Kumbukizi: Rais Idi Amin alipoanzisha Tume kuchunguza watu kupotea na kutekwa, ripoti haikuwahi kuwekwa hadharani!

Kumbukizi: Rais Idi Amin alipoanzisha Tume kuchunguza watu kupotea na kutekwa, ripoti haikuwahi kuwekwa hadharani!

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu,

IMG_20251229_011312_121.jpg

Mwaka 1974, Rais Idi Amin kupitia Tangazo la Kisheria Na. 2 la mwaka 1974 alianzisha Tume ya Uchunguzi kuhusu Watu Waliopotea nchini Uganda, ikiwa ni jitihada ya kuchunguza matukio ya watu kutoweka yaliyoripotiwa tangu alipochukua madaraka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1971. Tume hiyo ilipewa jukumu la kuchunguza matukio hayo, kubaini waliohusika, na kutoa mapendekezo ya namna ya kukomesha ukiukwaji huo wa haki za binadamu, ambapo tume hiyo lifanya kazi licha ya Wauganda wengi kuikataa na kuhoji uhalali wake.

Tume ilifanya kazi kati ya mwaka 1974 na 1975, ikiendesha vikao vya hadhara, kusikiliza ushahidi wa mamia ya waathirika na mashahidi, na kurekodi kesi mbalimbali za watu waliodaiwa kutekwa au kupotea. Katika uchunguzi wake, tume ilihitimisha kwa kulaumu vyombo vya usalama (kama jeshi), kwa vitendo vya utekaji na ukiukwaji wa haki za binadamu, bila kumhusisha moja kwa moja Idi Amin katika matukio hayo.

IMG_20251229_011319_068.jpg

Ripoti ya mwisho ya tume hiyo haikuwahi kutangazwa hadharani. Badala yake, iliwasilishwa kwa Idi Amin pekee na kuwekwa kuwa siri. Hatua hiyo ilifuta uwezekano wa uwajibikaji wa wazi, kuzuia utekelezaji wa mapendekezo yoyote ya mageuzi ya vyombo vya usalama, na kudhoofisha haki kwa waathirika na familia zao.

Kwa mujibu wa taasisi za kimataifa; International Center for Transitional Justice (ICTJ) na African Transitional Justice Hub, tume hiyo ilibaki kuwa jaribio lililoshindikana la kuleta uwajibikani kwenye matukio hayo ya watu kutekwa na kutoweka.

IMG_20251229_011316_105.jpg

Baada ya kumalizika kwa kazi ya tume hiyo, makamishna walitishiwa na kulengwa na dola kama hatua ya kulipiza kisasi, kwa sababu ya kuashiria uwezekano wa Amin kuhusika na kutoweka kwa watu kwa nguvu (USIP, 2009). Mwenyekiti wa tume alipoteza wadhifa wake serikalini, Kamishna mwingine alidaiwa kufunguliwa mashtaka ya uongo ya mauaji na kuhukumiwa kunyongwa, huku kamishna wa tatu akikimbia nchi ili kuepuka kukamatwa (Hayner, 1994). Inadaiwa kuwa makamishna watatu kati ya wanne walipotea. Kutokana na hali hiyo, tume hiyo haikuwa na athari yoyote au ilikuwa na athari ndogo sana kwa nchi wala kwa namna Amin alivyoendesha utawala wake hadi alipoondolewa madarakani mwaka 1979.

Licha ya Tume hiyo kutokuwa na athari yoyote chanya kwenye vitendo vya utekaji, watu kupotea na ukandamizaji mwingine wa haki za binadamu, Amin aliweza kuitumia kujionesha kama kiongozi mwenye kujali, jambo lililomsaidia kujijengea mtaji wa kisiasa. Hili linathibitishwa na kuchaguliwa kwake kuwa mwenyekiti wa Umoja wa Nchi za Afrika (OAU) mwaka 1975, mara tu baada ya kumalizika kwa kazi ya tume hiyo. Aidha, Uganda ilichaguliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu mwezi Mei 1976 (Decker, 2013).

Source African Transitional Justice Hub
 
"His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Haji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular"
 
"His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Haji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular"
Kwanini madikteta vilaza, waliokimbia shule, wauaji huwa wanapenda Title ya Doctor, hawajiamini?
 
Positive side ya tume ya Idd Amin ilikuwa imenyooka ikasimamia haki na ukweli na kufanya uchunguzi wa uwazi na ukweli kwa kuendesha vikao vyake hadharani, live.

Mwisho wa siku ikasema ukweli kwa kulaumu vyombo vya ulinzi na usalama kwa vitendo vya utekaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
 
Naona mfumo wa Samia upo kama wa Idd Amin. Amin alikuwa na watu makatili walipanga na kuteleza uhuni kama Maliyamungu, Mustapha Adrisi, Butabika, Lumago.

Samia ana Abdul, Haji Kheir, Mafwele, Mombo, Wambura, CoC Haji Othman.

Amin alijiita kiongozi wa binadamu,wanyama, samaki na aliyewashinda mabeberu wa Kiengereza. Samia anasema who are you, hawatutishi, kwanza wanatupa vijisenti.

Abdul ni kama Maliyamungu kwa Samia. Ukatili mkubwa wanaofanya inawezekana unachangiwa sana sababu sio Mtanganyika kama Maliyamungu Mkongo alivyokuwa anawaua Waganda kwa ukatili mkubwa.
 
Kesi ya Tanzania inaenda kuwa kama Rwanda, mauaji yametokea, ila haki itakuja tendeka baadae sana, na kila mmoja atafikishwa kwenye chombo cha sheria. Kwenye hii Dunia, hakuna viongozi au utawala uliofanya mauaji ya alaiki, na likaachwa lipite, haijawah tokea na haitatokea. Mark my words.
 
Positive side ya tume ya Idd Amin ilikuwa imenyooka ikasimamia haki na ukweli na kufanya uchunguzi wa uwazi na ukweli kwa kuendesha vikao vyake hadharani, live.

Mwisho wa siku ikasema ukweli kwa kulaumu vyombo vya ulinzi na usalama kwa vitendo vya utekaji na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kusema ukweli kwa kulaumu vyombo vya ulinzi huku kuacha Mkuu wao anaewaongoza na kuwapa order! Aaah bana Mkuu
 
Idd Amin aliunda tume ya kuchunguza watu kupotea na wengine kuuwawa...
Tume ilimkuta na hatia Idd Amina...lakini kwa mamlaka yake aliamua KUJISAMEHE MWENYEWE
 
Kusema ukweli kwa kulaumu vyombo vya ulinzi huku kuacha Mkuu wao anaewaongoza na kuwapa order! Aaah bana Mkuu

Kimsingi lawama zilielekezwa kwa Idd Amin ila hawakutumia lugha ya moja kwa moja. Ukisema utekaji, mauaji, utesaji umefanywa va vyombo vya ulinzi na usalama kama jeshi, polisi, usalama na wakuu wa hivyo vitengo wanahusika. Ina maana hata Mkuu wao anahusika.

Kila siku Rais anapokea briefing ya kila kinachoendelea nchini kutoka kwa hawa wakuu wa hivi vyombo. Tukio lolote kubwa la kuua maelfu lazima Mkuu wao atoe go ahead, kuruhusu au kukataa.
 
Back
Top Bottom