Ukisoma vizuri maoni ya Mzee ES, utajua Tanzania ina watu wa fikra za namna gani, na utajua kwa nini hatuendelei. Viongozi wengi tulionao,, na wanasiasa wanaotamba sasa wana fikra za aina ya ES.
Binafsi simjui, lakini mawazo yake yanatosha kunieleza mtazamo wake. Bila shaka, kwa mawazo haya amewaharibu wengi. Sijui kama ni mzee au kijana. Kama ni mzee haoni mbali. Kama ni kijana, bado ana muda wa kujifunza. Akubali kufungua pazia machoni pake, akubali kuchungulia nje ya dirisha. Ataona mazuri mengi ambayo hakuyajua kabla!
Watanzania wanajua kilichotokea katika uchaguzi. Walijua kabla ya uchaguzi. Wanajua mfumo uliotumika. Hawakuwa na madaraka nao. Ni wafungwa. Ni watumwa wa siasa zao wenyewe.
Wanajua kilichowasambaza vigogo wote wa CCM nchi nzima katika wiki ya mwisho wa uchaguzi. Wanajua makada wa CCM waliofunzwa 'mbinu za kushinda uchaguzi' katika cha usalama wa taifa, mkakati uliosimamiwa na Mkapa, Malecela, Mangula na Bosi wa Usalama wa Taifa, mapema kabisa hata kabla ya mgombea kupatikana.
Bwana ES, kama ni mwana CCM, wenzake wanamficha mambo mengi. Au anayajua lakini anakufa nayo kwa sababu ana maslahi binafsi.
Anajua yaliyotokea Karagwe? Uhuni ambao haupaswi kuhusishwa na watu wanaojitambulisha kuwa ni waungwana wa kisiwa cha amani! Anajua Mzee Kahama alikuwa anasindikizwa na FFU kuwatembelea kina nani, na aiwa amebeba nini usiku wa kuamkia Desemba 14, 2005? Anajua mkakati wa kununua shahada na vituo feki vya kupigia kura?
Anajua kwamba vyama vingi, CHADEMAM kikiwamo, havikuwa na wawakilishi kila kituo, wakati CCm kilikuwa nao na kiba pesa ya ziada ya kuwapa hata wasio wake? Anajua kuwa katika kujumlisha matokeo ya vituo ndani ya kata, hakukuwa na wawakilishi wa chama?
Hakuhusika katika kufunzwa namna ya kuwapigia kura wasiojua kuandika au kusoma?
Hakujua matokeo ya ghiliba za Mkapa na dola nzima, kuwatisha ananchi kwamba wakichagua upinzani yatawapata makubwa? Anadhani vilipotea hivi hivi? Hajui nguvu ya maRC na maDC walioamrishwa na Mkapa, kwamba hatasubiri vikao kuwashughulikia iwapo watapitisha wagombea wapinzani?
Hakujua nguzu ya kipesa ya CCM na jinsi ilivyotumika kueneza propaganda mbovu za kichawi dhidi ya upinzani? Hakujua kwamba tangu Tanzania iwe huru hakuna mgombea urais aliyetangazwa kama Kikwete katika nchi nzima?
Hajui ghiliba zilizowapata watu kama Lwakatare hadi siku yenyewe ya kupiga kura?
Tukirejea kwa Mbowe, mze ES hakujua hadhi na uwezo wa CHADEMA kabla ya uongozi wa Mbowe? Hakujua udhaifu wa chama kimtandao na kimkakati - kwa sababu nyingi tu?
Anapuuza nguvu ya ubunifu na ufundi wa kampeni uliotumiwa na chama kidogo kama CHADEMA kukua na kuleta msisimko nchi nzima kiasi cha kutajwa kila kona na wana CCM - bila shaka kwa hofu? Anadhani hofi hiyo imekwisha?
Amefanya utafiti kujua maoni ya watanzania leo kuhusu CHADEMA? Amekwenda Ubungo, Kawe, Kibaha, Karagwe, Muleba, Hai, Vunjo, Bukoba Mjini, Muleba Kaskazini, Shinyanga Mjini, Songea Mjini, Mpanda Kati na kwingineko kujua kilichotokea?
Anajua kuwa ufafanuzi wa Mbowe kuhusu sera ya majimbo ndiyo unashika gumzo kichinichini sasa, baada ya watu kutafakari sasa? Na anajua moto utakaowaka?
Na kuhusu Kikwete. Mzee ES anajua kwamba huyu jamaa ni Machiavellian wa kutisha? Ampe muda.
Lakini zaidi, wengi tunasahau kwamba nchi yetu haina Usalama wa Taifa. Tuna usalama wa rais! Mambo mengi ya kipuuzi yanayofanywa na viongozi wetu dhidi ya wananchi wake yasingefanyika kama tungekuwa na usalama wa taifa. Tunahitaji kulitafakri hili.
Na tataizo jingine la mzee ES, anapenda - kama walivyo wengi ndani ya CCM, labda ikiwa ishara ya uchovu na kuishiwa - kujadili watu badala ya masuala. ndiyo maana anashindwa kuona suala katika hoja ya Sumaye.
Maskini ES, hajui kwamba Kikwete alijiandaa miaka 12 iliyopita, na amekuwa akinusa wanaotaka kuwania urais na kuwabomoa kupiia vyombo vya habari ambavyo pia amevitumia kwa muda wote huo bila watu kujua!
ES hakumbuki kashfa ya Sumaye kutumia milioni 500 katika ziara moja nje ya nchi (Marekani na Ulaya) miaka kama minne iliyopita? nani alimpangia ziara hiyo? nani alimpangia watu wa kuandamana nao? Nani aliwalipa posho? BIla shaka ES anajua wizara husika! Na nani alipeleka vielelezo kwenye gazeti la RAI? Anajua mchango wa gazeti hilo kwa JK?
