Kuna aliyepangilia mambo haya, hayakufanyika kwa bahati nasibu

Zacht

JF-Expert Member
Jul 17, 2020
1,009
2,197
Hebu fikiria unaokota saa jangwani ungehitimisha kwa kufikiri nini? Je, ungedhani kuwa mtu amedondosha saa hio? Au ungedhani kuwa saa hiyo ilikuja yenyewe?

Kwa kweli hakuna mtu mwenye akili timamu atakayesema kuwa saa hiyo ilitokea tu katika mchanga. Saa hio lazima iwe na mtengenezaji. Ikiwa saa inasema wakati sahihi tunatarajia mtengenezaji lazima awe na akili. kipofu haiwezi kutoa saa inayofanya kazi.

Fikiria kuchomoza kwa jua na kuzama muda wao umedhibitiwa sana ni nani anayedhibiti majira ya kuchomoza na kuchwa kwa jua? Ikiwa saa haiwezi kufanya kazi bila mtengenezaji mwenye akili timamu, jua linawezaje kuonekana kuchomoza na kuzama kama saa? Je! Hii inaweza kutokea yenyewe?

Fikiria pia kwamba tunafaidika na jua kwa sababu linakaa katika umbali ulio salama kutoka duniani, umbali ambao una wastani wa maili milioni 93. Kama jua lingekaribia zaidi, basi dunia ingeungua. Na kama lingekuwa mbali sana, dunia ingegeuka barafu na kufanya maisha ya wanadamu na viumbe wengine hapa yasiwezekane.

Nani aliamua mapema kuwa huu ulikuwa umbali sahihi? Je, inaweza kutokea kwa bahati tu? Bila jua, mimea isingekua. Kisha wanyama na wanadamu wangekufa na njaa. Je! Jua liliamua tu kuwa huko lenyewe?

Miale ya jua ingekuwa hatari kwetu kama kusingekuwa na kinga katika anga letu (ozone layer). Ambayo inazuia miale hatari ya jua isitufikie. Ni nani aliyeweka ngao hii karibu itukinge sisi ? Au nalo imetokea kwa bahati kama jua?

Tunahitaji kupata jua, tunahitaji nishati ya jua na nuru yake ili kuona wakati wa mchana. Lakini pia tunahitaji machweo. Tunahitaji joto, tunahitaji baridi la usiku na tunahitaji kiza ili tupate kulala(kupumzika). Nani aliye yapangilia mahitaji yetu?

Haiwezekani vitu hivi vyote vikatokea kwa bahati nasibu eti jua likakaa umbali ambao hatuta athirika nalo , ozone layer nayo ikatokea kwa bahati nasema haiwezekani na haingii akilini kwa mwenye kufikiri vizuri na kwa utulivu.

Muumba ambaye alitupa mwanga, nguvu, ulinzi na uzuri anastahili shukrani zetu. Hata hivyo kuna watu wanasisitiza kwamba hayupo. Je! Wangefikiria nini ikiwa wangepata saa jangwani? Saa sahihi na inayofanya kazi? Saa iliyoundwa vizuri?

Je, hawatahitimisha kwamba kuna mtengenezaji wa saa? Mtengenezaji wa saa mwenye akili? Mtu anayethamini uzuri? Huyu ndiye Mungu aliyetuumba.
 
Wenzako tumejadili sana haya makitu humu zaidi ya miaka mitano sasa.

Huu mfano wako wa saa hauna tofauti na huyo Mungu. Ukisema hajaumbwa utakuwa upo sawa na aliyeokota saa akasema hii saa imetokea tu from nowhere pasipo na muundaji wake.

Sawa, tukubaliane yupo mpangaja. Bila shaka mpangaji amepangiliwa vyema kuliko alivyovipanga.

Tuchukulie mfano wa haraka haraka. Kama muumbaji aliweza kufikiri na kuumba vitu vyenye akili na visivyo na akili, vyenye uhai na visivyo na uhai, vilivyoko kwenye mahesabu makali na vingine vilivyokaa shagala bagala kwanini naye asiwe na chanzo chenye maarifa kuliko yeye?

