Kumbe tatizo la umeme TANESCO tunawalaumu bure!

GAGL

JF-Expert Member
Aug 5, 2010
390
392
Wana JF nimekaa na kutafakari sana kuhusu suala la mgao wa umeme ambalo mwisho wake hakuna ajuaye. Lakini mara zote tunawalaumu TANESCO kwa kuwa ndo tunaowaona wakikusanya vibil vyao kila kukicha. Angalia hii, tanesco ni shirika la ugavi wa umeme tz. Kumbe hawa jamaa hawazalishi umeme, kazi yao ni kugawa kwa watumiaji tu. Kwa hiyo ukiona umeme unakatika mara kwa mara, cha kwanza tumuulize mzalishaji, yeye akisema kuwa anazalisha then ndo tuwaulize tanesco kulikoni. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, nani anazalisha umeme? Tanesco walitakiwa wafanye kazi na Tanegco:- Tanzania electric generation corp, bahati mbaya tanegco haipo. Nasema tanesco hawazalishi umeme, isipokuwa tutawalaumu kwa ubovu wa mitambo yao. Nawasilisha.
 
TUMOMBE MUNGU ALETE MVUA YA KUTOSHA HUKU TUKIACHA MAASI YETU ...then tuone kama kutakuwa na mgao...!
 
unamaanisha nini Mwalimu?

Huwezi kukaa tu Mungu akakupa maendeleo.

Kumuamini au kumuomba Mungu hakuna uhusiano wowote na maendeleo

Asians kama Wajapani na Wakorea hawaamini Mungu lakini wanamaendeleo, wazungu hali kadhalika

Ingelikuwa kumuomba Mungu kuna uhusiano wowote na maendeleo hawa wasingepata

Maendeleo yanakuja kwa juhudi, mipango, mikakati, uwajibikaji sio kuomba Mungu
 
Wana JF nimekaa na kutafakari sana kuhusu suala la mgao wa umeme ambalo mwisho wake hakuna ajuaye. Lakini mara zote tunawalaumu TANESCO kwa kuwa ndo tunaowaona wakikusanya vibil vyao kila kukicha. Angalia hii, tanesco ni shirika la ugavi wa umeme tz. Kumbe hawa jamaa hawazalishi umeme, kazi yao ni kugawa kwa watumiaji tu. Kwa hiyo ukiona umeme unakatika mara kwa mara, cha kwanza tumuulize mzalishaji, yeye akisema kuwa anazalisha then ndo tuwaulize tanesco kulikoni. Swali la kujiuliza hapa ni kwamba, nani anazalisha umeme? Tanesco walitakiwa wafanye kazi na Tanegco:- Tanzania electric generation corp, bahati mbaya tanegco haipo. Nasema tanesco hawazalishi umeme, isipokuwa tutawalaumu kwa ubovu wa mitambo yao. Nawasilisha.

hizo unazoongea ni system za nchi nyingine kabisa, kwa Tanzania Tanesco wanazalisha umeme na sasa ndio wananunu kidogo kwa wazalishaji wengine, SONGAS nk
 
Asians kama Wajapani na Wakorea hawaamini Mungu lakini wanamaendeleo, wazungu hali kadhalika

Hiyo kauli haijakaa sawa maana huko Nippon kuna ma Buddha na wa Shinto kibao. Na hizo ni dini. Sasa kama hawaamini mungu sijui watakuwa wanatafuta nini kwenye hizo dini
 
Ili kuleta ufanisi TANESCO inabidi ivunjwe mara mbili, iwepo TANESCO uzalishaji umeme na TANESCO usambazaji umeme. Kwa kufanya hivi hali ya uwajibikaji itaongezeka.
 
Hiyo kauli haijakaa sawa maana huko Nippon kuna ma Buddha na wa Shinto kibao. Na hizo ni dini. Sasa kama hawaamini mungu sijui watakuwa wanatafuta nini kwenye hizo dini

Kibao as in how many?

Kuwepo kwa madhabahu na mahekalu ya Buddha na Shinto hakumaanishi kuwa ndo Mungu anaabudiwa au hata kuaminiwa.

Jiulize Mjapani kwa mwaka mzima anamtaja au kumkumbuka Mungu mara ngapi?

Ukija katika hiyo dini yenyewe ya Budha, kuna sects ambazo haziamini uwepo wa Mungu hususan huyu Mungu mwenye nguvu za kufanya kila kitu na kutatua kila tatizo.

Dini ya Shinto vile vile haiamini Mungu, rather inaamini kuhusu nature na mambo ya spirits na vitu kama hivyo.

kwa hiyo hata kama Wajapani watakuwa wanafuata hizo dini ulotaja (which they dont), hawaamini Mungu kwa sababu basics za hizo dini si uwepo wa Mungu (at least not this The all knowing, The all powerful God)
 
Kibao as in how many?

Kwa mujibu wa Wiki, "The highest estimates for the number of Buddhists and Shintoists in Japan is 84–96%"

Kuwepo kwa madhabahu na mahekalu ya Buddha na Shinto hakumaanishi kuwa ndo Mungu anaabudiwa au hata kuaminiwa.
Ala! Kumbe hayo ni mapambo tu. Mweeee

Jiulize Mjapani kwa mwaka mzima anamtaja au kumkumbuka Mungu mara ngapi?
Funny! Kwani kumtaja mungu ndo kunamaanisha nini, kwamba wewe ndiyo mcha mungu sana?

