Mh! Mbona haya madude yameongezeka sana nchini miaka ya karibuni?
Swali gumu kisayansi na zito,gumu kijamii.
Si Tanzania tu bali worldwide kuna ongezeko la matetemeko.
Zipo sababu nyingi zinazopelekea matetemeko,hivyo kujua specifically haya ya sasa East Africa sababu ni zipi inakuwa ngumu hadi research za maana na ngumu kisayansi zifanyike.
Hata hivyo vipo vitu vya kueleweka ambavyo vinaweza kuhusishwa na hali hii ya sasa hivi.
Chanzo kikuu cha matetemeko ya A.Mashariki huwa ni bonde la ufa.
Ukitazama haya yote yaliyotokea karibuni ni maeneo lilikopita bonde la ufa.
Sifa ya matetemeko ya rift valley huwa sio makubwa kiivyo.Yanatuumiza sababu ya umaskini,hatutayarishi mazingira yetu kama vile namna ya ujenzi,maeneo ya kujenga etc.
Labda kwanini frequency imeongezeka ndio hoja ya msingi na ngumu sana.
Kipindi hiki cha March huwa jua linakuwa ikweta utosini,ni wakati wa full moon pia.Inadaiwa uvutano wa jua,mwezi na dunia ndio unaleta shida.Gravitational pull inaongezeka na maeneo yenye ardhi nyepesi kama kwenye fault lines kunapata msukosuko na seismic activities zinakuwa high,maeneo yaliyo karibu na ikweta yakiathirika zaidi.
So dunia ikipata msukosuko wowote,ni rahisi kusababisha mtetemo Rift Valley.
Jambo lingine ni kuwa hapo penye bonde la ufa ni eneo ambalo tectonic plates mbili za Somali na Nubian zinaachana taratibu na baada ya miaka mingi Somali plate itajitenga na the rest of Africa na kuwa kipande ardhi binafsi like island,so in a million years East Africa yote inaweza kuwa kisiwa. Forces zinazotenganisha plates hizo mbili zinasababisha ardhi kuwa nyepesi kwenye ule ufa (thin crust) na msukumo toka ndani ya dunia unaongezeka na kusababisha seismic activities.Hivyo tutegemee constant earthquakes ndogo ndogo katika rift valley kwa miaka yote,provided hakuna jambo geni litakalosababisha ongezeko la seismicity.However,hii factor ya rift valley haijibu swali lako linalohusu "ongezeko la matetemeko(frequency),mpaka labda kuwe na kitu kigeni kinachobadilisha mwenendo wa formation ya kijiografia ya eneo hilo,so inaweza kuwa utengano wa hizo plates umefikia kiwango cha kutrigger seismicity au kuna jambo lingine linalocapitalize maumbile ya rift valley na kusababisha seismicity.
Kuna jambo lingine jipya linalozungumzwa sana na wanasayansi duniani.Hili ni global,na kama lipo sahihi basi tuna wakati mgumu kidogo miaka inavyozidi kusonga kwa generation hii yetu.
Inasemekana jua lina athari ya moja kwa moja kwa weather na dunia yenyewe na kusababisha vitu kama matetemeko,mafuriko,ukame,hailstorms,etc.
Kuna kitu kinaitwa solar cycles,ni mzunguko wa miaka 11 wa kuchemka na kupoa kwa jua.Linapochemka wanaita solar maximum,linapopoa wanaita solar minimum.Kuna wakati vipindi vya kupoa vinakutana vyenyewe na kupoa kwa muda mrefu(miaka),hivyo wanaita grand solar minimum/minima.
Sasa huku kuchemka na kupoa kwa jua kuna athari ya moja kwa moja kwenye mabadiliko ya hali ya hewa nje(space weather) na ndani ya dunia (atmosphere).
Kuna kitu kinaitwa galactic cosmic rays(gcr),aina fulani ya mionzi ya kinyuklia inayotoka sehemu nyingine ya ulimwengu (milky way) na kuingia kwenye solar system yetu.Research za hivi karibuni zimeonyesha pia mionzi hiyo inaweza kuwa intergalactic(kutokea malimwengu mengine outside our milky way).
Imegundulika mionzi hiyo ina athari kwa tabia za kijiografia za dunia kwa kadri ya kiwango cha mionzi hiyo kinavyopata nafasi ya kuifikia dunia.Ni mionzi ya hatari.
