Mshua wangu ameomba msaada kwa jamaa mmoja ambaye ni mzoefu kuagiza magari toka Japan. Katika pita pita yake net akakutana na ka suzuki swift ka mwaka 2003, engine cc 1300, FOB USD 1,200, akauliza CIF to dar ikajibiwa na jamaa wanaouza gari ni USD 2450. Hapo kwa kukosa uzoefu akaona bora atafute msaada wa huyo mzoefu. Huyo mzoefu katoa mchanganuo ufuatao
1.CIF = USD245
2.Paytrade = USD 150
3. Bank charges CRDB=USD 50
Mshua wangu tayari kesha mpa Tshs.4,000,000/= kuagiza hilo gari, sasa wanavutana na huyo mzoefu juu kiasi atakchopaswa kulipa kama kodi baada ya gari kuwasili Bandarini, mzoefu anadai atatakiwa kulipa 3.5M, na mshua anasema kwa hesabu zake kodi ni 1,872,000/=
Mimi nimejaribu kupita thread moja humu Jf ila hesabu zimenishinda, naomba wajuzi mnisaidie ili niepushe hili zogo, ukizingatia mie ndo nilitoa wazo la kimwomba huyo mzoefu maana asije akaona nami nimshiriki kulamba cha juu. Msaada tafdhali