Kumekucha, List of shame inanukia!

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,882
35,899
Kama ni bahari basi kumechafuka.

Tundu Lissu yuko ndani ya nyumba na Lema anapiga jaramba tayari kuingia kuchukua nafasi ya mtu.

Upande wa pili hali si hali mwangwi ungali unaendelea kurindima:

Screenshot_20230131-174712.jpg

Screenshot_20230131-174638.jpg

Screenshot_20230131-172039.jpg

"Pana mafisadi mapapa hapa. Manono kuliko ya enzi zile."

Ama Kwa hakika historia haiachi kujirudia.

CHADEMA, kumekucha muda wa "list of shame" ni huu.
 
Mnapenda udaku!!!.. si mlisema mambo ya haki za binadamu.. hadi mtu akutwe na hatia au?
Kwani hatia ni ipi? Mapesa yamefikaje kwenye account zisizojulikana china huko?

Ina maana, bank kuu, wizara ya pesa, wale vigogo wenyewe wa plea bargaining hawakujua?

Kwamba timu nzima ya vigogo serikalini wenye dhamana ya kutulindia mali haikujua?

Si tulikwisha kubaliana kuwa ukishikwa na exhibits hakuna haja ya uchunguzi, ama?
 
Kuwa makini na kitu kinaitwa "List of Shame" wakati mwiingine unaweza kuwa mtego wa kujitega wenyewe, kama kweli ni list of shame basi pawepo na ushahidi wa utosha kuthibitisha hilo, sio siasa.

Vinginevyo kuna kuumbuka, pale ambapo yule utakaemwita mwizi, siku ikifika akapiga u-turn akahamia upande wako, hapo unakuwa mtihani, na kwenye hili tusijidanganye utamkataa kujiunga na chama chenu.
 
Cocochannel umefufuka,karibu tena naona lile zuio lilikupeleka likizo kwani kibarua kilikata,naona unapiga jaramba pamoja na Magonjwa Mtambuka na Hata Jane Lowasa

🤣🤣🤣 Huwa nipo..
Nasema tenwa hizo kazi mnazonipatia humu za maneno yenu.. mnipege misharaha basi.. 🤗🤗🤗
 
Ni ngumu sana kuitetea CCM; itakudhalilisha tu mahali fulani.

Serikali yetu imejaa mambo ya ajabu sana.
 
Kam vile ujuio wa lisu haijabadili lolote wananchi wengi wamewapuuza

Sababu unajuwa Ni nn ninkwamba wananchi wana njaa sana
 
Kuwa makini na kitu kinaitwa "List of Shame" wakati mwiingine unaweza kuwa mtego wa kujitega wenyewe, kama kweli ni list of shame basi pawepo na ushahidi wa utosha kuthibitisha hilo, sio siasa.

Vinginevyo kuna kuumbuka, pale ambapo yule utakaemwita mwizi, siku ikifika akapiga u-turn akahamia upande wako, hapo unakuwa mtihani, na kwenye hili tusijidanganye utamkataa kujiunga na chama chenu.

Siasa za kuvizia vizia kama fisi haziwezi kutufikisha mbali. Koleo na liitwe kwa jina lake.

Kwanini tusiwe wawazi kuwa msimamo wetu ni huu. Anayetaka kuja karibu asiyetaka Kwa heri?

Kwa nini tuogope kuwaaibisha wanaostahili kuaibishwa?

Kwa nini tuwepo au tuishi kiujanja ujanja? Kwani tunachokitaka hatukujui?

Ninakazia:

Huko bank kuu, wizara ya pesa, na vigogo walioshiriki kwenye wizi huu kujaribu kuwalinda au kuwaonea aibu hakumsaidii Samia, CCM, Chadema wala awaye yote.

"Mwizi ni mwizi tu. Mahali pake si ujaji mahakama kuu bali ukonga, segerea, au kisongo magereza huko."
 
Siasa za kuvizia haziwezi kutufikisha mbali. Koleo na liitwe Kwa jina lake.