Kama umeutazama uumbaji ulivyo wa utata ukafikia kukubali lazima kuwe na aliyeumba, moja kwa moja muumbaji nae atahitaji awe ameumbwa kwa sababu yeye ni wa utata kuliko huu uumbaji wenyewe! Yeye ni wa maajabu zaidi kuliko uumbaji ulivyo wa maajabu.
Kama ni computer, basi yeye atakuwa ni super computer Kuliko computer sisi.

Je, utakubali kwamba muumbaji nae ameumbwa? Kadhalika kama ameumbwa, vivyo hivyo aliyemuumba nae atatakiwa awe ameumbwa pia.

Kama sisi na ulimwengu tumepatikana kutokana na ufahamu wa Mungu aliye tuumba, basi huyo Mungu nae haiwezekani awe ametokea tu from nowhere asiwe ametokana na fahamu zilizo juu ya uwezo wake pia.

Huu mlolongo hauna mwisho kama utataka kulazimisha kwamba tumeumbwa!

Umejitazama wewe ulivyo wa maajabu pamoja na mazingira akili yako ikagoma kabisa kwamba lazima kuwe na aliyekuumba wewe pamoja na hayo mazingira. Kwanini basi useme aliyeviumba hivi vyote hana mwanzo wala mwisho?

Je, mtu mwenye akili nyingi kama yeye aweza kutokea tu pasipo na chanzo kilichomleta yeye pamoja na maarifa yaliyomjaa kiasi hicho hadi kufikia kuumba mambo ya kutisha kama tuyaonayo?

Tafakari utagundua bado hatujui kitu bado.

Vitabu vilivyoletwa na waliotugeuza watumwa na wakatufunga minyororo visiwe sababu ya kufunga fahamu zetu.
 
Ahimidiwe yeye aliye juu ya vitu vyote, Mwenyezi Mungu Muumbaji
 
Hebu fikiria unaokota saa jangwani ungehitimisha kwa kufikiri nini? Je! Ungedhani kuwa mtu amedondosha saa hio? Au ungedhani kuwa saa hiyo ilikuja yenyewe?
Mfano wa saa hauna uhusiano na uwepo au kutokuwepo kwa Mungu.
 
Wenzako tumejadili sana haya makitu humu zaidi ya miaka mitano sasa.

Huu mfano wako wa saa hauna tofauti na huyo Mungu. Ukisema hajaumbwa utakuwa upo sawa na aliyeokota saa akasema hii saa imetokea tu from nowhere pasipo na muundaji wake.

Sawa, tukubaliane yupo mpangaja. Bila shaka mpangaji amepangiliwa vyema kuliko alivyovipanga.

Tuchukulie mfano wa haraka haraka. Kama muumbaji aliweza kufikiri na kuumba vitu vyenye akili na visivyo na akili, vyenye uhai na visivyo na uhai, vilivyoko kwenye mahesabu makali na vingine vilivyokaa shagala bagala kwanini naye asiwe na chanzo chenye maarifa kuliko yeye?

Kama umeutazama uumbaji ulivyo wa utata ukafikia kukubali lazima kuwe na aliyeumba, moja kwa moja muumbaji nae atahitaji awe ameumbwa kwa sababu yeye ni wa utata kuliko huu uumbaji wenyewe! Yeye ni wa maajabu zaidi kuliko uumbaji ulivyo wa maajabu.
Kama ni computer, basi yeye atakuwa ni super computer Kuliko computer sisi.

Je, utakubali kwamba muumbaji nae ameumbwa? Kadhalika kama ameumbwa, vivyo hivyo aliyemuumba nae atatakiwa awe ameumbwa pia.

Kama sisi na ulimwengu tumepatikana kutokana na ufahamu wa Mungu aliye tuumba, basi huyo Mungu nae haiwezekani awe ametokea tu from nowhere asiwe ametokana na fahamu zilizo juu ya uwezo wake pia.

