Kumkataa Mchumba wa kwanza ni nuksi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumkataa Mchumba wa kwanza ni nuksi?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Gaga, Mar 24, 2011.

 1. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kuna kitu hii huwa naisikia sana kwa watu wazima,zamani kabla ya miaka ya tisini wasichana wengi walikuwa wanatafutiwa wachumba, au wazee wa jirani au ukoo fulani wanaleta posa moja kwa moja nyumbani kwa wazazi wa msichana husika,kwa wakati huo ukikuta kuna msichana yupo kwao mpaka miaka 40 hajaolewa ukiuliza utasikia huyu alimkata mchumba wake wa kwanza akapata laana kwa mungu

  Nikiangalia kuna ndugu zangu wawili wanawake watu wazima nao naambiwa na ma mdogo waliwakataa wachumba wao wa kwanza huko zamani na sasa ni watu wazima mmoja kajizalia watoto mwingine bado hajazaa.Naomba wanaJf wanijuze hii ni kweli? vipi kwenye jamii inayokuzunguka yupo aliyekataa kuolewa badae akakosa mume? Hii ipo katika karne hii ya millenium?naomba kuwakilisha
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hamna lolote!!Imani potofu tu ndo maana waliamini kwamba mtoto akianza kuota sijui ni meno ya chini au ya juu anatakiwa auwawe!
   
 3. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mwenzangu embu toeni mauzoefu mdongo wangu aondoe hofu, kachumbiwa na mkaka mmoja yeye anataka kutoa nje, ila ma mdogo kaleta hizi story za zamani zinamtia hofu.
   
 4. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Aisee hii sidhani kama ina ukweli japo kwetu pia kuna sis wangu alikataa mchumba miaka ya zamani na alikuwa boyfriend wake alipopeleka posa kwa wazaai akasita kuolewa akidai yule ni muislam na yeye mkristo, akapata mwanamme mkristo mapenzi motomoto walipofikia mbali kutaka kuoana akagundua jamaa ana mke baada ya ndugu mwingine kuona picha ya harusi kwenye magazeti chakavu, yule jamaa muislam alikuwa keshaoa tena mke mwingine, sista akajikuta mikononi mwa mwanaume abusive mwarabu na muislam kazaa nae watoto wawili na sasa hivi wameachana anaishi maisha ya upweke peke yake sanasana kawa mwizi kwa yule first love wake aliyemkataa
  Nahisi kuna pigo fulani mtu anapata akifanya haya hasa yale ya kuumiza sana mtu uliyekuwa nae, kama hivi unamkataa mchumba ambae ulikuwa nae muda mrefu kama boyfriend wako.Nakumbuka yule kaka wa kwanza alilia sana mpaka kulazwa. na haya ni malipo yake
   
 5. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mimi pia nilikataa mchumba wangu kuolewa. naendelea kuhesabu namba i hope hapa sasa kitaeleweka naomba yasinikute haya.pepo mbaya tokaaaaaaaaaaaa
   
 6. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #6
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Kama sijaelewa hiyo bold hapo
   
 7. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #7
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Imani tu ndugu yangu!! Mimi nina dada yangu alikataa wachumba saba wengine hata alikuwa hawajui lakini kaolewa vizuri na ana watoto wanne
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Mar 24, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Imani potofu tu.
  Ila hata kama ingekua kweli sio akili kumkubali mtu ambae hutaki kuolewa nae kisa uonaogopa kutokuolewa!!!Ni bora asiolewe kuliko kuingia kwenye ndoa na kutoka haraka au kunyanyasika ndani yake!!!
  Ila kama anataka kuolewa tu ili mradi mwambie akubali tu!
   
 9. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kiswahili kigumu mwali ila ndio hivyo
   
 10. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Soooooo sad story kwa hiyo anachakachuliwa kama mwizi wakati alikuwa na chance ya kutawala yeye jukwaa.maamuzi mengine bana. ila huwezi mlaumu mtu kwa wakati huo huwezi jua alikuwa anawaza nini, na kila mtu anapofanya maamuzi lazima akubaliane na matokeo. huyu alitake risk ila outcome yake ndio haikuwa nzuri
   
 11. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Huyu ni kiboko atakuwa mamaaa wa makamasutra, wachumba saba lazima atakuwa bomba kama wewe dena
   
 12. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  BlackBerry story ya sista ako inasikitisha ila naona mungu ndio alimpangia, ahsante kwa kushare nasi tunapata funzo fulani, ila huyu mdogo wangu hakuwa nae huyu jamaa.kamuona tu kaamua kumposa ki old fashion na yeye kwa sasa bado yuko chuoni ila hana bf unafikiri akubali kudate nae kwanza au ammwage tu
   
 13. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #13
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Siku nzima nilikuwa sijacheka umenifanya nicheke kweli asante u made my evening
   
 14. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Ahsante dena unafikiri akikubali kuolewa nae atakuwa amecheza pata potea? ila twende mbele turudi nyuma dada yako ana bahati wachumba saba wote aliwapiga chini?
   
 15. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  We mtoto huwa una mambo?? makamasutra nayo unayajua! hahahahahaaaaaa
   
 16. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hata mie nahisi ni nuksi fulani...:smash:
   
 17. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #17
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Nakwambia ni mzuri wa sura na umbo walikuwa wanakuja hata wengine hajawahi kuongea nao kumwambia kuwa wanampenda. Wawili ndo alikuwa anawajua hao wengine walikuwa wa njiani ooohhh huyu mtoto wa fulani amemaliza shule (darasa la saba) sio degree anafaa sana kuolewa si unajua mambo ya village tena mnajuana kama nyanya sokoni.

  Mie nilikataa wawili tu walinichumbia sina habari narudi shule naambiwa kuna barua za posa nikawaambia mshindwe mie mpaka nimalize shule kweli sikuolewa mpaka nimemaliza na nina kazi
   
 18. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #18
  Mar 24, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Kumbe dena mlikuwa primary? mwenzko huyu yupo 27yrs karudi shule bado ndio anamalizia, mie kwa mbali natamani amkubali ila amwambie wa date kwanza kuonana tabia ndio amkubalie.na ma mdogo nae ndio kaja na hiyo single basi anahaha kutafuta ushauri
   
 19. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #19
  Mar 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 253
  Trophy Points: 160
  Ndio mimi nilikuwa mdogo bado. Hakuolewa lakini alienda mpaka form iv ndo akaolewa baadae ndo akaja kuendelea na chuo. Mmmhh hiyo 27 tena anakataa nini sasa au nae hajatulia?? Mwambia aolewe
   
 20. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #20
  Mar 24, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  kwaiyo ata km ajampenda amkubalie tu kisa KUOGOPA LAANA?
  unajua maana ya laana lakin ?
  km ni ivo bas ata ukimkataa mkaka akikutaka bas utapata LAANA kwamba autatongozwa teeeeeeeeeeena!
  iyo kitu hamna ...km mkrisru wanasema mume bora anapatikana kwa goti na kuomba sio mtu akija ata km teja,mwizi tu umkubalie eet ukikataa LAANA Inakuja....MISUSE OF NENO LAANA......divide by uoga multply na hamu ya bnt kuolewa na wazee kuonekana wameoza matokeo yake ndo ayo ata akija kibaka kukuchumbia inabd ukikubali ukidiss laana ..mhh mhh apana nooo!

  mwambie dogo atupe kule izo iman potofu
   
Loading...