Kuna aina ya utapeli zain...

Kuna aina ya utapeli zain...

Makalangilo

Senior Member
Joined
Mar 9, 2009
Posts
133
Reaction score
19
Jamaa wa zain na shindano lao la kujibu maswali na kupata points lianelekea la kitapeli.Droo za kila sikuza kupata 500,000 hazipo!

Kama kuna jamaa walioshuhudia hizo droo naomba wanieleze zinatangaziwa kwenye chanel gani?
Ati particiapte in tonights draw...hakuna lolote wizi mtupu!
 
Jamaa wa zain na shindano lao la kujibu maswali na kupata points lianelekea la kitapeli.Droo za kila sikuza kupata 500,000 hazipo!

Kama kuna jamaa walioshuhudia hizo droo naomba wanieleze zinatangaziwa kwenye chanel gani?
Ati particiapte in tonights draw...hakuna lolote wizi mtupu!

Mi naona hizi simu zimebuni mbinu mpya ya kuibia wananchi... sijui kama wahusika wa mawasiliano wana taarifa kuhusu huu utapeli unaoendelea Tigo, Zain, Voda na hata Zantel... especially kipindi hiki cha kombe la dunia.... just imagine zimeback siku 5 bado wanakwambia ushinde ticket... Hii ndio Tanzania zaidi ya uijuavyo!!
 
Na kama utakuwa makini sana kila msg moja unayotuma inakatwa Tsh 300/=.

Kwangu mimi sishangai sana, maana hii inatokana na sisi watanzania kutaka mambo makubwa bila ya kujishughulisha, ndio maana inakuwa rahisi sana kwetu kuibiwa tena kwa urahisi.

Ukilifikiria sana hilo suala la zain, lazima utahisi kuna kitu kisicho na uhalali kinaendelea, haiingii akilini muda ambao msg inaingia na kile kinachozungumziwa katika msg hiyo kinakuwa contrary to each other. Nafikiri hili ni suala la kwanza kabisa la mtu kujiuliza mara mbili kabla ya kutenda.

Otherwise ngoja tusikilize wajumbe wenye ufahamu na jambo hili watoe mchango wao
 
Jamani tukumbuke Zain africa imeshauzwa kwa bharti Ya India nafikiri katika kuelekea makabidhiano kuna kamchezo kanafanywa na wafanyakazi wa zain
 
Makampuni ya simu yanawaibia wananchi kwa laghai na kujipatia mapesa mengi pengine kuliko hata hela wanazolipwa kwa huduma za ki simu.Sasa waachiwe tu waendelee kuwatapeli wananchi au hatua gani zichukuliwe ili kuwadhibiti?

Mbona kombe la dunia linatumika kwa kujitajirisha kwa ulaghai mkubwa wa Zain na hakuna anayekohoa japo kidogo?
 
Kibaya zaidi ni kuwa vituo vyetu vya Televisheni na radio vinakuwa washiriki katika hili. yapo matangazo meeengi yanayokutaka upige namba 15*** ili kushiriki shindano fulani lakini ni machache sana sana, kama yapo, ambayo yatakuambia hela utakayokatwa kwa kila meseji unayotuma. Kwa kifupi, yanacheza na ufahamu duni wa watanzania walio wengi ambao huishia kugeuzwa Wajinga waliwawo!!
 
Back
Top Bottom