wataalamu hawakushauri tununue mitambo ya wizi, walio toa uamuzi wa kununua mitambo ya wizi ni idrisa akisaidiwa na baadhi ya wapambe ambao wengine hatujajua nini ili kuwa interest yao. walicho sema wataalamu ni kununua mitambo in general, specific ilikuja kwa watawala au viongozi, ku-source hiyo mitambo ya wezi, ambao mpaka leo hii aliyekuwa analipwa hizo hela hatuambiwe, kwanini? kama hakuna kitu cha ajabu?
spinning....
...Bravo Mh Zitto na endelea na misimamo yako thabithi yenye manufaa kwa taifa letu.
Masatu,
CCM ndivyo mlivyo.
jibu specific, na sio sweeping statement ambayo ina beba mazuri na uchafu, je aliye lipwa hela richmond aka dowans ni nani? na hii hela ya mitambo tutampa nani?spinning....
kwi!kwi!kwi!Is Zitto CCM? je wewe chama gani homeboy?
kwi!kwi!kwi!
Mimi mtoto yatima.
Jasusi huyu ni Masatu kweli ama kuna nguvu nyuma ya Masatu ? Huge U turn indeed
Masatu,
Mkuu wangu labda wewe omba radhi kwa sababu unachobishana hapa JF ni ubishi tu usiozingatia umuhimu wa hoja nzima ya mahitaji yetu.
Zitto na viongozi wengine wote wanafikiria kama wewe, yaani kutatua tatizo ndio mpango yakinifu wa maendeleo yetu..kwa njia hiyo hatuwezi kuwa wabunifu hata kidogo..Hatuwezi kujenga mipango bora ya ujenzi wa taifa letu changa na maskini ikiwa tunafikiria kutatua marttatizo kama vile maskini mwenye njaa anayetafuta mlo wa siku..
Mawazo ya Zitto yaweza kuwa mazuri kwa sasahivi kwa sababu tu tuna njaa, lakini ktatizo mloshindwa kuliona ni kuuza mwili wetu kwa sababu ya mlo wa siku. Kesho tutaendelea kuuza mwili na mwisho wake kuzoea umalaya wa kuuza mwili, jambo ambalo Zitto, Lipumba na viongozi wengine wameshindwa kuliona.
Mkuu wangu kama serikali imeshindwa kutekeleza hata mradi mmoja wa ufaji umeme kama tulivyoahidiwa, Zitto alitakiwa kusimama upande wa pili kama kiongozi wa Upinzani ambaye analitakia mema Taifa letu badala yake amejiunga na mpango wa kutatua matatizo tuliyokuwa nayo kwa njia ya Umalaya.
Well wewe unaweza kuomba samahani lakini navuyojua mimi njaa hiyo ya siku mbili tatu, hatujafa bado.. kweli tuna shida lakini hatuwezimkuuza mwili wetu kwa sababu Zitto kasema.
As a fact mimi naunga sana mpango wake wa kuachana na siasa kutogombea Ubunge arudi kazini akafanye kazi alosemea..I thought he stand with us kama wapinzani wa utawala huu unapofikia maswala mazito kama haya lakini anapounga mkono upotoshaji huu kwa sababu tu matokeo yake yamepangwa kuwa hivyo... nasikitika kusema kachuuzika! He is a Lost boy kisiasa!
Dark City,
Mkuu wangu umesema kweli.. wakati wa Mkapa tulikaa kizani karibu mwaka mzima..Sikumsikia Zitto wala machizi wengine wakizungumza lolote kana kwamba wananchi tumeshasahu hali ile...Yote hii Zitto anacheza ili Kigoma wapate generator ambayo kaahidiwa kama Tanesco watachukua mtambo huu.... hakuna zaidi, ni mchezo wa CCM...
Janja yao kwisha gundua!
Mheshimiwa watani zangu wazaramo wana msemo ufuatao "akutukanae kilabu cha pombe usisubiri kesho yake na wewe mrudishie matusi yake huko huko kilabu cha pombe" Kwa kuwa kashfa nilizitoa hapa JF nalazimika kuomba msamaha hapa hapa JF na ni matumaini yangu utanisamehe.
...
