KUMBUKIZI: Abajalo Vs Sparrow, Van Dame anachukua maamuzi ya kijasiri, Louis Mfede anausimika Ufalme wake, Kally Ongala anaamua Mechi

Gang Chomba

JF-Expert Member
Feb 29, 2008
20,301
4,681
Ukiniuliza kule Ulaya ni Mshabiki wa Timu gani basi ni wazi kuwa ntakujibu Mimi ni Mshabiki na Mfuasi wa AC Milan.

Ukija Bongo ukiniuliza basi ntakwambia nipo Yanga, lakini pia ni mshabiki lialia wa Tangu na Tangu wa Club Deportivo Abajalo maarufu kama Abajalo Mnyama Mkubwa yenye Maskani yake pale Estadio di Mashujaa pale Sinza.

Ngoja Leo nikupe kisa kimoja kulihusu chama hili la wana lililowahi kutikisa Soka la Mchangani miaka ya 90s na miaka ya 2000.

Siku moja bana pale Makulumla ilipigwa Mechi ya mwisho ya makundi itakayo amua ni timu ipi itakwenda kwenye hatua ya 16 bora kati ya Abajalo na Sparrow.

Kwenye kundi hilo palikuwa na machama kama Abajalo, Messina, Sparrow, TP, Sinza Star, na Kijitonyama Star.

Kwenye Mechi hio Abajaro Ngilimaa walikuwa wakihitaji sare tu kufuzu na Sparrow walikuwa wakizihitaji alama 3 kwa hamu na gamu ili wapate kuungana na Messina ambao walikuwa tayari waneshafuzu.

Sparrow iliokuwa inaundwa na wachezaji waliokuwa wanatokea Maeneo ya kuanzia Kijitonyama Mabatini mpaka maeneo ya Wanyama Mori huku ikiwachukua Nyota wengine wa maeneo ya Karibu na Uwanja wa El Santiago di Mapambano uliopo maeneo ya Mapambano walikuwa wapo karibu kabisa na Maskani ya Klabu ya Abajalo na hata vijiwe walikuwa wakiingiliana.

Kwa kifupi miaka ile hizi timu za Abajalo, Sparrow, TP, Sinza Stars, Wakushi na machama mengine yalikuwa yanaundwa na wachezaji wa Maeneo ya Sinza na Kijitonyama na Mwenge ambayo ni maeneo yalioungana na vijana na masela wao wengi walifanana kwa tabia na hata makuzi.

Mapema Siku ya Mechi mwendo wa Saa 5 Asubuhi Nyota wa Abajalo Louis Mfede alitimba kwenye maskani ya Sparrow kwa ajili ya kubariz na wana.
Kama kawaida ya Vijana wa maeneo ya Sinza na pembezoni wanapokutana basi lazima Pombe inywewe saana.

Masela wa Sparrow walipomuona Nyota wa Abajalo ametimba maskani hapo basi wakaangusha Bapa kisha wana wakaanza kugonga Mtungi sambamba na Mfede.

Tungi liliendelea na mpaka inafika mida ya saa 9 Alaasir Mshambuliaji huyo Nyota wa Abajalo alikuwa nyakanyaka.

Masela wa Sparrow wakasema naaam, tumeipunguza nguvu kubwa ambayo Abajalo wangeitumia kutuangamiza.
Na hivyo wakajiandaa pale kisha wakaita Gari Basi na kuamsha zao kuelekea Estadio di Makulumla pale MwembeChai huku wakimuacha Mfede akiwa chakali palepale.

Kufika Kinesi Mwembechai Sparrow wakakuta Abajalo wameshafika Uwanjani na wana miamba yoote kasoro Louis Mfede.
Siku hio Abajalo ilikuwa na Nyota kama Roberto Kalikawe, Daniel Peter, Shomari Show Me the Way, Baba Dimo, Modest na Kali Ongala, kwa hakika mwamba pekee aliekosekana Siku hio alikuwa ni Louis Mfede Mtu ambae inaaminika alikuwa na kipaji cha Soka kuliko washambuliaji woote kwenye Kaunti ya Sinza na maeneo ya Jirani.

Basi mpaka filimbi ya kwanza inapulizwa Abajalo walianza mechi bila ya kuwa na Nyota wao na mshambuliaji wao huyo ambae mara zoote alikuwa akiwapa matokeo mazuri. Kwa kifupi Mfede aliibeba Mgongoni Abajalo Siku zote za maisha yake ya Soka na aliitumikia kwa Moyo mmoja.

Sparrow waliutawala saana mpira kwa kipindi choote cha kwanza huku nyota wao kama Saga, James Kabambo, Kipago, Muba Semtumbi, Samora, Ally Zomboko na Willy Buyoya wakitakata sana.
Kwa kifupi hii mechi ilikuwa ni ya kukata na Shoka na hakika siku ile vipaji viliumana pale uwanjani na mpaka Filimbi ya mapumziko inapulizwa mechi ilikuwa patulo ya 0-0.
Kwa jinsi Sparrow walivyo tawala Soka kwa kipindi cha kwanza ni dhahiri kuwa kila mmoja pale Uwanjani aliamini Abuja angekufa Siku hio.

Lakini kipindi cha pili wakati kinaanza Watu walishuhudia geti la Uwanja wa Makulumla likifunguliwa mpaka mwisho tena kwa nguuvu sana.
Kila mmoja Uwanjani hapo alishtuka na kutaka kujuwa ni nini kinaendelea Uwanjani hapo?!