Kama ES hajui mnyukano wa chini kwa chini ya JK na Sumaye kwa miaka kama mitano iliyopita, basi yu CCM nusu nusu!
Na sasa je, ES anajua kwamba JK amelinunua gazeti hilo kwa kuwekeza ndani ya Habari Corporation asilimia 70 kwa mgongo wa Rostam Aziz? Berlusconi mpya!!!
ES anajua jinsi CCM wanavyomalizana, si kisiasa tu bali hata kwa kutoana roho? mambo mengine ni very sensitive bwana, lakini vi vema kizazi hiki kijisafishe.
Kuhusu magazeti, ES ni wa kuogopwa. Pamoja na miaka 14 ya demokrasia - tunazungumzia diversity na plurality - mwenzetu anafikiria kufutia magazeti. Wanaojua, wanayatetea hata yale ya udaku. Yana mchango wake.
Na kama Watanzania wangejua umbumbu wao unaendelezwa na nini, ni haya magazeti ya udaku, yasiyoandika issue bali personalities, na wansiasa wanayapa mtaji ili yaendelee kuvuta hisia za wananchi, wao wavurunde wasiandikwe, ili wakifika wakati wa uchaguzi, wananchi wasiwe na ufahamu mkuvbwa wa masuala yanayoendelea, wasubiri kugawiwa fulana na kofia, na kutishwa kwamba wakichagua upinzani watakuwa kama Rwanda na Burundi!
Lakini magazeti makini yote yametekwa na JK sasa. Na sheria mbovu zinazotawala uandishi na uchapishaji nchini ndizo zinawamaliza kabisa waandishi, wanabaki kuogopa kushitakiwa...wanaufyata, wanaanza kujikomba ka watawala, nchi inaliwa!
Mdomo pekee uliobaki wa wananchi kusema mambo yao ni Tanzania Daima. Wanaliogopa Tanzania Daima ndi hao wanaomulikwa nalo. Huwezi kusoma uchambuzi wa gazeti hilo, hasa wa Jumapli, ukalibeza. labda kama upeo wako msomaji ni hivyo hivyo, hobela hobela!
Upeo mdogo wa Bwana ES nimeuona zaidi katika kujadili uhusiano wa Mbowe na viongozi wa CCM! Ana akili ka ya Mrema, ya kudhani mtu unayetofautiana naye kisera hupaswi kukaa naye, kufanya urafiki, kusaidiana naye katika masuala ya kifamilia hata kibiashara. Kizazi cha kina Mbowe kiko tofauti, kinajua mipaka hiyo. Wahafidhina wanazubaa, wanashangaa, na wanapotosha hata kwa mambo madogo.
kumbe ndiyo maana watu walishangaa kuona anamkumbatia Kikwete baada ya matokeo kutangazwa! Bado tuna nji ndefu.
Mwisho, akubali kwamba kilichoandikwa ni kweli. Kinamkera kwa sababu mpango wao umejulikana. Lakini kabla ya Mbowe CCM imewafanyia wengi uhuni huo. Kumbe hajui kwamba dhamira ya kwanza ya JK kummaliza Mbowe ilijadiliwa waziwazi Songea alikokuwa amealikwa kuwa mgeni rasmi siku ya Ukimwi duniani, Desemba 1, 2005? Sisi tunajua.
Hajui kwamba hata katika kikao cha juzi cha NEC - kwanza hata katika kamati ya maadili ya CCM - JK alianza kwa kukataa uwepo wa mtandano ndani ya CCM, akasema haya mambo yanasambazwa na wapinzani kina Mbowe ili CCM ionekane imegawanyika? Hajui? Sisi tunajua.
Hajui kwamba baadhi ya wajumbe wa NEC wamekerwa na maneno hayo, kwamba rais ajielekeze kwenye hoja ya mgawanyiko ka sababu upo, na kwamba Mbowe hahusiki? Sisi Tunajua.
ES hajui, kwa sababu nilizokwishataja hapo nyuma, kwamba JK anamwogopa Mbowe kisiasa? Hajui siasa zilizvyo? Hujuma kupitia vyombo vya habari, usalama wa "taifa", wakuu wa mikoa, na umafya wa kizamani dhidi ya upinzani kupitia tume ya uchaguzi vitaendelea kuwalinda wenye madaraka? Anadhani Watanzania hawataamka hata siku moja, bali wataendelea kuhatamiwa kama mayai?
Sisi hatudhani hivyo. Na hatuko wachache, wala dhaifu kiasi hicho. JK anajua. Ndiyo maana ananekana kujali, na hata kutumia baadhi ya mambo ya Mbowe (jambo linalokubalika kisiasa) kjijenga. Na huwezi kujijenga bila kubomoa washindani wako. Na katika Bara, hana mshindani zaidi ya Mbowe.
Tusisahau pia kwamba hata kama si lazima Mbowe awe rais, tunaweza kumtumia Mbowe kulijenga taifa. Kwanza aijenge CHADEMA kama taasisi halafu atumike kwa sababu yupo, na anataka. Hata kama tunataka kuwajenga wengine, kina JJ, Zitto, wewe na mimi na wengine, hatuwezi wala hatupaswi kufanya hivyo kwa kumbomoa Mbowe. Hiyo itakuwa ni mbinu ile ile, chafu ya CCM kupitia kwa watu wanyonge wa kuwaza, kutafakari na kuchambua.
Sisi hatutakubali kutumika
MAN