Mheshimiwa naomba kuwasilisha
kma ni kweli ulipost thred y kumtukan mhe.zito nkupongeza kwa uungwana wako wako wa kumuomba radhi kupitia jukwaa hilihili ulilomtumia,
nchi yetu hivi sasa ipo taabuni shauri ya wajinga wachache wasioona mbali ni kweli yawezekana mitambo ile ni ya kifisadi lakini by that time we had no option lakini watu wakaona labda kama vile kuna watu fulani watamake kwelikweli,huo haukuwa uamuzi mzuri,
inafsi ni mfuatiliaji mzyri wa television series ya kimarekani ya 24,kuna seasons zingine mfano season 3 au season 7 jack bauer analazimika kufanya mahusiano na magaidi just ili apate anachokitaka na kwa kwetu tulichokitaka ni nchi kuwa kwenye umeme ili shughuli za uzalishaji mali zisisimamae,leo hii nani anaweza kutueleza ni mamiliono mngapi yanapotea kutokana na viwanda au ofisi mbalimbali kuwa hazifanyi kazi?au ghrarama ambazo zinakuwa incurred kwa ajili ya majenereta?
BANIANI MBAYA LAKINI KIATU CHAKE DAWA
Mkuu wangu, yaani sina la kuongeza... Nafikiri, Tanzania we need Jesus! ni wakati wa ukombozi wa kiroho!Huu wote ni ukosefu wa principles tu, hamna geni!
Tuwafungulie kutoka jela walawiti, wauaji, majambazi, n.k. kwa vile nchi yetu haina pesa za kutosha?!!
Watu wengine mnaonekana mko tayari kulala (kimapenzi) na wazazi wenu eti kwa vile tu jambazi limewashikia mtutu kichwani!! Let's suffer na vibatari vyetu, lakini Dowans na nduguye Richmond nasema NO!!!
Mh Zitto, nianze kwa kukiri mimi nilikuwa miongoni mwa wana JF wengi tuliokuzonga kwa kejeri, shutma, kashfa na dhihaka kadha wa kadha kuhusiana na msimamo wako kwenye suala zima la ununuzi wa mitambo ya Dowans.
Mheshimiwa, ulikuwa sahihi kwa kusimamia kile unachoamini ni sahihi. Hii ndio sifa adimu ya kiongozi. Naamini hata wewe mwenyewe ulijua toka mwanzo kuwa uamuzi wako wa kutetea ununuzi wa mitambo ile hautakuwa popular na pengine ni kitanzi cha kisiasa. Lakini kwa ujasiri usiomithilika uliendelea kujenga hoja na wengi tulitia pamba masikioni mwetu na kukuita majina mabaya lukuki. Binafsi nilikwenda mbali zaidi na kukuita fisadi. Hili ndilo limenisukuma kuandika waraka huu mfupi ili kukuomba msamaha kwa maandishi yote machafu juu yako. Naamini tupo wengi wa aina hii lakini wenzangu wanakosa uthubutu wa kukiri na wanajichimbia kwenye keyboard zao.
Masatu kuomba radhi sio tu kumenichanganya bali kumenionyesha ni jinsi gani baadhi ya watu JF wanavyokuwa wavivu wa kufikiri kwa mustakabali wa nchi hii,nasisitiza tena kitendo cha Mbunge Zitto kutaka kutushawishi watz kununua mitambo chakavu ya DOWANS sio tu ni cha kulaaniwa bali ni kitendo ambacho kimemvunjia sana heshima Mbunge Zitto!
Taifa leo lipo latika kiza, kwa sababu ya watu wachache waliokataa ushauri wa wataalam. Wale "wapiganaji" wanaona soni nyuso zimewashuka wanatapatapa kutafuta justification ya uamuzi wao mbovu ambao umeligharimu na utaendelea kuligharimu taifa kwa hasara kubwa.
Mheshimiwa watani zangu wazaramo wana msemo ufuatao "akutukanae kilabu cha pombe usisubiri kesho yake na wewe mrudishie matusi yake huko huko kilabu cha pombe" Kwa kuwa kashfa nilizitoa hapa JF nalazimika kuomba msamaha hapa hapa JF na ni matumaini yangu utanisamehe.
Nimalizie kwa kukiri na kusema kuwa Mh, wewe ni hazina ya taifa hili. Kama kiongozi vision yako ni kubwa kuliko umri wako. Pamoja na kuwa wanasiasa wanaepuka sana kujiingiza katika masuala tata kwa kuchelea kushusha credibility zao wewe umeweka utanzania wako mbele bila kuogopa kupoteza umaarufu wako wa kisiasa and spot on, you got it right.
Bravo Mh Zitto na endelea na misimamo yako thabithi yenye manufaa kwa taifa letu.
Mheshimiwa naomba kuwasilisha