kwakukimbia anapandisha mimi nashuka yule mwizi alikuwa kawaacha wananchi hatua zakutosha nanajua alikuwa anakimbilia kujisalimisha juu pale magereza sasa ile ananikatibia tu mi nikajifanya kama nimemkwepa akajua dogo ananiogopa

Ile kunivuka hatua moja tu nikaingiza mguu wangu kwenye mguu wake mmoja aliounyanyua hivyo mguu wangu ukawa kati kati yamiguu yake akajigonga pale pale akadondoka nikawa kama nimempotezea dk kazaa naile ananyanyuka tu wananchi wakawa wamefika dah ili tukio huwa linaniumaga sana kwenye maisha yangu naumia huwa naomba msamaa kila niendapo nyumba ya ibada huwa naamini mimi ndio sos yayule mwizi kufa
Dah wewe jamaa umenikumbusha mbali sana hiyo mitaa .

Nimejikuta keko tena , mitaa yangu ilikuwa hapo kwenye Saccos ya magereza nikipenda kuangalia mpira maeneo hayo kwa dogo mmoja anaishi nyuma ya kota za magereza .

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Kuna siku nikiwa nna miaka 15 natokea ddc keko naelekea keko machungwa kile kibonde chakutoka magereza kuelekea kwakina mbwana matumla nikaskia kelele za mayowe yamwizi yule mwizi alikuwa anakuja kwakukimbia anapandisha mimi nashuka yule mwizi alikuwa kawaacha wananchi hatua zakutosha nanajua alikuwa anakimbilia kujisalimisha juu pale magereza sasa ile ananikatibia tu mi nikajifanya kama nimemkwepa akajua dogo ananiogopa

Ile kunivuka hatua moja tu nikaingiza mguu wangu kwenye mguu wake mmoja aliounyanyua hivyo mguu wangu ukawa kati kati yamiguu yake akajigonga pale pale akadondoka nikawa kama nimempotezea dk kazaa naile ananyanyuka tu wananchi wakawa wamefika dah ili tukio huwa linaniumaga sana kwenye maisha yangu naumia huwa naomba msamaa kila niendapo nyumba ya ibada huwa naamini mimi ndio sos yayule mwizi kufa
Ulifanya kazi ya Kizalendo kabisa, ilikuwa ni muda wa kulipia uhalifu alioufanya na wewe ulitumika kama chombo tu kukamilisha safari yake.
Jambo baya ni ile mtu asiye na hatia kabisa ateseke kwaajili yako.
 
Kuna siku nikiwa nna miaka 15 natokea ddc keko naelekea keko machungwa kile kibonde chakutoka magereza kuelekea kwakina mbwana matumla nikaskia kelele za mayowe yamwizi yule mwizi alikuwa anakuja kwakukimbia anapandisha mimi nashuka yule mwizi alikuwa kawaacha wananchi hatua zakutosha nanajua alikuwa anakimbilia kujisalimisha juu pale magereza sasa ile ananikatibia tu mi nikajifanya kama nimemkwepa akajua dogo ananiogopa

Ile kunivuka hatua moja tu nikaingiza mguu wangu kwenye mguu wake mmoja aliounyanyua hivyo mguu wangu ukawa kati kati yamiguu yake akajigonga pale pale akadondoka nikawa kama nimempotezea dk kazaa naile ananyanyuka tu wananchi wakawa wamefika dah ili tukio huwa linaniumaga sana kwenye maisha yangu naumia huwa naomba msamaa kila niendapo nyumba ya ibada huwa naamini mimi ndio sos yayule mwizi kufa
dah inahuzunisha sana mkuu ila ndoivo we ndo ulikuwa nafasi ya kumuokoa lakini ndoivo..dah niko nasikiza wimbo wa angera-bless ,
 
Kama watu wanaamini katika karma sijui kama basi watueleze yesu wakati anasurubiwa msalabani alikuwa analipa karma IPI,stephano wa biblia naye kufa kwakusurubiwa mijuu guu,alikuwa analipa karma ipi!?

Mimi hapa ninaishi maisha magumu no karma ipi nailipa!?

In upuuzi kuamini katika upuuzi
 
Sio Yesu pekee aliyesubiliwa zilikuwa ni hukumu za wayahudi hata kabla ya Yesu.
Yesu alichukua uovu wa wanaomuamini
 
Kuna siku nikiwa nna miaka 15 natokea ddc keko naelekea keko machungwa kile kibonde chakutoka magereza kuelekea kwakina mbwana matumla nikaskia kelele za mayowe yamwizi yule mwizi alikuwa anakuja kwakukimbia anapandisha mimi nashuka yule mwizi alikuwa kawaacha wananchi hatua zakutosha nanajua alikuwa anakimbilia kujisalimisha juu pale magereza sasa ile ananikatibia tu mi nikajifanya kama nimemkwepa akajua dogo ananiogopa

Ile kunivuka hatua moja tu nikaingiza mguu wangu kwenye mguu wake mmoja aliounyanyua hivyo mguu wangu ukawa kati kati yamiguu yake akajigonga pale pale akadondoka nikawa kama nimempotezea dk kazaa naile ananyanyuka tu wananchi wakawa wamefika dah ili tukio huwa linaniumaga sana kwenye maisha yangu naumia huwa naomba msamaa kila niendapo nyumba ya ibada huwa naamini mimi ndio sos yayule mwizi kufa
Siku zake zakufa zilifika Hawa wezi wakikukuta wanakumaliza wewe
 
Back
Top Bottom