Elections 2010 Kumbe yule mnajimu anachungulia humu JF

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
16,598
14,328
Baada ya tabiri zake mbili za hivi karibuni kuhusu uchaguzi kuonekana ni za uongo, yule mnajimu ameanza kutapatapa. Kwanza alitabiri kutokuwepo kwa uchaguzi mwaka huu 2010, pili akatabiri kifo cha mgombea maarufu wa urais kabla ya uchaguzi. Yote hayakutokea.

Humu JF tuliwahi kuandika kwa mzaha tu kuwa lazima jamaa atahusisha kifo cha kocha Syllesaid Mziray na mgombea urais Kuga Peter Mziray. Post hiyo iko HAPA.

Na kweli imetokea hivyo, nimesoma katika gazeti moja la udaku eti mnajimu anasema kocha Mziray aliingilia nyota ya mgombea urais Mziray. Nadhani huyu jamaa aliisoma ile post, ila naona wahusika wa hayo majina wamchukulie hatua ili aache kabisa kutabiri.
 

dotto

JF-Expert Member
Sep 29, 2010
1,725
252
Alishindwa kabisa kutuma majini yake kuua. Ni muuaji wa makusudi.
 

kaburunye

JF-Expert Member
May 12, 2010
674
72
Ni kweli ilikuwa amuue mgombea mmoja lakini naona imeshindana kwa sababu fulani fulani. Mzee alikabwa koo sana huyu ili asitekeleze uuaji alioukusudia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom