Kumuamini Mungu lazima uwe na dini za wageni?

Nazungumzia na mtu anayesema hakuna Mungu hivyo ni wazi anaelewa aina ya huyo Mungu.
Sasa huyo anayesema hakuna mungu unaanzaje kumuambia kua umuoneshe mungu ilihali umekiri kua anasema hakuna mungu

Ataonaje kitu ambacho hakipo?

Wewe unayesema kipo ni wazi unakielewa kinafananaje mpaka ukajua kipo.

Tuelezee sifa za huyo mungu wako ili tujiandae kupata majibu ya namna hiyo hiyo iwapo ukituonesha
 
Navyozungumzia ulimwengu usioonekana ni katika jitihada za 'kukuelewesha' kuwa ulimwengu unaoonekana kwa macho (physical world) ni sehemu ndogo tu ya uumbaji wa Mwenyezi MUNGU.

Mungu ninayeuamini ameelezewa vizuri katika 'Biblia' kwa ufupi sana,halinganishwi na kitu chochote anauliza katika ISAYA ...Mtanifananisha na nani,nikapate kuwa sawa naye? Inueni macho yenu juu mkatazame,ni nani aliyeziumba hizi? Huyo ndiye namuamini kwa kifupi sana.
Una uhakika gani kwamba ulimwengu umeumbwa na Mungu? Unahakikishaje hii habari si hadithi tu?

Na imekuwaje Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote aumbe ulimwengu ambao mabaya yanaweza kutokea wakati alikuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezi kutokea?

Na imekuwaje Mungu aweke habari zake kwenye Biblia ambayo ina utata mwingi wa lugha na tafsiri na watu kujua kusoma badala ya kuweka habari zake kwenye DNA kila mtu azijue bila kujali lugha, tafsiri na uwezo wa kusoma?
 
Sasa huyo anayesema hakuna mungu unaanzaje kumuambia kua umuoneshe mungu ilihali umekiri kua anasema hakuna mungu

Ataonaje kitu ambacho hakipo?

Wewe unayesema kipo ni wazi unakielewa kinafananaje mpaka ukajua kipo.

Tuelezee sifa za huyo mungu wako ili tujiandae kupata majibu ya namna hiyo hiyo iwapo ukituonesha
Huwezi kupinga tu au kusema kitu fulani hakipo huku ukiwa hujui sifa za hicho unasema hakipo.
 
Huwezi kupinga tu au kusema kitu fulani hakipo huku ukiwa hujui sifa za hicho unasema hakipo.
Kwani kwako iwe rahisi kusema kitu fulani kipo wakati hujui sifa za hicho kitu unachidai kipo?

Mtu anayesema kitu fulani hakipo ana maanisha kinaonekana hakipo?
 
Kwani kwako iwe rahisi kusema kitu fulani kipo wakati hujui sifa za hicho kitu unachidai kipo?

Mtu anayesema kitu fulani hakipo ana maanisha kinaonekana hakipo?
Kuna niliposema sijui sifa za hicho kitu nachosema kipo? Ukisema kitu fulani kipo au hakipo lazima ujue sifa za hicho kitu huwezi kulala na kuamka tu na kuamua kujisemea kitu fulani hakipo au kipo.
 
Kuna niliposema sijui sifa za hicho kitu nachosema kipo? Ukisema kitu fulani kipo au hakipo lazima ujue sifa za hicho kitu huwezi kulala na kuamka tu na kuamua kujisemea kitu fulani hakipo au kipo.
Kwa hiyo sifa za mungu wako unazijua?

Basi zitaje hapa uthibitishe maneno yako
 
Kwa hiyo sifa za mungu wako unazijua?

Basi zitaje hapa uthibitishe maneno yako
Nitaje nimtajie nani kwa sababu wewe unayesema hayupo pia unazijua sifa zake pia na ndipo ukafikia kusema hayupo bila hivyo usingesema kitu hakipo hali ya kuwa hukujui.
 