Kwanini tusiwe wazi tu kuwa msimamo wetu ni huu anayetaka kuja leo karibu asiyetaka Kwa heri?

Kwa nini tuogope kuwaaibisha wanaostahili kuaibishwa?

Kwa nini tuwepo kiujanja ujanja?

Ninakazia:

HuKo bank kuu, wizara ya pesa, na vigogo walioshiriki kwenye wizi huu kujaribu kuwalinda haimsaidii Samia, CCM, Chadema wala awaye yote.

Mwizi ni mwizi tu. Mahali pale si ujaji mahakama kuu bali ukonga magereza.
Tatizo sheria ya vyama vya siasa haisemi fulani akituhumiwa kwa wizi haruhusiwi kujiunga na chama cha siasa akipendacho..

Ndio maana nikaandika, ukituhumu, hakikisha una ushahidi wa kutosha, lakini sio kutoa tuhuma bila ushahidi.

Kule kusema msimamo wetu ni huu, hakuwezi kuwazuia wao kujiunga na chama chako wakiwa na madoa yao, hii tayari itaharibu taswira yako kwa jamii husika.
 
Kam vile ujuio wa lisu haijabadili lolote wananchi wengi wamewapuuza

Sababu unajuwa Ni nn ninkwamba wananchi wana njaa san
Ujio wa Lissu umeiweka agenda ya maisha magumu juu kuliko wakati wowote ule nchini.

Screenshot_20230131-174638.jpg

Si bungeni si mtaani.

Mwendo umekuwa wa kukurupusha mapanya. Bashiru kasikika.

Kumbe wezi wetu wengine sasa tunajua ni vigogo. Kaa Kwa kutulia usubiri orodha yao.

Kwamba kule wizara ya pesa au bank kuu hawakujua?
 
Tatizo sheria ya vyama vya siasa haisemi fulani akituhumiwa kwa wizi haruhusiwi kujiunga na chama cha siasa akipendacho..

Ndio maana nikaandika, ukituhumu, hakikisha una ushahidi wa kutosha, lakini sio kutoa tuhuma bila ushahidi.

Kule kusema msimamo wetu ni huu, hakuwezi kuwazuia wao kujiunga na chama chako wakiwa na madoa yao, hii tayari itaharibu taswira yako kwa jamii husika.

Vyama vya siasa havitegemewi kuwa na malaika. Uchafu wa mtu ni wake labda kama una baraka za chama chake.

"Vyama vya siasa vinategemewa tu kuwa na agenda za maana zenye kuwavutia watu."

Agenda zetu za wazi za kutaka usawa, haki na maisha bora kwa watu haziwezi kumvumilia mwizi bila kujali alipo.

Kwamba kuna rundo la mapesa lilishia China? Tunataka ushahidi upi kuwaaibisha wenye kuhusika? Labda kama tunadhani kuna majini yalifanya hilo?

Kwani waliozikusanya pesa hizo wanasema walizipeleka wapi au kwa nini walizipeleka huko? Kwa nini kuoneana aibu au kulindana hapa? Kila mmoja na akaubebe msalaba wake mwenyewe.

Kwamba hatujui mlolongo wa utunzaji wa pesa za serikali? Kwamba hata kikinuka kama hivi nani wanapaswa kuwajibika hatuwajui? Labda kama ni shamba la bibi.

Ushahidi upi tunaoutaka?

Kwani mzee Lowassa na akina Msabaha waliachia ngazi kwa ushahidi upi? Wengine si walisema walikuwa mbangusilo tu?

Au list Ile pendwa of shame ilituathiri sisi nini? Haikusaidia kuwawajibisha watu ile?

Wana tuingieni chimbo. Wote waliohusika kwenye hili wakapate kuanikwa peupe.

Hata kama Mbowe, Lissu, Samia, Mpango, Luoga, Dotto, Zitto, Rungwe, wewe, mimi nk walihusika na waanikwe tu!
 
Back
Top Bottom