Kuna haja ya Kuruhusu JWTZ - Operation Kibiti?

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Wakuu ni wazi kuwa tunakoelekea Sasa Tanzania inaface insecurity kama Kenya Ambapo Askari wana popolewa kila na Alshaabab

Namshauri Rais na Timu yake ni wakati wa Kutumia Elite Special special force kama ya JWTZ Nina Imani tutauangamiza Mtandao wa Wahalifu hasa eneo la Kibiti.

Tumechoka na watu wanaua Askari wanapora silaha 8, Halafu siku hiyo hiyo Mtu anakuja kudanganya kwenye media kuwa tumeyakamata silaha ni kweli Unapunguza tension kwa wananchi lakini Mioyoni mwenu Mnajua Kua hamjakamata Silaha yeyote.

Pia Kiwepo kikosi cha Kuchunguza kwa Nini wanaouwawa ni watu wenye mahusiano ya Moja kwa Moja na Chama cha Mapinduzi Chuki hii imesababiswa na Nini na Imeanzia wapi?

Nina amini Military Operation ya JWTZ itazaa Matunda kwanza huwa wako friendly sana na Raia ulilinganisha Polisi.

Hata Nchi Za Uingereza Ni Mara Kibao (Special Air Services) SAS na US Marine na Navy Seal Wanatumika kwenye Majanga Mbalimbali.


1_2.jpg
View attachment 511126
1423903222944.jpeg
 
Bado unaendelea kushauri nguvu na kutisha watu ndio vitumike kuliko akili, nafikiri wangefanya utafiti wakujua chanzo cha hayo mauaji kwanza, wajue ni nani/ kikundi gani kinahusika na wanatumia mbinu gani kutekeleza hayo mauaji. Jeshi sio mchezo ndugu yangu wakienda hapo itakua ni mwendo wa amri tu, kumbuka wanaouawa ni viongozi sio wananchi wa kawaida.
 
Jeshi lina utaalam wakukusanya inteligence kwaajili ya vita. Sidhani kama kuhoji raia ni taaluma yao.
Kwenye hilihili jeshi la polisi kuna watu sema vipaumbele vya viongozi wao ndio vinaweza kuwa tatizo.

Nakumbuka kuna askari mmoja alimkomalia mke wa mheshimiwa flani hivi kwa issue ya sheria barabarani ikasemekana apandishwe cheo.
Sasa imagine anakutana na msala kama huu!!!!
Siasa imeliharibu sana jeshi la polisi.
Ukimkomalia Manji akalala ndani unapanda cheo.
Ukimkomalia Mbowe, unakula mbavu tatu.
Ukimkamata Lema kibabe, mkuu anakupandisha cheo mwenyewe!

Hapo ndio utakuta misfit leaders kibao kwenye jeshi!
Hili jeshi lililoko sasahivi lisivunjwe, lifanywe blue gurd, vichambuliwe vichwa vinavyojitambua tuunde jeshi linalojali qualifications na professionalism.
 
Kule inatakiwa waende kikosi kazi cha JWTZ wakasafishe majambazi na wakae na wananchi ili wawape ushirikiano , ,,,police wao tuwaachie mambo ya upinzani na ishu zingine ,,,, haiwezekani mpaka leo watu wanakufa tu majambazi wanatamba ,,ina maana intelejensia imeshindwa kufanya kazi yake,,, kule wapelekwe Jeshi la ulinzi na askari wawapelelezi wa kujichanganya na raia kupata detail
 
Isije ikatokea kama watu wa mtwara walivyopigika

Sawa liende lakini litumie uweledi ,taaluma na sio kuonea raia lakini pia itakuwa dharau kwa jeshi la police

Umeweka amri mwisho kulala saa 12 watu wametii lakini mwenyekiti kauliwa saa tano usiku hivyo hajaacha trace yeyote ile kaondoka kwa kujinafasi.




