Kumwita Mke wako MAMA Imekaaje Hii?

Kumwita Mke wako MAMA Imekaaje Hii?

The Businessman

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2014
Posts
7,397
Reaction score
9,264
Za sahizi wakuu!
Niliwahi kumsikiliza Dk Ndodi aliwaponda sana watu wanaowaita wake zao MAMA, alisema ni kuwakosea adabu wazazi waliotuzaa.
naomba tushare hapa najua kuna watu wa kila rika.
 
Mmmmhh...mi huwa nasikia baba anamuita hivyo mama
 
Haijakaa vizuri kabisa hiyo hivi mke wako unamuitaje mama wajameni.tatizo watu wengine huwa wanaona soo ama soni kusema "mke wangu" mbele za watu wengine sijui kwa nini... mke ni mke tu hawezi badilika.. ni nafuu basi kama unamuita mama umalizie kabisa "mama fulani" inaleta maana kuliko kumuita tu mama
 
Imani yangu hairuhusu kabisa kumwita mwenza wako, mama, dada, kaka,baba. Ukishatamka hilo ndio basi yaani unyumba hakuna, sema watu wanadharau sana hayo makatazo na wengine wanakuwa hawajui.
 
Mie napendwa kuitwa hivyo yani tena niambiwe"mama yangu nikuombe kitu"hata kama kipo nje ya uwezo wangu nitajitahidi nimfanikishie
 
Niheshima tu wala halina shida sababu mwanamke yeyote ni mama, ndomana hata wababa wengine huita watoto wao wa kike hivyo pia.
 
ni hivi, hata dini yangu inakataza hili swala kwa sababu huwezi kumfananisha mama yako na chochote kile. unapoamua kumuita mkeo mama au mumeo baba ndoa haipo tena kwa kua tu huwez lala na mama yako au baba yako. halafu kuwapachika majina mazito hivi mnapata wapi ujasiri??? siwez muita mume baba wala sitaki kuitwa mama kwa kua sijamzaa na sifikii upendo anaopewa na mama yake had afikie hatua ya kuniita hivo.
 
Za sahizi wakuu!
Niliwahi kumsikiliza Dk Ndodi aliwaponda sana watu wanaowaita wake zao MAMA, alisema ni kuwakosea adabu wazazi waliotuzaa.
naomba tushare hapa najua kuna watu wa kila rika.

ni kutojielewa tu ndio maana ndoa zinakufa
 
Niheshima tu wala halina shida sababu mwanamke yeyote ni mama, ndomana hata wababa wengine huita watoto wao wa kike hivyo pia.

Anamwita mama kwa sababu hawezi kulala/ kufanya naye tendo la ndoa ki maadili kwa vile yule ni mwanae ukikuta mzazi Ke au Me analala na mwanae huyo ana mapungufu ya akili.
 
mke wangu ni mpenzi wangu. For over 15 years of our ndoa sijawhai kumwita mama wala mke wangu, huwa ninamwita jina lake.....naye anafurahi kwani anajiona bado kabinti before my eyes.
 
ni hivi, hata dini yangu inakataza hili swala kwa sababu huwezi kumfananisha mama yako na chochote kile. unapoamua kumuita mkeo mama au mumeo baba ndoa haipo tena kwa kua tu huwez lala na mama yako au baba yako. halafu kuwapachika majina mazito hivi mnapata wapi ujasiri??? siwez muita mume baba wala sitaki kuitwa mama kwa kua sijamzaa na sifikii upendo anaopewa na mama yake had afikie hatua ya kuniita hivo.
Mamaa ...nawewe si ubadili jina unatulazimisha kuwakosea wazazi!
 
nazani ni urahisishaji wa mambo na haina maana una heshima ya mama yangu, ila tisa kumi nilichoka kuona wenzetu wa West Africa baadhi ya wanawake wanaita waume zao "Sir" na mume anaona sawa kabisa.
 
Niheshima tu wala halina shida sababu mwanamke yeyote ni mama, ndomana hata wababa wengine huita watoto wao wa kike hivyo pia.

Nadhan hii ndio point kubwa kumpa heshima tu mwenza wako!
 
Back
Top Bottom