Mjegejo Wa Begeju
Member
- Jun 17, 2023
- 93
- 220
Africa ndiyo bara linaloongoza kwa kuwa na maajabu mengi yasiyo na tija. Ni bara ambalo linaamua kumchagua binadamu mmoja kumfanya awe mungu, jambazi la kuheshimika, tapeli, muuaji na fisadi.
Huyu akichaguliwa na kupewa vyeo hivyo anaachagua naye watu wa namna yake ambao watatenda kama yeye. Hawa wanakuwa wapambe au chawa wake. Hawamsaidii kumrudisha njia kuu. Wao wanamsaidia kuendeleza wizi, ujambazi, ufisadi, uuaji, utapeli, uchawi n.k
Then hawa maskini wanaanza kumlipa huyu kubwa la majambazi kwa kupitia kodi zao. Huku wakimsifu na kumuabudu. Na kwa kupitia kodi hizo hizo anapata pesa za kuajiri wanajeshi kutoka kwa hawa hawa maskini walalahoi kwa ajili ya kumlinda.
Nao wanaona fahari kubwa kumlinda mtu anayekula pesa zao na kuuza rasilimali zao kwa faida yake na watu wake. Hawa wanajiona wao ni bora zaidi kuliko baba na mama zao. Ambao wanaishi katika shida kubwa sana.
Wanaendelea kumlinda mtu ambaye atauza rasilimali zao na kujifaidisha yeye huku wao na watoto wao wakiendelea kuishi maisha magumu. Lakini wanafurahi kwa kuwa wana uhakika wa kupata mabaki kidogo ya chakula toka mezani na kulamba lamba mikono ya walioshiba.
Ni africa hii ambayo mwizi wa kuku anauawa halafu mwizi wa mabilion anasifiwa na kupongezwa sana. Huyu ambaye kwa kuuza rasilimali na kufanya ufisadi anasababisha raia wengi wafe kwa kukosa huduma za afya, chakula bora, msongo wa mawazo, maisha magumu, kupoteza matumaini n.k
Africa ni bara ambalo Rais au Kiongozi wake anaweza toka nchini kwake kwenda kusuluhisha ugomvi wa mbali huku kwake hali ikiwa ni ya kutisha kwa vifo na majanga makubwa. Na huko aendako anabeba wapambe wengi kwa ajili ya kuwapatia per diem na kufanya shopping.
Ni Afrika ambapo wawakilishi wa Wananchi maskini wanakuwa wapambe wa serikali. Na wananchi wanaowakilishwa hawaoni tatizo. Kodi zao zinapotumika kuneemesha wachache wateule wananchi wanaona sawa tu.
Ni Afrika hii ambayo watu hukosoa au kupongeza kwa kuzingatia Dini, Kabila au Kanda. Pia huzingatia ulaji wa sehemu husika. Miaka zaidi ya 50 baada ya Utumwa na Ukoloni Africa inaenda tena kuwaita waliowafanya watumwa na kuwatawala kuwa mabwana zao.
Miaka mingi baada ya uhuru Africa inarudi na kusema hatuwezi jitawala, hatuwezi jiendesha. Tunataka watu weupe wafanye hivyo kwa niaba yetu. Halafu ikiwapendeza watupatie chochote kitu.
Afrika ina maajabu ya kipumbavu yasiyo na tija kwa watu wake.