Kumbukumbu na shukrani kwa ushirikiano

Kumbukumbu na shukrani kwa ushirikiano

Nimesoma kuanzia comment ya kwanza hadi sasa, hakuna aliyesema kuwa hukufaa..
Huu ni ujumbe kwa mh RAIS kuwa inabidi asikilize sauti za watanzania kukuhusu.
mh, umekuwa sehemu ya reforms katika wizara hyo, umekuwa sehemu ya jamii, umeokoa haki za wengi, haukusita kushirikiana na jamii ulipotakiwa kufanya hivo.

Mh. Rais ana deni la kukurudisha katika wizara hii..mimi nitatunza namba zako hadi mwisho dahari.

Mungu akujalie maisha marefu yenye heri na baraka uendelee kututumikia.
 
INAPENDEZA SANA KWA KWELI...

ninachokupendea huna vinasaba vya kujikweza(kunyanyua mabega) kwani umekua ukimsikiliza kila mtanzania wa kawaida ukipata muda, kwenye hilo nini ushaidi na hongera kwa hilo mweshimiwa
 
😀spana kama spana. Ndani ya moyo wa mtu ndiyo kuna spana za kumuangamiza. Hizi za walimwengu ambazo, watu wanakutana kwa kusudi lao juu yako, na wanaambukiza wengine hata kuuliza ukweli hawataki, halafu wanatafuta upande hasi tu kuhusu wewe, upande chanya wanafukia, mimi nazionaga kama burdani ya wakati tu, na wakati ukishapita, yote hudhihirika uhalisia.

Tuendelee kumshukuru Mwenyezi Mungu, mfalme wa nyakati.
Mheshimiwa hizi congratulations siyo unafiki ni real kabisa mimi kama mkongwe wa JF. Kingine sisi wengine tutakufuata hukohuko utakapogombea ubunge tuje tukupigie kura.
 
Ndioo, mwakani wizard ianzishe mfuko kama wa Sheikh Kishki watu walipiwe mahari
 
Pesa za bure huwa zinaliwaje kwanza mbona unaleta stori za ramli chonganishi rafiki
Kugonga gonga meza tuuu bungeni, na kuzurura zurura tu in the name of "ziara za kikazi" na ma camera kibao kuwafokea wananchi huku mnawaza chaguzi . Kwakifupi hamstahili pesa mnazolipana kwenge kilinge chenu cha bunge na hivyo viinua mgongo. Kwa mabadikiko gani mnayoleta nchi masikin miaka zaid ya 60 toka uhuru? Heb mheshimiwa we mwenyewe sema ukweli.
 
Kugonga gonga meza tuuu bungeni, na kuzurura zurura tu in the name of "ziara za kikazi" na ma camera kibao kuwafokea wananchi huku mnawaza chaguzi . Kwakifupi hamstahili pesa mnazolipana kwenge kilinge chenu cha bunge na hivyo viinua mgongo. Kwa mabadikiko gani mnayoleta nchi masikin miaka zaid ya 60 toka uhuru? Heb mheshimiwa we mwenyewe sema ukweli.
Inategemea uchambuzi wako unafanyika ukiongozwa na idadi ya D ngapi.
 
Wasaalam.

Tarehe 14 Julai, 2025 nimekuwa sehemu ya Kikao cha mwisho cha Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Sita tangu iingie madarakani, kilichofanyika Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 14 Julai, 2025.

Picha ya 1 ni ya kumbukumbu ya Wajumbe wa Baraza tukiwa pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka.

Picha ya 2 nikitembea kwenye viwanja vya Ikulu ya Chamwino kuwahi Kikao husika.

Hakika, Mungu ni mwema kutuwezesha kuiona siku hii ya kihistoria⚘️🇹🇿.

Ahsanteni sana Wananchi wote na Wadau wote kwa ushirikiano wenu.

Tuendelee kushirikiana daima kuelekea Uchaguzi Mkuu hapo Oktoba 2025✍️🇹🇿.
View attachment 3405905
View attachment 3405906
Thank you and bye bye u will back again Insha ALLAH.
 
Back
Top Bottom