Kumpeleka mwanao shule za kata ni kwenda kumzika kielimu

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
62,314
109,352
Wadau nawatahadharishe kitendo cha kukosea na kumpeleka mwanao shule ya kata kitaigharimu elimu ya mwanao. Mwanangu toka ameenda shule wiki iliyopita amefundishwa somo moja tu tena kwa kiwango cha chini sana.

Siku nzima wako darasani wanapiga story, walimu wakipita ni kuangalia wasumbufu na kuishia kuwarusha kichura.

Ni kwanini hiyo elimu waalimu hawafundishi ipasavyo, hao viongozi watoto wao hawasomi humo hivyo wanabaki kuchukua sifa majukwaani kwamba kuna elimu bure wakati ki ukweli ni kaburi la elimu.
 
Hakuna cha elimu ya bure bali nia yao ilikuwa kuhamishia gharama za elimu kwa serikali.
Kwa vile serikali bado haijabeba gharama hizo kwa kiwango cha kuridhisha matokeo ni kama hayo yaliyokupata. Mkuu ukiweza mlipie mwanao ili apate elimu ya uhakika.
 
Mkuu kinachoendelea huko naona ni kifo cha elimu yetu dhahiri. Kibaya zaidi huo uozo ulioko huko serekakini ndio wanataka kuhamishia kwenye shule za binafsi. Sipati picha huko tuendako na tukija kuamua kuchukua hatua ndio tutakuwa tumeshachelewa. Ngoja nifanye utaratibu tu nimpeleke mtoto wangu kusoma Kenya.
 
sio kweli mkuu,kama mwanafunzi anjielewa...hapo shida ni kwa mwanafunzi maana walimu mbona shule zngne wanajitoa sna na wanafanya kazi,lada shule ambazo zina upungufu wa waalimu.ila tulosoma shule hizo mbona wengi tumefaulu mkuu?
 
Wewe mpeleke private,atausikilizia mkopo
We mwanao unampeleka shule za kata kwa sababu ya mkopo? Sasa akienda kusoma huko na akapata zero form 4 mkopo anaupataje?
Fikiria vizuri na mtoto sio lazima aunge moja kwa moja Chuo kikuu anaweza kumaliza form six ukampeleka vyuo vya kati akapata diploma ya fan fulan akaajiriwa baadae Chuo kikuu atajisomesha mwenyewe au kumuongezea nguvu kidogo wakati huo tayari kaajiriwa!!
 
Ni vizuri pia,

Sent from my phone,the name its none of your business
 
Huyu mleta mada anafikiria vipato vyetu vinalingana,wengine kupata mlo tu ni shida halafu anatuhamasisha tupeleke watoto wetu shule za private,sijui atatusaidia kulipa ada?,
Nyongeza:hivi matokeo ya kitado cha nne na cha sita shule za kata wanapata four na ziro wote?
Au hizo shule za private hua hawapati four au ziro?
 
Mkuu sikuhamisishi bali nazungumza ukweli wa shule hizo. Hizo shule zimegeuka vijiwe rasmi kwa majina ya shule.
 
Ahsante sana LOWASSA ulianzisha shule za kata nikapata nafasi, second selection nikasoma, sasa napata mshahara wangu SAFI kabisa!
Muhudumu, naomba kiroba kingine
 
sio kweli mkuu,kama mwanafunzi anjielewa...hapo shida ni kwa mwanafunzi maana walimu mbona shule zngne wanajitoa sna na wanafanya kazi,lada shule ambazo zina upungufu wa waalimu.ila tulosoma shule hizo mbona wengi tumefaulu mkuu?
Uelewa wa mtoto ndio jambo la msingi, japo ni kweli kuwa shule hizi zina changamoto nyingii..... hivyo mwanafunzi lazima atumie jitihada binafsi ili aweze kufaulu
 
We mwanao unampeleka shule za kata kwa sababu ya mkopo? Sasa akienda kusoma huko na akapata zero form 4 mkopo anaupataje?
Fikiria vizuri na mtoto sio lazima aunge moja kwa moja Chuo kikuu anaweza kumaliza form six ukampeleka vyuo vya kati akapata diploma ya fan fulan akaajiriwa baadae Chuo kikuu atajisomesha mwenyewe au kumuongezea nguvu kidogo wakati huo tayari kaajiriwa!!
Kaka umemaliza.!!,
 
Back
Top Bottom