Kumswaga mwizi kama kuku nikumuongezea mbinu za wizi

Akabi kemanya

JF-Expert Member
Oct 26, 2021
226
346
Kama bandiko linavyojieleza kumswaga mwizi kama kuku nikumuongezea umakini wa kuiba

Niwazi kuwa wote tumesikia masikitiko ya mama dhidi ya madudu yaliyo ibuliwa kwenye lipoti ya mkaguzi w hesabu za serikali

Mama analalamika mama anaudhunishwa na huu ujambazi unaofanywa kwenye hii miladi ya serikali

Ila kimsingi kilio cha mama nikama kilio cha samaki ndani ya bahari, huwezi kutatua tatizo kwa njia ileile iliyo feli jana

Mwizi wa kuku au mbuzi ni mwizi nijizi jambazi kama majambazi wengine, hivyo kimsingi hawa majambazi wa pesa za umma wanatakiwa washughulikiwe kama majambazi wengine wanavyo shughulikiwa huku mtaani

Nahapo walau ndipo tatizo hili la ujambazi wa mali za umma litapunguwa, lakini kwa kuwa serikali yenyewe imebariki jambo lenyewe tena ikalibatiza jina zuri kabisa eti ufisadi badala ya ujambazi

Leo mama anawaambia wezi eti Niheri watupishe maana hawana sifa tena, niseme tu kauli ya mama inawa imarisha kimbinu majambazi hawa na kuwaongezea kasi ya kuiba na kupanua mtandao wao
 
Back
Top Bottom