Huu mlolongo hauna mwisho kama utataka kulazimisha kwamba tumeumbwa!

Umejitazama wewe ulivyo wa maajabu pamoja na mazingira akili yako ikagoma kabisa kwamba lazima kuwe na aliyekuumba wewe pamoja na hayo mazingira. Kwanini basi useme aliyeviumba hivi vyote hana mwanzo wala mwisho?
Kwa mujibu wa Biblia Mungu hana mwanzo wala mwisho. Kama wewe unaweza kututhibitishia kuwa ana mwanzo na mwisho, tusaidie tujue. Je tuamini hata hicho Biblia inasema au tuamini mafikara yako tu ambayo haya reference
Je, mtu mwenye akili nyingi kama yeye aweza kutokea tu pasipo na chanzo kilichomleta yeye pamoja na maarifa yaliyomjaa kiasi hicho hadi kufikia kuumba mambo ya kutisha kama tuyaonayo?

Tafakari utagundua bado hatujui kitu bado.

Vitabu vilivyoletwa na waliotugeuza watumwa na wakatufunga minyororo visiwe sababu ya kufunga fahamu zetu.

Nakuhakikishia kuwa Biblia au tuite maandiko ya Mungu yapo juu ya wazungu-beyond their thinking capacity
Ni kweli kabisa kuna watu wanatumia vibaya dini kujinufaisha.
Kuna hao wazungu walitumia dini kutufanya watumwa wao.
pia Kuna Wafrika wenzetu-hapa naongelea manabii na mitume -nyeo ambavyo wamejipachika wenyewe-ambao wenyewe kwa hiari na ujinga wetu tunawaamini bila kulazimishwa tunawapelekea hela na kuwatajirisha. Sisi tukiwa na shida wanatuombea, wao wakiwa na shida tunawachangia
Kakobe naye ni mzungu kwani-lakini ana watumwa pale anawatumia kupiga hela. Ana Mabilion ya hela benki anakula maisha
Mzee wa Upako yupo pale anapiga hela
.

Zaburi 139:14Nakusifu maana nimefanywa kwa namna ya ajabu,
matendo yako ni ya ajabu;
wewe wanijua kabisakabisa.
15Umbo langu halikufichika kwako
nilipotungwa kwa siri na ustadi ndani ya dunia.
16Wewe uliniona hata kabla sijazaliwa,
uliandika kila kitu kitabuni mwako;
siku zangu zote ulizipanga,
hata kabla ya kuweko ile ya kwanza.
17Ee Mungu, mawazo yako ni makuu mno;
hayawezi kabisa kuhesabika.
18Ningeyahesabu yangekuwa mengi kuliko mchanga.
Niamkapo, bado nipo pamoja nawe.
 
Elewa nilichokimaanisha kwanza
 
Weye acha longo longo wazungu waliokuketea Biblia unasema imewazidi uwezo???

Kwani kabla ya Biblia tuliishije??! Miaka ya 1400 huko kwa mfano?? Kabla hatujaletewa Biblia na wazungu ili watutawale kwamba hatukua na Mungu? mungu wetu ndo huyo huyo wa Wazungu??

Kuamini uwepo wa Mungu au kutokuwepo toka kwanza kwenye vifungo vya Biblia na Quran(unazoita reference) halafu ndo ujaribu kufikiria

Usiniulize mimi kama naamini Mungu yupo au Lah

Ila ukiniuliza kuhusu dini zilizokuja na mijeledi na jambia ntakujibu SIZIAMINI
 
Wenzako tumejadili sana haya makitu humu zaidi ya miaka mitano sasa.

Huu mfano wako wa saa hauna tofauti na huyo Mungu. Ukisema hajaumbwa utakuwa upo sawa na aliyeokota saa akasema hii saa imetokea tu from nowhere pasipo na muundaji wake.

