Kuna daladala zinaonekanaga kuanzia saa 6 usiku mpaka 11 alfajir

Nyingine hazina taa kabisa zinategemea mataa ya barabarani

Ila zinatuokoa kinoma usiku aisee kwa hapa dar, yani unapiga vyombo unajua hata saa 9 usiku hukosi gari ya kurudi kitaa.
Hahahahahaaa noma sana mkuu
 
Enzi za 2012 kurud nyuma dar njia ya sinza kariakoo au sinza magomen kariakoo ikifika saa moja zinaingia Hiace Kali mziki mnene huku wamefungulia magic fm tunakula Kwetu fleva na Dj majaa majee majii majizo foshzo saiz nae boss kaajiri watangazaji na madj.

Enzi hzo kutoka ubungo mpaka magomen pembeni na katikat ya barabara Kuna miti
 
Uzuri hazina ruti maalum, abiria mnaoenda eneo fulani mkiwa wengi mnapelekwa chap.

Kuna siku saa 8 usiku pale ubungo nikaigumia hiace moja basi ile kupanda tu hatujakaa sawa wajeda kama watano hao nao wakaja kupanda, wakamwambia kondakta usiwe na wasi wote tutakulipa nauli!

Ikawa ahueni maana kondakta mwanzoni alibaki katumbua macho hajui la kufanya
 
Back
Top Bottom