Mara Paaah umma wa Soka uliokusanyika ukamshuhudia Shabiki kiongozi wa Abajalo na Mwamba aliekuwa akitikisa kwa Ubabe Dar es Salam nzima Ayou Mkobo maarufu kama Jean Cloude Van Dame akiingia Uwanjani hapo huku akiwa kaushika Mkono wa Mfede uliokuwa umepita nyuma ya Shingo yake na Mkono mwingine akiwa amemkumbatia Nyota huyo.

Moja kwa Moja Mfede alifikishwa kwenye Benchi la Abajalo na kisha akapewa Maji ya Kunywa ya Baridi na kumwagiwa Maji meengi sana ya Baridi Mwilini. Kisha baada ya hapo Mfede akaelezwa aende kwanza kukaa Juani. Huku kipindi cha pili kikiwa kinaendelea na hapo ikiwa ni kama mwendo wa dakika za 60 Mfede akaambiwa arudi kwenye Benchi na kisha akamwagiwa tena Maji ya Baridi na baada ya Hapo akaanza kutroti.

Yowe likalipuka tulipokuwa tumejikunyata washabiki watiifu wa Abajalo huku upande wa Sparrow hali ikawa tofauti kwani washabiki wao weengi waliishiwa nyimbo na ukimya ukatawala.

Nakumbuka ilikuwa ni dakika ya 75 Ubao wa kamisaa ukainuliwa na Abajalo wakafanya mabadiliko na hatimae game changer akaingia.
Huku walinzi wa Sparrow wakiwa bado wana mdharau Mfede kwa kuwa waliishuhudia hali aliokuwa nayo tangu Asubuhi, Mfede aliupata Mpira mmoja kisha akamzunguka Mlinzi wa Sparrow na kuachia kigongo ambacho kilikwenda kula nguzo na kutoka Nje.

Baada ya shambulizi hilo sasa Sparrow wakahamaki na kugundua kuwa mission yao imefeli, na Abajalo wamekamilika na wanaitaka Mechi hio ili wafuzu kwenda hatua inayo fuata.
Sparrow walikuwa wamechelewa, Sparrow walishindwa tena kuwakabili Abajalo kwani Mfede aliingia na kwenda kuua ulinzi wa wapinzani na kupindua mechi na utawala woote wa Sparrow, huku sasa kiungo cha Abajalo kikianza ku dominate Mechi hio.

Maji ya jiooni Louis Mfede anapiga chenga wachezaji wawili wa Sparrow, huku mabeki wa Timu hio wakiwa wamejipanga mtego wa Offside, Mfede anapiga pasi ya mwisho inayokwenda kutua kwa Kally Ongala na bila ajizi Ongalla anacheka na Nyavu.

Mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa Abajalo wanaibuka miamba katika mechi hio huku Sparrow inakwenda kupata anguko kisoka kwa maana toka hapo Sparrow hawakuweza tena kumudu kucheza na Abajalo na walipotea katika ulimwengu wa Soka.

JE UNAJUWA HATUA YA ROBO FAINALI ABAJALO WALIKUTANA NA NANI NA NUSU PIA ILIKUWAJE?!
NA JE UNAJUWA FINAL ILIKWISHAJE NA TIMU GANI ILINYANYUA NDOO?!

Endelea kunywa Mtori, Nyama utazikuta chini.
 
Haya ndio mambo ya kuongelea sasa kwa uandishi wa kutukuka.
Sio jamaa moja hivi linavaa viatu Kama mtumbwi vimekwisha upande kiasi kwamba hata likitembea linalalia upande mmoja,Lenyewe kutwa kuchwa linaongelea habari za uchawi michezoni na kujifanya linajua soka la bongo kuliko mtanganyika yoyote.
 
Haya ndio mambo ya kuongelea sasa kwa uandishi wa kutukuka.
Sio jamaa moja hivi linavaa viatu Kama mtumbwi vimekwisha upande kiasi kwamba hata likitembea linalalia upande mmoja,Lenyewe kutwa kuchwa linaongelea habari za uchawi michezoni na kujifanya linajua soka la bongo kuliko mtanganyika yoyote.
Hapa anasemwa Popoma au Likud, aisee hii story imekumbusha kwetu Yombo Dovya na timu yetu ya Liverpool...
 
Haya ndio mambo ya kuongelea sasa kwa uandishi wa kutukuka.
Sio jamaa moja hivi linavaa viatu Kama mtumbwi vimekwisha upande kiasi kwamba hata likitembea linalalia upande mmoja,Lenyewe kutwa kuchwa linaongelea habari za uchawi michezoni na kujifanya linajua soka la bongo kuliko mtanganyika yoyote.
Hahahahaha
 
Haya ndio mambo ya kuongelea sasa kwa uandishi wa kutukuka.
Sio jamaa moja hivi linavaa viatu Kama mtumbwi vimekwisha upande kiasi kwamba hata likitembea linalalia upande mmoja,Lenyewe kutwa kuchwa linaongelea habari za uchawi michezoni na kujifanya linajua soka la bongo kuliko mtanganyika yoyote.
@GENTAMYCINE
 
Kally Ongala alipokua mchangani alikua hatari sana, ila wakati anacheza Yanga alikua wa wastani.
Kuna mechi mmoja ya Watani, Mwameja aliteswa sana na Kally Mnyama alikufa 3.
Kally alikua hashikiki siku iyo.

Ilo dude linalo itwa Van Dame nahisi kiganja chake cha mkono kinakaribia futi mmoja Jamaa ana mwili mkubwa na angekua Mbele jamaa angekua mbalisana kwenye michezo.
 
Back
Top Bottom