Kumbe Warusi walionywa kuhusu shambulizi wakapuuza wakasema ni Propaganda. Sasa imewatokea puani

Sexer

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
8,216
7,908
Yaani warusi wa Moscow wameambukizwa tabia za warusi wa tandahimba.
——––————————————————
Ikulu ya Marekani imethibitisha kuwa ilionya mamlaka za Urusi mapema mwezi Machi kuhusu kuwepo na uwezekano wa shambulio linaloweza kulenga “maeneo yenye watu wengi” mjini Moscow.

“Mapema mwezi huu, serikali ya Marekani ilipata taarifa kuhusu mipango ya shambulio la kigaidi mjini Moscow- hasa linalolenga mikusanyiko ya watu wengi, ikiwemo matamasha,” msemaji wa Baraza la Taifa la Usalama la Marekani, Adrienne Watson (pichani) amesema.

Marekani “iliwapa taarifa hizo mamlaka za Urusi”, aliongeza kusema.

Mwandishi wa habari wa BBC wa masuala ya usalama, Gordon Corera amesema Urusi ilipuuzia taarifa hizo ikisema ni “propaganda” – hata baada ya Marekani kuonesha wasiwasi huo kwa raia wake wanaoishi Urusi.
 
Back
Top Bottom