Mojawapo ya athari ya mionzi hiyo iliyogundulika ni kuwa inachangia
kutengeneza mawingu(cloud cover).
Inapoingia kwenye anga la juu,mionzi ile inareact na molecules za gases zinazohusika kutengeneza maji na kufanya precipitation yake (kugandisha).
Mojawapo ya kazi ya mawingu ni kureflect mwangaza(mionzi) wa jua kurudi kwenye jua ili isizidishe kiwango cha joto duniani.
Sasa kuna natural mechanism inayoendesha mfumo wa utengenezaji mawingu na kiwango cha GCRs kinachoruhusiwa kupenya anga ili kufanya kazi hiyo.Mfumo huo unategemea solar cycles.
Jua linapochemka(solar maxima) usumaku wake(magnetic field) unaongezeka na kuwa strong,consecutively na usumaku wa dunia pia huongezeka na kuwa strong.
Usumaku wa jua hudhibiti(kuzuia) uingiaji mkubwa wa gcrs kwenye anga.Hivyo cloud formation inakuwa ndogo,as a result more sun rays zinaingia duniani na joto linaongezeka.
Wakati wa solar minima,(kupoa),usumaku wa jua hupungua,hivyo gcrs nyingi hupenya anga,cloud formation inakuwa kubwa,mionzi ya jua huwa reflected kwa kiwango kikubwa na hivyo joto kupungua duniani.
Kupungua kwa joto chini duniani na kuongezeka kwa cloud formation juu angani kunaathiri evaporation,hivyo unyevunyevu(humidity) unapungua na kuathiri mfumo wa kutengeneza mvua na mfumo wa kuzalisha chakula cha mimea.Hii inaleta ukame na mafuriko(mvua zinakuwa haba na zikiachia mara moja moja zinakuwa kubwa sana).
Kama kiwango cha solar maxima kikiwa kikubwa kwa minajili ya kukaa muda mrefu(grand solar maxima),gcrs(cosmic rays) zinapata nafasi ya kushuka hadi kwenye surface ya dunia.Kwa sababu ni nuclear charged particles,along the way zina tabia ya kureact na natural chemicals angani na kuvuruga tabia za mifumo ya hali ya hewa na kusababisha vitu kama hailstorms,na weather disturbances nyingine.
Pia gcrs zina tendency ya kureact na madini ya silica,yaliyomo kwenye miamba,na hili huleta disturbances kwenye fault lines, huleta ongezeko la volcanic activities such as earthquakes,tsunamis etc.
Wanasayansi wanasema yes,kuna ongezeko la gcrs kwenye anga la dunia katika kipindi hiki cha miaka ya karibuni ambapo jua limeanza kupoa.
Na ni kipindi hiki cha kuanzia 2018 dunia inaanza grand solar minimum ambayo hatujawahi kuishuhudia katika enzi zetu,ilitokea nyuma sana kizazi hiki cha teknolojia hakikuwepo.They called it little ice age.
Kisayansi,wanasema sio kwamba hiyo global cooling italeta shida ya baridi kali sana,bali hayo mambo ya kisayansi niliyoeleza hapo juu ndio itakuwa tatizo linalokuwa experienced zaidi from now kwa kadri solar minima inavyozidi.
Huu ugunduzi mpya pia unaleta sababu mpya ya chanzo kikubwa cha global warming,sio man made bali ni haya mabadiliko ya mifumo ya kimaumbile ya huko angani,jua likiwa main culprit.
Wakati wa solar maxima weather ilikuwa so stable but beyond 2000 ilipoanza cooling,weather disturbance imekuwa kubwa.
Ndivyo wanasayansi wanavyosema duniani huko.
Kumbuka East Africa ipo along equator,hiki ni kipindi ambacho jua liko karibu na Ikweta,sasa kama hayo mengine yapo na sisi tuna hii rift valley yetu hapa,huenda disturbance ikawa kubwa kwenye ule ufa.
Mwaka jana Kenya ulitokea ufa mkubwa mno along rift valley.ntaweka video hapo chini.Wanasayansi wanasema ndio safari ya "wana wa israel kwenda KISIWA cha ahadi imeanza"