Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 98,027
- 142,937
Julius,'
Kuna mengi ya kujifunza kutoka Chile. To always be ready for the emergency na spirit ya self reliance. Nimewakubali.
Ni kweli wamejiandaa ila kama sikosei hili tetemeko halijapita katikati ya mji na limepita pembezoni kidogo, hapo ni pa kumshukuru Mungu pia kama linge hit capital nadhani sasa ingekuwa habari nyingine!
ha, mrembo, kumbe kwa analysis na wewe umo?................ angalau umeanalyse critically................ unajua niko well coversant na human settleent issues, sasa waliotangulia wameignore urban development and human settlement factors.............. kaazi kwelikweli............... kamata mvinyo hapo kwa afta yako...........
Kidogo najaribu mwayego vipi ishu yako hujatupa feedback lol🙄
kiongozi mimi mambo ya chile siko deep...!ILA HILO JINA ULILORUDISHA NDO NIMEKUBALI NA NIMEHAMASIKA KUPOST SREDI😀😀Tetemeko lililotokea jana huko Chile ni moja ya matetemeko makubwa sana kutokea duniani. Vipimo vyake vilikuwa 8.8 kwenye mzani wa Richter. Hakika hili lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile la Haiti lililotokea mwezi uliopita ambalo vipimo vyake vilikuwa 7.0
Cha kushangaza hili la Chile inaonekana maafa yake hayatakuwa makubwa sana ukilinganisha na lile la Haiti. Hii pengine ni kwa sababu Chile ilikuwa imejiandaa vya kutosha na janga kama hili kwa sababu ya uwepo wake kwenye ule ukanda wa ring of fire kwenye bahari ya Pacific ambako matetemeko mengi ya ardhi hutokea. Maandalizi hayo yanaelekea yameweza kuepusha maafa makubwa zaidi ya yaliyotokea.
Mpaka sasa Chile hawajaomba msaada kutoka kwa yeyote yule, si Marekani wala majirani zao Argentina. Bila shaka wana uwezo na ujuzi wa kutosha kukabiliana na kilichotokea.
Sasa nimekaa hapa nikakumbuka Mzee Mwanakijiji hupenda kusema taifa lisilojiandaa kwa majanga hujiandaa kwa maafa. Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.
Tetemeko lililotokea jana huko Chile ni moja ya matetemeko makubwa sana kutokea duniani. Vipimo vyake vilikuwa 8.8 kwenye mzani wa Richter. Hakika hili lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile la Haiti lililotokea mwezi uliopita ambalo vipimo vyake vilikuwa 7.0
Cha kushangaza hili la Chile inaonekana maafa yake hayatakuwa makubwa sana ukilinganisha na lile la Haiti. Hii pengine ni kwa sababu Chile ilikuwa imejiandaa vya kutosha na janga kama hili kwa sababu ya uwepo wake kwenye ule ukanda wa ring of fire kwenye bahari ya Pacific ambako matetemeko mengi ya ardhi hutokea. Maandalizi hayo yanaelekea yameweza kuepusha maafa makubwa zaidi ya yaliyotokea.
Mpaka sasa Chile hawajaomba msaada kutoka kwa yeyote yule, si Marekani wala majirani zao Argentina. Bila shaka wana uwezo na ujuzi wa kutosha kukabiliana na kilichotokea.
Sasa nimekaa hapa nikakumbuka Mzee Mwanakijiji hupenda kusema taifa lisilojiandaa kwa majanga hujiandaa kwa maafa. Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.
Ni kweli wamejiandaa ila kama sikosei hili tetemeko halijapita katikati ya mji na limepita pembezoni kidogo, hapo ni pa kumshukuru Mungu pia kama linge hit capital nadhani sasa ingekuwa habari nyingine!
ha, mrembo, kumbe kwa analysis na wewe umo?................ angalau umeanalyse critically................ unajua niko well coversant na human settleent issues, sasa waliotangulia wameignore urban development and human settlement factors.............. kaazi kwelikweli............... kamata mvinyo hapo kwa afta yako...........
Kuna mengi ya kujifunza siyo tu kutoka Chile bali hata kutoka Haiti kutokana na matetemeko haya. Kubwa ni kuwa tunatakiwa kujenga utamaduni wa kuwa na plan B kutokana na ukweli kuwa maafa mengi ya asili kama vile matetemeko, mafuriko vimbunga, volcano na kadhakli hutokea bila kutoa taarifa.