Ukija katika hiyo dini yenyewe ya Budha, kuna sects ambazo haziamini uwepo wa Mungu hususan huyu Mungu mwenye nguvu za kufanya kila kitu na kutatua kila tatizo.
Yeyote yule wanayemwamini au chochote kile wanachokiamini, ndiyo mungu wao huyo. Au kwako mungu ni lazima awe huyo "mwenye nguvu za kufanya kila kitu na kutatua kila tatizo"?

Dini ya Shinto vile vile haiamini Mungu, rather inaamini kuhusu nature na mambo ya spirits na vitu kama hivyo.
Bado hoja ipo palepale kuwa hayo wanayoyaamini ndiyo mungu. Au kwako wewe mungu ni nani/nini?

kwa hiyo hata kama Wajapani watakuwa wanafuata hizo dini ulotaja (which they dont), hawaamini Mungu kwa sababu basics za hizo dini si uwepo wa Mungu (at least not this The all knowing, The all powerful God)
Wajapan hawafuati hizo dini?
 
Kwa mujibu wa Wiki, "The highest estimates for the number of Buddhists and Shintoists in Japan is 84–96%"

Hiyo ni ile inayoandikwa kwenye cheti cha kuzaliwa kama inavyoandikwa kabila lako tu. Haimaanishi kuwa wanaamini Mungu. Ni more of a culture than a religion

Ala! Kumbe hayo ni mapambo tu. Mweeee

Yap kwa sasa ni mapambo. Walikuwa wakiamini na kufata na kutekeleza enzi hizo. Sasa hakuna anaekwenda.

Funny! Kwani kumtaja mungu ndo kunamaanisha nini, kwamba wewe ndiyo mcha mungu sana?

Kutokumtaja kunaonyesha watu kuwa indifference na uwepo wake. Hawamtegemei kwa lolote. Maisha yao hayazunguki, wala kutambua uwepo wake. Na wakimtaja ni katika kupinga uwepo wake. Kuwa hawaamini kuwa kuna Mungu.

Yeyote yule wanayemwamini au chochote kile wanachokiamini, ndiyo mungu wao huyo. Au kwako mungu ni lazima awe huyo "mwenye nguvu za kufanya kila kitu na kutatua kila tatizo"?

Bado hoja ipo palepale kuwa hayo wanayoyaamini ndiyo mungu. Au kwako wewe mungu ni nani/nini?

Wajapan hafuati hizo dini?

Hawaamini kuwepo kwa Mungu, wanaamini kila kitu kilikuja wenyewe tu. Huko unakotaka kunipeleka wewe ni sawa na kusema atheist anaamini Mungu kwa sababu anaamini "kutokuwepo kwa Mungu"

Nimemzungumzia Mungu anaeweza kila kitu na kumtolea mfano kwa sababu ya chimbuko la hoja iliyokuwa ikijibiwa.

Kwa anaetaka tumuombe Mungu atuletee mvua ili tuepukane na mgao wa umeme. Anaeamini Buddha au Shinto hafanyi maombi ya aina hii kwa sababu haamini kama kuna Mungu achilia mbali Mungu anaeweza kila kitu.
 
Hiyo ni ile inayoandikwa kwenye cheti cha kuzaliwa kama inavyoandikwa kabila lako tu. Haimaanishi kuwa wanaamini Mungu. Ni more of a culture than a religion

Sijui wewe umezaliwa lini na wapi lakini mimi cheti changu cha kuzaliwa hakijaandikwa kabila langu!!

Hayo mengine tuyaache maana mada ishatekwa nyara....
 
Huh.......hakijaandikwa kabila la baba au mama?! basi changu kitakuwa feki, itabidi nikaombe kipya fasta :(
 
Huwezi kutaka maendeleo kwa kumtegemea Mungu. Hivyo vitu haviendi pamoja

Hakuna jinsi yoyote ile unaweza kufanya jambo bila kumtegemea YEYE. Awe mti, ng'ombe, sanamu maadamu waamini yupo na uhai na mafanikio yako yatoka kwake huna Budi kumtegemea.
 
Gaijn unachokosa kukielewa ni nini maana au ni nani au ni nini ni Mungu! Nyani Ngabu ameelezea kile ambacho mimi nakiamini. Nway turudi kunako mada ya msingi
 
Hakuna jinsi yoyote ile unaweza kufanya jambo bila kumtegemea YEYE. Awe mti, ng'ombe, sanamu maadamu waamini yupo na uhai na mafanikio yako yatoka kwake huna Budi kumtegemea.

Sawa na tukunje mikono tuombe mungu atuletee maendeleo, kwa kuanzia atuondolee tatizo la mgao wa umeme
 
Mkuu hili la kukunja mikono, kuchora nne na kulala usingizi wa pono pasipo kufanya kazi silo tunalomaanisha
 
Hata mana iliposhushuwa kutoka mbinguni ilibidi watu waiandae/waipike ndio waile - hata kama unamuamini na kumuomba Mungu inabidi ujipange na ujitume ili maendeleo yaje, kwa mfano, tunaweza kuwa na mikakati endelevu ya kuvuna mvua na kutumia hayo maji kuleta nishati ya umeme ila kwa sasa hata mgawo hauna mpangilio!
 
Tungekuwa tunaweza tungekuwa tumeshafanya....
 
Back
Top Bottom