Nitaje nimtajie nani kwa sababu wewe unayesema hayupo pia unazijua sifa zake pia na ndipo ukafikia kusema hayupo bila hivyo usingesema kitu hakipo hali ya kuwa hukujui.
Mimi nayesema hayupo namaanisha kisichopo hata kuonekana hakionekaniki

Wewe unayetaka kunionesha ni wazi kwamba unajua kiundani kua mungu huyo yupo na ukajua kua anaweza hata kuoneshwa na watu wakamuona

Sasa tuambie vigezo gani ambavyo huyo mungu ako navyo ili pindi unapotuonesha tuweze ku confirm kua tumeoneshwa mungu ambaye umemkusudia
 
Nazishangaa Sana fikra zako! Asingekuja Africa? Kwanini ufikiri kuwa asingekuja!? Basi ndo alikuja na ktk kuja kwako ndipo tukapata habari za uislam, na ktk dunia hii ya maendeleo ya kiteknolojia hata Kama asingekuja ningesikia habari ktk vyombo mbalimbali vya mawasiliano . Si wote walioingia ktk uislam ilikua Ni matokeo ya kutembelewa au kutawaliwa na waarabu, binaadam anatabia ya kujifunza na kutafuta habari . Pia nikutoe wasiwasi, japo nimezaliwa ktk uislam ndio! Lakini baada ya kukua nilipata nafasi ya kuwa huru kuchagua muelekeo wa maisha yangu kidini, kisiasa na kiuchumi, ktk kuisoma dini hii nikapata uhakika kuwa sijapotea njia kuzaliwa ktk dini hii, Ni dini ya kweli na Haki, kwani wangapi hawakuzaliwa ktk dini ya uislam na baada ya kujua ukweli wakaamua kuingia ktk uislamu? Ni wengi tu, I am very confident kusema kuwa I am in a right track and sijawa brain washed ata kidogo, just read Islam and come back again to argue with me. Najua ukiusoma utaona kitu ambacho Mimi nimekiona.
Aisee ... imani
 
Mimi nayesema hayupo namaanisha kisichopo hata kuonekana hakionekaniki

Wewe unayetaka kunionesha ni wazi kwamba unajua kiundani kua mungu huyo yupo na ukajua kua anaweza hata kuoneshwa na watu wakamuona

Sasa tuambie vigezo gani ambavyo huyo mungu ako navyo ili pindi unapotuonesha tuweze ku confirm kua tumeoneshwa mungu ambaye umemkusudia
Hapo kusema kwako kuwa huyo mungu hayupo ulikuwa umetumia vigezo gani? mfano nikienda kukuonesha mlima wa Kilimanjaro, je ndio hicho(mungu) ambacho wewe unasema hakipo?
 
Hapo kusema kwako kuwa huyo mungu hayupo ulikuwa umetumia vigezo gani? mfano nikienda kukuonesha mlima wa Kilimanjaro, je ndio hicho(mungu) ambacho wewe unasema hakipo?
Kisichopo hakionekani hakuna namna yeyote unayoweza uks detect kisichopo kua hakipo

Mfano wako bado upo kwenye assumption uidhinishe iwe ndio hoja unayoitetea

Kwa hiyo twende na mlima kilimanjaro kua ndio mungu unayesema yupo na muumbaji wa vyote?
 
Kwa maana hiyo ni kwamba pia huwezi kujua kuwa kitu hicho hakipo.
 
Sasa mbona wewe unasema kabisa kuwa kitu fulani hakipo? kwa maana unajua kabisa kuwa hicho kitu hakipo kuna sababu na ushahidi ndio maana ukasema hivyo.
Ushahidi nimekuwekea ila haupo unaweza ukathibitisha vipi kua haupo?
 
Huwezi kupinga tu au kusema kitu fulani hakipo huku ukiwa hujui sifa za hicho unasema hakipo.
Sasa mbona mimi nikikuuliza kama Mungu wako kaumba ulimwengu au hajaumba ulimwengu (sifa yake) ili niweze kumchambua vizuri huyo Mungu unataka kumtenganisha huyo Mungu na sifa zake, unataka nijibu kuhusu huyo Mungu bila kuhusisha sifa yake ya uumbaji?
 
Uumbaji ni sifa ya Mungu sijamtenganisha nayo, ambapo hatuelewani na ndipo lilipo tatizo lako ni uhusishwaji wa Mungu na uumbwaji wa huu ulimwengu.

Uumbaji ni sifa yake na katika alivyoumba huu ulimwengu ni kimoja wapo na si kwamba anaitwa muumbaji kwa sababu ya kuumba huu ulimwengu tu.
 
Back
Top Bottom