Hata hivyo madai yako kuwa tetemeko la Chile ambalo lilipima Richter 8.8 liltakiwa lilete madhara makubwa zaidi kuliko lile la Haiti ambalo lilikuwa Richter 7.0 siyo sahihi kabisa katika kupima madhara ya matetemeko. Hiyo Richter scale inayotumika kukokotoa nguvu ya tetemeko inaunganisha mambo mawili: urefu wa mtikisiko wa ardhi kwenda juu na chini (vertical amplitude) na urefu wa juu ya ardhi au ukubwa wa eneo lililotikisika. Inawezekana mtikisiko wa kwenda juu usiwe mkubwa lakini ukawa umetopkea katika eneo kubwa sana hivyo Richter magnitude ikawa ni kubwa sana pia, na vile vile inawezekana mtikisiko ule ukawa ni mkubwa sana wa kutisha lakini ukawa umetokea eneo dogo tu hivyo Richter magnitude yake ikawa siyo kubwa sana. Kwa sasa hivi wataalamu wa seismology wanashughulika ili kuweka kipimo sahihi zaidi cha madhara ya tetemeko locally badala ya yiyo Richter ambayo inapima nguvu ya tetemeko katika eneo kubwa (distributed.)
Pamoja na ubovu wa infrastructure na standards za majengo ya Haiti, kumbuka kuwa ile ikulu yao ilikuwa imejengwa imara sana kuhimiri matetemeko kwa standards za kisasa sawa na zinazutumika eneo lote lile including Chile. Hata hivyo Ikulu ile bado ilianguka wakati nyumba za aina hiyo huko Chile hazikuanguka. Tofauiti hapa ni kuwa mtikisoko wa Haiti ulikuwa ni wa nguvu sana kuliko ule wa Chile, ila ulitokea kwenye eneo dogo tu la mji wa Port Au Prince.wakati lile la Chile halikuwa na nguvu kama zile za Haiti lakini lilitokea katika eneo kubwa sana tena ndani ya maji.
My 50cents napendekeza Serikali yetu ijufunze yafuatayo:
1.Physical Planning (both to urban and rural)
2.Ku-enforce building code (kama ipo)
3.Environment Protection (enforcement)
4.Public Education and awareness campaign
5.Kitengo/Kikosi cha maafa kiondolewe OPM.......Kiundwe Kikosi/Kitengo Maalum kitakachoshughulikia maafa (Kambi za JKT zaweza kutumika kama centres za vikosi hivyo).....Kikosi hicho kishughulikie ku-enforce hayo hapo juu
6.Serikali Itenge resources kuhakikisha hayo hapo juu yanatimia ikishirikiana na private sectors
Tetemeko lililotokea jana huko Chile ni moja ya matetemeko makubwa sana kutokea duniani. Vipimo vyake vilikuwa 8.8 kwenye mzani wa Richter. Hakika hili lilikuwa kubwa zaidi kuliko lile la Haiti lililotokea mwezi uliopita ambalo vipimo vyake vilikuwa 7.0
Cha kushangaza hili la Chile inaonekana maafa yake hayatakuwa makubwa sana ukilinganisha na lile la Haiti. Hii pengine ni kwa sababu Chile ilikuwa imejiandaa vya kutosha na janga kama hili kwa sababu ya uwepo wake kwenye ule ukanda wa ring of fire kwenye bahari ya Pacific ambako matetemeko mengi ya ardhi hutokea. Maandalizi hayo yanaelekea yameweza kuepusha maafa makubwa zaidi ya yaliyotokea.
Mpaka sasa Chile hawajaomba msaada kutoka kwa yeyote yule, si Marekani wala majirani zao Argentina. Bila shaka wana uwezo na ujuzi wa kutosha kukabiliana na kilichotokea.
Sasa nimekaa hapa nikakumbuka Mzee Mwanakijiji hupenda kusema taifa lisilojiandaa kwa majanga hujiandaa kwa maafa. Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.
Nyani,Binafsi kwa kweli nimevutiwa na jinsi Chile walivyokabiliana na wanavyoendelea kukabiliana na janga hili. Inavyoelekea hata majengo yao yamejengwa imara kuweza kuhimili matetemeko makubwa kama hili la jana. Sasa sijui sisi kama taifa tumejifunza nini kutoka Chile jinsi ya kujiandaa na majanga haya ya asili.