Kwani hao wauaji hawatumii simu hawawasiliani?usalama wanafanya kazi gani

Kwani viongozi wasipewe ulinzi?
Kama yule mwenyekiti angekuwa na ulinzi huyo muuaji angejulikana na kukamatwa
 
Hivi karibuni utamsikia siro anasema wamewaua majambazi watatu maeneo ya kibiti na kabla ya kufa majambazi yalikua yanasema ALLAH AKBAR,Kibiti boys sio kina ADAM MALIMA wakiendelea na mbinu zao za kukamata mateja kinondoni manyanya watakufa ovyo.The guys are well organized and equiped,waacheni wajeda wakapashe misuli moto
 
Troll JF,
Nadhani ulichoandika hapa juu ya kutumia JWTZ ni sawa kabisa na mada yako uliyoandika juu ya graduates kujiajiri kwenye kilimo Kwa kutumia mfano wa Dr. Kikwete.

Hasa pale , ulipolinganisha graduates na rais msitafu, Dr . Kikwete kuwa yeye analima basi na graduates wakalime waachane na kutembea na bahasha au kujitolea ofisini.

Kwa kifupi , hujui uandikacho na hujui na labda hufahamu implication yake katika image ya nchi Kwa kutumia JWTZ katika operation hiyo .

Ama unajua lakini unajitoa ufahamu.
 
Bado unaendelea kushauri nguvu na kutisha watu ndio vitumike kuliko akili, nafikiri wangefanya utafiti wakujua chanzo cha hayo mauaji kwanza, wajue ni nani/ kikundi gani kinahusika na wanatumia mbinu gani kutekeleza hayo mauaji. Jeshi sio mchezo ndugu yangu wakienda hapo itakua ni mwendo wa amri tu, kumbuka wanaouawa ni viongozi sio wananchi wa kawaida.
Mapolisi wa tanzania ni majing ajinga sana... hayana akili hata moja... hayajui namna ya kusolve situation na kutengeneza mahusiano na wananchi wao wanachoelewa ni kupiga pingu na kupiga watu tanganyika jeki..... yan hata kama hujaresist arrest yanakutwanga tu makofi.... yan kama yamesetiwa iv..
 
apana hii ni kaz ya police pale itakapo onekana kuwa swala hili limewashnda polisi ndo wanaweza wakaingia wazee wa kaz wa kishirikiana na polisi wenyewe lakn 2tambue mgawanyo wa kaz kila jeshi na kaz yake akuna kuingilia majukum otherwise kuwe na dhalula sana ya kulazmika kufanya hvyo
 
Nguvu pekee haitoshi kutatua tatizo, mnatakiwa mlielewe hilo.. Jeshi la Wananchi litaenda kufanya kipi cha ziada..? Hakuna adui anaeonekana akiwa na silaha nzito za kijeshi akishambulia polisi na wananchi huko.. Tukubali tu weledi wa Jeshi letu la Polisi katika kupambana na uhalifu umeshuka sana.. Kwenye kukusanya intelejensia Polisi wamefeli vibaya sana hapo.. Tuombe msaada kama tulivyowahi kuomba huko nyuma toka Scotland yard, waje kusaidia..
 
Mapolisi wa tanzania ni majing ajinga sana... hayana akili hata moja... hayajui namna ya kusolve situation na kutengeneza mahusiano na wananchi wao wanachoelewa ni kupiga pingu na kupiga watu tanganyika jeki..... yan hata kama hujaresist arrest yanakutwanga tu makofi.... yan kama yamesetiwa iv..
Mkuu tusiwahukumu, sio wote wengine wana ubinadamu sana, tena wana utu na wameridhika na mishaahara yao. Mfano juzi wakati Malima anafokeana na yule askari aliyepiga risasi,ukiangalia yule askari mwingine alikua anamsihi mwenzake kutulia na kutokufyatua risasi. Afu pia wanapewa amri tu na hawaruhusiwi kupinga hiyo amri,
 
Back
Top Bottom