Jana jioni nilikuwa mahali having dinner with a friend, sasa kuna vijana kama wa4 walikuwa meza ya jirani wanakula na kunywa, baada ya muda jamaa mmoja kati ya wale wa4 akaanza kulia hadi ikabidi mwenzao mmoja aondoke nae akampakia kwenye gari haoo wakaondoka.
Sasa ndio tukawa interested kujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mpaka mtoto wa kiume atoe chozi namna ile, ikabidi tujongee tupate kuuliza maana tulihisi ni msiba.
Ndio tukapewa story;
Jamaa alikuwa na mchumba wake ambae wamedumu kwenye mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja na miezi4 na walitaraji mwezi wa6 mwaka huu wafunge ndoa. Na katika mahusiano yao walikubaliana hakuna kugegedana hadi watakapofunga ndoa.
Awali walikubaliana kuanza mipango ya kutambulishana mwezi wa11, na kijana alimpeleka binti kwao, ikawa imebaki kijana kwenda kwa akina binti na walikubaliana waende mwezi wa12, ila baadae binti akahairisha na kumueleza kijana kuwa isingekuwa muda mzuri kwani kwao kuna matatizo ya kifamilia.
Kumbe binti kule alikokua alianzisha mahusiano na kijana mwingine na mapenzi yalikuwa motomoto kabisa na walikuwa wakila tunda kama kawaida, baadae binti akanasa ujauzito na ndio kisa cha kumwambia kijana asubiri kwanza kwenda kujitambulisha.
Baada ya kunasa ujauzito wakakubaliana wahalalishe mahusiano yao kwa kutambulishana na waanze michakato ya kufunga ndoa na mwanaume alompa ujauzito. Mipango ilianza vyema kabisa na wakapanga kufunga ndoa mwezi wa4 mwaka huu.
Binti alishindwa namna ya kumueleza kijana ikabidi aanze visa tu, kwanza akamwambia kijana ameamua kurudi kuishi nyumbani kwao kwa muda maana mambo hayaendi vizuri hivyo hawakuonana tangu disemba, akimuuliza kuhusu mipango ya kutambulishwa ukweni anamjibu asubiri.
Sasa kati ya hao friends wake aliokuwa nao jana alipata habari bibie anaolewa na mipango iko hatua za mwisho kabisa. Jana ndio katika maongezi ndio anamwambia rafiki yake kuwa "yaani wewe na J kwa jinsi mlivyokuwa mnapendana nilijua mngeoana kabisa, kwani nini kilitokea mkaachana?" Jamaa akamjibu, "J bado tunapendana na hatujaachana na mwaka huu lazima tufunge ndoa Mungu akijaalia".
Rafiki mtu akahisi jamaa anatania.
To cut the story short, jamaa akaelezwa kila kitu na ili kuthibitisha akampigia rafiki wa J simu na akamthibitishia kuwa J anaolewa, ndio jamaa kupatwa na mshtuko na kuanza kulia.