Kumbe uchawi ni kanuni na mahesabu

Kumbe uchawi ni kanuni na mahesabu

THEGENTLEMAN1996

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2017
Posts
518
Reaction score
593
Habari ndugu zangu,

Tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kufahamu chochote kuhusu uchawi, uganga na mizimu ipokuwa nilisoma thread za mshana jr na wengine tu. Sasa huku nilipo naishi kwenye chumba ambacho nimepanga kwa mama mmoja ambaye nilisikia habari zake kuwa ni mchawi sana.

Mama huyu ni daktari wa hospital fulani. Huyu mama anaishi na kijana mmoja ambaye ni mganga wa jadi kutoka Kigoma. Sasa huyu kijana mganga amekua rafiki yangu kiasi fulani hunipa story za kazi yake hiyo tulipiga story akaniambia "hiki kipaji kapewa na mungu"

Kiukweli jana tulitoka kwangu tukaingia kwake chumbani hapo sasa ndo nikakuta tunguri, sarafu, mizizi, mapembe, filimbi, karatasi nyeupe
nguo za rangi nyekundu, nyeupe, nyeusi nilkuta na vitu vingine vingi.

Sasa nikamtania hivi "hizi sarafu zote si uziue tu upate pesa gafla"
akasema hawezi ni vitendea kazi.

KANUNI & MAHESABU

Alitoa vitabu vyenye kufundisha na kuelekeza uchawi na nguvu za ajabu.
pia alinionesha karatasi zenye michoro ya majini, kafara na matambiko.
michoro ipo kama tunavochora katika masomo ya kawaida, kuna maandishi yako kwa lugha ya kiarabu maandishi hayo niliwahi kuyaona kwenye nyumba nyingine tena mkoa mwingine niliona karatasi ambazo zina kanuni ya mazindiko ya biashara, mapenzi n.k

Hivyo basi jana hayo nilishuhudia hayo kwa kifupi...!

NB: Uchawi upo ila siutumii wala kuutii naamini katika mbingu
 
Haya mambo yana uwanja mpana sana kama hauko huko ni vigumu kuyaelewa... Usiyaamini sana wala usiyapuuze sana baki na imani yako

Kidubuli
 
Habari ndugu zangu,

Tangu kuzaliwa kwangu sikuwahi kufahamu chochote kuhusu uchawi, uganga na mizimu ipokuwa nilisoma thread za mshana jr na wengine tu. Sasa huku nilipo naishi kwenye chumba ambacho nimepanga kwa mama mmoja ambaye nilisikia habari zake kuwa ni mchawi sana.

Mama huyu ni daktari wa hospital fulani. Huyu mama anaishi na kijana mmoja ambaye ni mganga wa jadi kutoka Kigoma. Sasa huyu kijana mganga amekua rafiki yangu kiasi fulani hunipa story za kazi yake hiyo tulipiga story akaniambia "hiki kipaji kapewa na mungu"

Kiukweli jana tulitoka kwangu tukaingia kwake chumbani hapo sasa ndo nikakuta tunguri, sarafu, mizizi, mapembe, filimbi, karatasi nyeupe
nguo za rangi nyekundu, nyeupe, nyeusi nilkuta na vitu vingine vingi.

Sasa nikamtania hivi "hizi sarafu zote si uziue tu upate pesa gafla"
akasema hawezi ni vitendea kazi.

KANUNI & MAHESABU

Alitoa vitabu vyenye kufundisha na kuelekeza uchawi na nguvu za ajabu.
pia alinionesha karatasi zenye michoro ya majini, kafara na matambiko.
michoro ipo kama tunavochora katika masomo ya kawaida, kuna maandishi yako kwa lugha ya kiarabu maandishi hayo niliwahi kuyaona kwenye nyumba nyingine tena mkoa mwingine niliona karatasi ambazo zina kanuni ya mazindiko ya biashara, mapenzi n.k

Hivyo basi jana hayo nilishuhudia hayo kwa kifupi...!

NB: Uchawi upo ila siutumii wala kuutii naamini katika mbingu
Hebu endelea kuandika, mbona hujamaliza?
 
Ianzishwe shule rasmi ya uchawi ili tusiojua tujue. Kama ni mahesabu tujue namna ya kukokotoa. Kweli upo wanaojua wanatumaliza kimyakimya na anaekumaliza ni rafiki yako pasipo kujua. Ee Muumba tuepushe na hili janga

Sent using Jamii Forums mobile app
Uchawi ni kitu kidogo mno haihitaji hata kusomea chini ya mnazi! Ni kaelimu kaduchu saaana ukijua utacheka sana na kufurahi mnnooo! Na utajiamini na kumheshimu Mungu mmmmnooo!!!
 
Inasemekana Kwa huu ukata ulivyo waganga wanapiga hela hatari..watu wameshindwa kupambana na hali zao wakiamini wamerogwa..matokeo yake waganga wanajenga shavu hatari Kwa majogoo ya uganga toka wateja walioshikiwa akili..
 
hivi huku jf, ni kweli kwamba hakuna mtu/mchawi hata moja anaeweza kujitolea kufundisha!!?
 
Back
Top Bottom