GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 390
- 395
Wana JF nimekaa na kutafakari sana kuhusu suala la mgao wa umeme ambalo mwisho wake hakuna ajuaye. Lakini mara zote tunawalaumu TANESCO kwa kuwa ndo tunaowaona wakikusanya vibil vyao kila kukicha. Angalia hii, tanesco ni shirika la ugavi wa umeme tz. Kumbe hawa jamaa hawazalishi umeme, kazi yao ni kugawa kwa watumiaji tu. Kwa hiyo ukiona umeme unakatika mara kwa mara, cha kwanza tumuulize mzalishaji, yeye akisema kuwa anazalisha then ndo tuwaulize tanesco kulikoni. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, nani anazalisha umeme? Tanesco walitakiwa wafanye kazi na Tanegco:- Tanzania electric generation corp, bahati mbaya tanegco haipo. Nasema tanesco hawazalishi umeme, isipokuwa tutawalaumu kwa ubovu wa mitambo yao. Nawasilisha.