Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,442
Kwako mpenzi wangu wa zamani, ambaye ulinifikisha uliponifikisha kupitia utapeli wa kimapenzi ambao ulinifanyia. Kwako niliamini kabisa kwamba, nimepata mpenzi wa kweli na wa kuaminika, kumbe nilikuwa nimevaa mkenge, kama wanavyosema watoto wa mjini.
Tulipokutana kwa mara ya kwanza, Machi 16, 2002, nilikwambia ukweli wangu wote, kuhusu maisha yangu ya nyuma ya kimapenzi na hata familia yangu. Sikudanganya hata kidogo. Nawe kwa upande wako ulijifanya ati unaniambia ukweli kuhusu maisha yako, wakati ukijua kwamba, kila neno ulilotamka lilikuwa ni uongo mkubwa ajabu. Kila neno lilikuwa ni sumu ya nyoka moma.
Kwanza uliniambia kwamba, hukuwahi kuwa na rafiki wa kiume kwa sababu ya chuki yako dhidi ya wanaume. Uliniambia ati mwaka 1995, wakati ukiwa na miaka 18 ulibakwa na kijana mmoja mlipokwenda kwenye pikiniki na tangu hapo ukawa huwapendi kabisa wanaume. Nilikuhurumia na kukupa pole kutoka moyoni mwangu.
Niliona kuwa ni vizuri nikakuchukulia polepole ili unizoee na kujenga imani yako iliyopotea dhidi ya wanaume. Kwa hiyo tangu hiyo Machi 2002, sikukutajia mambo ya tendo la ndoa. Bila shaka unakumbuka kwamba, tulianza kushiriki tendo la ndoa Juni, 2002.
Siku hiyo ya kwanza ilinionesha kwamba, hukuwa mgeni wa jambo hilo, kwani ulishiriki kitaalamu sana. Nilijiambia kwamba, labda ulifundishwa unyagoni mambo hayo na uliyaweka ili uje uyatumie kwa umpendaye. Kama vile ulikuwa ukijua kilichokuwa kinaendelea kwenye kichwa changu, uliniambia kwamba, bibi yako mzaa mama alikuwa akikufundisha mambo hayo ili uje umridhishe mumeo.
Mwaka 2003, nilianza kupata taarifa zako. Nilipata taarifa kwamba, umewahi kuishi na mwanaume mwaka 1997 na mkazaa mtoto wa kiume. Niliambiwa kwamba, huyo jamaa alifariki mwaka 1999, kwa maradhi ya kifua kikuu na mwaka huo huo mtoto wenu wa mwaka mmoja alifariki pia.
Nilipata taarifa zaidi kwamba, mwaka 1999 hadi 2001, uliishi na wanaume wawili tofauti, mmoja akiwa ni Mnyarwanda. Niliambiwa mmoja kati ya hao alikuwa ni mgonjwa sana, wakati napewa taarifa hizo, na mmoja mliachana baada ya mkewe kutaka kukuuwa, kufuatia fumanizi.
Sikutaka kukurupuka baada ya taarifa hio, bali niliendesha uchunguzi wangu na kubaini kwamba yote niliyoambiwa yalikuwa ni kweli. Ndugu na jamaa zako wengi waliamua kuficha siri zako nyingi ili kukulinda uolewe, kwani ulikuwa unawaaibisha kwa tabia zako.
Nilipokuja kukupa taarifa ulilia sana, ukisema kwamba, hayo ni majungu na kuwalaani hao walionipa taarifa hizo. Baada ya kukubana sana ulikubali kwamba, taarifa zile zilikuwa ni za kweli. Bila shaka unakumbuka nilivyokuwa nimechanganyikiwa. Kwanza kwa kudanganywa, na pili kwa kuhofia kwamba, huenda ulikuwa na virusi vya ukimwi.
Ni wazi unakumbuka kwamba, nilikutimua kwa uchungu siku ile ile. Niliamua baadaye kwenda kupima afya yangu ili kujua kama nilikuwa nimeukwaa. Kwa bahati nzuri nilikwenda kupima mara mbili na kuonekana sijaathirika.
Kupitia kwako nimejifunza jambo moja kubwa, sipaswi kuamini kauli za mpenzi bila kuchunguza kuhusu anachoniambia. Pia nimejua kwamba, siyo vyote vinavyong'aa ni dhahabu.
Lakini kwa upande wako, ni kwa nini usiwe mkweli kwa nafsi yako? Kwa nini uwe na moyo mgumu kiasi hicho kwa kujipenda kupindukia? Mimi nilikuhurumia kwa kukufukuza, kuna siku mwanaume mwingine atakata shingo yako, kutokana na utapeli wako wa kimapenzi…!
Copy to: Nivea, Lisa, Mrembo by Nature, King'asti, charminglady, Elizabeth Dominic, Asnam, Paloma, amu, MadameX, Madame B, gfsonwin, BADILI TABIA, vivian, Jeska, Mamndenyi, sweetlady, FirstLady, FirstLady1, Remmy, Mayasa, mwaJ, Swts, Smile