Kumbe Viazi-mbatata ni jina la Kizungu! Wanyakyusa ni noumer!

kiswahili kinatohoa baadhi ya Maneno kutoka katika lugha za asili kikiwemo na kinyakyusa, kisukuma, kizaramo n.k, ama niseme kibantu. pia baadhi ya Maneno ya kiasia kama kiarabu, kuhindi n.k, kwahiyo tunaposema mbatata ni viazi vitamu, hili neno asili yake unyakyusani Mbeya. na viazi mviringo(vya chipsi) wao uita indofyania. Wasafya wao viazi mviringo ama viazi ulaya uita indokani. kwahiyo usibishe unapofahamishwa.

Kaka nilipobisha ni wapi? Hiyo msg yangu inaonyesha kubisha au kuelewa tofauti zetu?, sio kila mtu ni Mnyakyusa kaka, mimi nilichokuwa nasimamia ni Kiswahili ninachokijua kuliko hicho Kinyakyusa

Kama Kinyakyusa Mbatata ni sweet Potatoes ni sawa tu, ila ukoenda sokoni kwa Dar na kuuliza Mbatata watakupa viazi ulaya (Mviringo)
 
Nimejaribu kukupa mifano kadha ila naona kama umejikita katika ubishani, unaambiwa kuwa mbatata ni viazi vitamu wala sio viazi mviringo ama viazi ulaya, sasa kama viazi mviringo ndio viazi mbatata, kwa hiyo neno viazi ulaya limekusudia viazi gani? viazi vitamu(mbatata) ni vikongwe na ni asili yetu yaani afrika karibu yote. lkn viazi ulaya mviringo ama vya chips asili yake ni ulaya, ndio maana vikaitwa viazi ulaya, kama ulikuwa ujajua basi ukweli ndio huu.
 
Acha ubishi kaka, Mimi sio amnyakyusa wala sikijui, lakini uniambia kiazi mbatata ni kipi mimi ntakwambia ni viazi ulaya vile vya chips na ndio kiswahili vinajulikna hivyo
Kama Kinyakyusa Mbatata ni viazi vitamu ni sawa tu na wala usinilazimishe mimi kuwa mbatata ni viazi vitamu kwa lugha yangu ya Kiswahili Mbatata ni viazi mviringo

Hebu angalia hizi link uone viazi mbatata
Mbatata/Viazi Vya Nazi Kwa Nyama Ya Ng'ombe | Alhidaaya.com

The CEO Culinary Artist Tanzanian Executive chef Issa Kapande: JIFUNZE KUTENGENEZA CHAKULA HIKI MCHANGANYIKO WA NJEGERE NA VIAZI MABATATA
 
Acha ubishi kaka, Mimi sio amnyakyusa wala sikijui, lakini uniambia kiazi mbatata ni kipi mimi ntakwambia ni viazi ulaya vile vya chips na ndio kiswahili vinajulikna hivyo
Kama Kinyakyusa Mbatata ni viazi vitamu ni sawa tu na wala usinilazimishe mimi kuwa mbatata ni viazi vitamu kwa lugha yangu ya Kiswahili Mbatata ni viazi mviringo
Yaishe sikuwezi nimechemka Mimi nakupa mji.
 
Hata viazi vitamu mnaita mbatata!!! Viazi vitamu ni ni vile vyenye matembele viaz mbatata ndio tunavyokula na mayai yaan chips mayai
 
Sweet potatoes sio Viazi mbatata,
Sweet Potatoes ni Viazi Vitamu (kuna vyeupe na Pink)

Viazi Mbatata ni Viazi Mviringo au Viazi Ulaya- irish potatoes

Kwa kinyakyusa, viazi vitamu ni mbatata na viazi mviringo ni ndofania
 
Si vigumu vile. Jina la kisayansi huonyesha "batatas" ambayo ni karibu sana na "Mbatata". Wikipedia ya Kiingereza ina maelezo ya tahajia:
"The first Europeans to taste sweet potatoes were members of Christopher Columbus's expedition in 1492. Later explorers found many cultivars under an assortment of local names, but the name which stayed was the indigenous Taino name of batata." Kwa hiyo Wahispania (=Columbus) na majirani wao Wareno waliendelea na jina la "batata".

Wareno walileta mmea na jina pia Afrika kupitia koloni yao ya Msumbiji, sawa na jina la chakula kingine "Mahindi" ambayo ni pia kiasili ya Amerika lakini iliitwa "nafaka ya Uhindi" kwa sababu Wahispania na Wareno waliamini mwanzoni ya kwamba walifika Uhindi (kabla ya kutambua eti ni kontinenti mpya).

Wanyakyusa walipokea jina la "mbatata" kutoka majirani wa kusini; angalia hapa Mbatata (Malawian Sweet Potato Cookies) • Curious Cuisiniere Upishi wa Malawi)
 
Yani hata Mimi nilipata tabu kidogo nilipokua Mbeya na tulibishana Sana'a... Nilichogundua watu walioishi mwambao wa pwani viazi ulaya/mviringo wanaita mbatata ila Mbeya wao viazi vitamu ni mbatata...kwahiyo wote mpo sawa kulingana na ulipokulia.
 
Haya bwana shinda wewe.lakini si kweli unavyosema.ukweli ni mbatata ni viazi vitamu
Watu wa pwani hasa Zanzibar viazi mviringo vile vya chips wao huita mbatata. Huwa wanavitumia hasa kwa urojo. Wakati viazi vitamu nadhani wanaita viazi sukari. Hivyo yawezekana unaebishana nae ni mzanzibar.
mbatata= viazi vitamu (mbeya) nyakyusa.
mbatata = viazi mviringo pwani znzbr
 
Yani hata Mimi nilipata tabu kidogo nilipokua Mbeya na tulibishana Sana'a... Nilichogundua watu walioishi mwambao wa pwani viazi ulaya/mviringo wanaita mbatata ila Mbeya wao viazi vitamu ni mbatata...kwahiyo wote mpo sawa kulingana na ulipokulia.
Watu kama Eddy Love watakuona wa kuja, lakini ukweli unabaki palepale kwa sisi tuliozaliwa na kukulia Dar, mbatata ni viazi Ulaya au Mviringo
 
Back
Top Bottom