Karma ya watani wa jadi (stori za vijiweni)

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
Karma ya watani wa jadi,

Karma is what?... Usimalizie bwana wapo watoto underage humu ambao matusi hayapaswi kuwa sehemu ya ukuaji wao.

Hivyo wacha turejee nyuma tuone ni kwanini wanazuoni waliona huo msemo unafaa...

Leo niko kijiwe cha kirumba sokoni, basi bwana wacha turejee mpaka mwaka 2012. Ambapo mashindano ya Kagame yalikuwa yamemalizika.

Kama kawaida ya wakubwa wetu hawa wa kariakoo (kile kitabia cha kumtaka mchezaji baada ya kucheza nae). Sababu ni scout mbovu na kutokuwa mikakati.

So baada ya mwamba kukiwasha vibaya mno alipokutana na vigogo hawa. Yeye akiwa APR aliwatoa udelele kwa performance yake. Kwa mjibu wa chanzo kisicho cha kuaminika ni kuwa wana Lunyasi ndio walikuwa wa kwanza kumfikia mwana wa kuitwa Mbuyu Twite.

Kama mwanasoka najua jina hili sio geni kwa sababu amekipiga jangwani kwa kiwango kikubwa mno. Ila story behind ya kwanini acheze jangwani na si msimbazi ilitikisa nchi.

Ilikuwa hivi; wana lunyasi kupitia kwa Isimaili Rage walidai kumsajili. Achana na kudai mpaka kwenye tamasha lao walilitaja jina lake mpaka namba ya jezi ya kuwa angeivaa namba nne. Kwa madai ya Rage ni kuwa

Wao ndio wa kwanza kugonga hodi APR ya Rwanda kutaka saini ya beki huyu. Aliyekuwa anarusha mpira kama Kona, aliyeweza kucheza nafasi nyingi uwanjani. Inasemekana lakini eti Mnyama alimalizana kila kitu na timu pamoja na mchezaji (ndio akajipa uhakika mpaka kumtambulisha plus namba ya jezi).

Wasichokijua ni upande wa pili wao walikuwa wakiwachora tu (kumbuka walikuwa chini ya Manji).

Siku ya siku mwamba si akadondoka Jiji la wazaramo ili msimbazi wamalizame mambo yaliyobaki. Unaambiwa kabla wana lunyasi hawajamchukua wakazungukwa na wana jangwani na kunasa saini ya Twite. Ambaye ilibidi arejeshe ile fee ya usajili. Aliyokuwa amepewa awali na Simba.

Fast forward mpaka dirisha hili la usajili 2023 miaka karibia kumi mbele. Wana Lunyasi nao wakafanya malipizi. Ndio maana Karma ikaitwa .... Haikujalisha miaka mingapi imepita.

Za vijiweni hapa zinasema kuwa ile namba sita iliyopigiwa kelele sio ile tunayoiona. Achana na amapiano bwana kumbe namba sita mwenyewe alikuwa ni yule mkongomani aliyetua upande wa pili. Inasemekana wananchi walibadiri gia angani na kumpa winga namba ile (namba inaweza kuvaliwa na yeyote lakini winga kuvaa namba sita...!).

Kwa vyanzo visivyokuwa vya kuaminika vinasema kuwa na wao walifanyiwa walichowafanyia mwaka 2012. Kwani tayari wananchi walikuwa wameongea na kufikia makubaliano ya awali na yule mwamba mwenye mapasi yake.

Kilichokuwa kimebakiza ni mazungumzo na timu aliyokuwa anachezea. Kama ni mfatiliaji utagundua kuwa mwana alikuwa na kesi yeye na timu yake kule kwenye vita Sasa. Walichokisahau ni wenzao kuanzia kwenye timu kisha wakamaliza kwa mchezaji.

Mwamba alipotua kwenye jiji la wazaramo hapo ndipo wana lunyasi walipowapiga changa la macho kwa kuwapokonya mchezaji wao pale terminal III.

Karma is karma je, lipo tukio lingine kama hili unalolijua kwa vilabu vyetu pendwa....!!
twite%25203.jpg
342758b6315f11dce280a9a294d4a2fa.jpg
 
Back
Top Bottom