Zacht
JF-Expert Member
- Jul 17, 2020
- 1,009
- 2,197
Hebu fikiria unaokota saa jangwani ungehitimisha kwa kufikiri nini? Je, ungedhani kuwa mtu amedondosha saa hio? Au ungedhani kuwa saa hiyo ilikuja yenyewe?
Kwa kweli hakuna mtu mwenye akili timamu atakayesema kuwa saa hiyo ilitokea tu katika mchanga. Saa hio lazima iwe na mtengenezaji. Ikiwa saa inasema wakati sahihi tunatarajia mtengenezaji lazima awe na akili. kipofu haiwezi kutoa saa inayofanya kazi.
Fikiria kuchomoza kwa jua na kuzama muda wao umedhibitiwa sana ni nani anayedhibiti majira ya kuchomoza na kuchwa kwa jua? Ikiwa saa haiwezi kufanya kazi bila mtengenezaji mwenye akili timamu, jua linawezaje kuonekana kuchomoza na kuzama kama saa? Je! Hii inaweza kutokea yenyewe?
Fikiria pia kwamba tunafaidika na jua kwa sababu linakaa katika umbali ulio salama kutoka duniani, umbali ambao una wastani wa maili milioni 93. Kama jua lingekaribia zaidi, basi dunia ingeungua. Na kama lingekuwa mbali sana, dunia ingegeuka barafu na kufanya maisha ya wanadamu na viumbe wengine hapa yasiwezekane.
Nani aliamua mapema kuwa huu ulikuwa umbali sahihi? Je, inaweza kutokea kwa bahati tu? Bila jua, mimea isingekua. Kisha wanyama na wanadamu wangekufa na njaa. Je! Jua liliamua tu kuwa huko lenyewe?
Miale ya jua ingekuwa hatari kwetu kama kusingekuwa na kinga katika anga letu (ozone layer). Ambayo inazuia miale hatari ya jua isitufikie. Ni nani aliyeweka ngao hii karibu itukinge sisi ? Au nalo imetokea kwa bahati kama jua?
Tunahitaji kupata jua, tunahitaji nishati ya jua na nuru yake ili kuona wakati wa mchana. Lakini pia tunahitaji machweo. Tunahitaji joto, tunahitaji baridi la usiku na tunahitaji kiza ili tupate kulala(kupumzika). Nani aliye yapangilia mahitaji yetu?
Haiwezekani vitu hivi vyote vikatokea kwa bahati nasibu eti jua likakaa umbali ambao hatuta athirika nalo , ozone layer nayo ikatokea kwa bahati nasema haiwezekani na haingii akilini kwa mwenye kufikiri vizuri na kwa utulivu.
Muumba ambaye alitupa mwanga, nguvu, ulinzi na uzuri anastahili shukrani zetu. Hata hivyo kuna watu wanasisitiza kwamba hayupo. Je! Wangefikiria nini ikiwa wangepata saa jangwani? Saa sahihi na inayofanya kazi? Saa iliyoundwa vizuri?
Je, hawatahitimisha kwamba kuna mtengenezaji wa saa? Mtengenezaji wa saa mwenye akili? Mtu anayethamini uzuri? Huyu ndiye Mungu aliyetuumba.