Sawa, tukubaliane yupo mpangaja. Bila shaka mpangaji amepangiliwa vyema kuliko alivyovipanga.

Tuchukulie mfano wa haraka haraka. Kama muumbaji aliweza kufikiri na kuumba vitu vyenye akili na visivyo na akili, vyenye uhai na visivyo na uhai, vilivyoko kwenye mahesabu makali na vingine vilivyokaa shagala bagala kwanini naye asiwe na chanzo chenye maarifa kuliko yeye?

Kama umeutazama uumbaji ulivyo wa utata ukafikia kukubali lazima kuwe na aliyeumba, moja kwa moja muumbaji nae atahitaji awe ameumbwa kwa sababu yeye ni wa utata kuliko huu uumbaji wenyewe! Yeye ni wa maajabu zaidi kuliko uumbaji ulivyo wa maajabu.
Kama ni computer, basi yeye atakuwa ni super computer Kuliko computer sisi.

Je, utakubali kwamba muumbaji nae ameumbwa? Kadhalika kama ameumbwa, vivyo hivyo aliyemuumba nae atatakiwa awe ameumbwa pia.

Kama sisi na ulimwengu tumepatikana kutokana na ufahamu wa Mungu aliye tuumba, basi huyo Mungu nae haiwezekani awe ametokea tu from nowhere asiwe ametokana na fahamu zilizo juu ya uwezo wake pia.

Huu mlolongo hauna mwisho kama utataka kulazimisha kwamba tumeumbwa!

Umejitazama wewe ulivyo wa maajabu pamoja na mazingira akili yako ikagoma kabisa kwamba lazima kuwe na aliyekuumba wewe pamoja na hayo mazingira. Kwanini basi useme aliyeviumba hivi vyote hana mwanzo wala mwisho?

Je, mtu mwenye akili nyingi kama yeye aweza kutokea tu pasipo na chanzo kilichomleta yeye pamoja na maarifa yaliyomjaa kiasi hicho hadi kufikia kuumba mambo ya kutisha kama tuyaonayo?

Tafakari utagundua bado hatujui kitu bado.

Vitabu vilivyoletwa na waliotugeuza watumwa na wakatufunga minyororo visiwe sababu ya kufunga fahamu zetu.
Hapa hawawezi kujibu kwa hoja, watakuja na blabla...
 
Hapa brainwashed wa dini hawatakuelewa sababu wamefunga akili zao
 
Weye acha longo longo wazungu waliokuketea Biblia unasema imewazidi uwezo???
Ndio
Kwani kabla ya Biblia tuliishije??! Miaka ya 1400 huko kwa mfano?? Kabla hatujaletewa Biblia na wazungu ili watutawale kwamba hatukua na Mungu? mungu wetu ndo huyo huyo wa Wazungu??
Wazungu hawakultulazimisha kufuata Mungu waliokuwa wanamjua. walitushawishi kwa hoja zao ,wapo walioamini wapo ambao hawakuamini pia
Kuamini uwepo wa Mungu au kutokuwepo toka kwanza kwenye vifungo vya Biblia na Quran(unazoita reference) halafu ndo ujaribu kufikiria
Naamini Miungu wapo wengi. Mimi najaribu kujifunza huyu anayeelezewa kwenye biblia.sijafika mwisho, ila at least nipo hapo. Wa koran niliishashindwana naye ,nahisi huyu Allah ni ameumbwa kupinga Mungu wa kwenye biblia
Usiniulize mimi kama naamini Mungu yupo au Lah
hiyo ni siri yako mkuu
Ila ukiniuliza kuhusu dini zilizokuja na mijeledi na jambia ntakujibu SIZIAMINI

kuamini au kutokuamini ni hiari yako. Hakuna anayekulazimisha. Unatakiwa tu kujulishwa​

Marko 16:16​

Yeyote atakayeamini na kubatizwa ataokolewa, lakini yeyote asiyeamini atahukumiwa.
 
Back
Top Bottom