Kumbe Tanganyika bado ipo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kumbe Tanganyika bado ipo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Cynic, Dec 6, 2009.

 1. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Wiki chache zilizopita nilitakiwa nitoe taarifa wazazi wangu walizaliwa lini na wapi. Nikataja mwaka na kwamba walizaliwa Tanzania. Jamaa akaniuliza nina uhakika mara tatu na mimi kwa kujiamini nikamwambia ndiyo. Baada ya muda akaniambia haiwezekani! Nikamwambia labda kwenye database yake itakuwa imeandikwa United Republik of Tanzania,
  Akaniambia pia haiwezekani. Ndipo akaniuliza nchi yenu haijawahi kubadili jina? Ndipo akili zikanijia na kumwambia kwamba ilikuwa inaitwa Tanganyika. Ndipo system yake ikakubali, na copy ya printout kuonyesha walizaliwa Tanganyika.

  Nilichojifunza hapa ni kwamba kumbe Tanganyika ipo na kumbe wengine bado wanaitambua. Na waTZ mliozaliwa kabla ya muungano msijisahau - hamkuzaliwa Tanzania
   
 2. Spear

  Spear JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 21, 2008
  Messages: 510
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  kwa tarifa yako Tanganyika ipo na itaendelea kuwepo,na kwa wale wasioipenda Tanganyika Mungu awataremshie lana katika maisha yao.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2009
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Hili jina Tanganyika hata mie huwa napata shida kuelewa ni wakati gani linakuwepo na wakati gani Tanganyika haipo.
  Ukiangalia kwa mfano Chama cha wanasheria huitwa Tanganyika Law Society na siyo Tanzania.Hebu tuchanganue ni wapi Tanganyika ina apply..na ni wapi haipo.Kulikwa pia na Tanganyika Packers japo imekufa miaka ya mwanzo ya 80.
   
 4. a

  alibaba Senior Member

  #4
  Dec 6, 2009
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 185
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Cynic,
  Ni kweli TANGANYIKA ilikuwepo, ipo na itaendelea kuwepo na Muda si mrefu toka sasa Jinamizi lake liotaibuka kudai nafasi yake. Narudia Muda si mrefu toka sasa.................
   
 5. T

  T_Tonga Member

  #5
  Dec 6, 2009
  Joined: Jul 24, 2007
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  duh nitafurahi ikiwa itarudi tunamuomba mungu irudi kama leo na kesho na sio kufichwa inajulikana kuwa tanganyika ipo na serekali yake ipo sasa hii ni kuonyesha kuwa mnawakandamiza wazenji tu
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ngoja nikuongezee na nyingine:
  1. Medical Council of Tanganyika ( sijui madaktari wa Zanzibar kama wana yakwao tofauti na hii au hii ndio yenye kushughulikia kote)

  2. Tanganyika Farmers' Association
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Naona Wakuu mnajidanganya wote nyinyi jina la (Tanganyika) litabaki lakini halitatumika kama mnavyotaka nyinyi lakini suala la Muungano upo bado pale pale na hiyo Tanganyika imekufa kama zamani alivyo kufa Baba Wa Taifa Mwalim Nyerere na Mzee Abeid amani Karume ikiwa hao watafufuka na hiyo Tanganyika itafufuka na Unguja pia itafufuka lakini kama hawatafufuka mpaka siku ya hukumu yaani kiama basi hiyo Tanganyika na Unguja hayo majina hayatarudi kama zamani hizo ndio ndoto za Sakafuni.......................Asanteni sana


  WANAOTAKA KUUVUNJA MUUNGANO BASI HAO NDIO NI MAFISADI.
   
 8. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2009
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa tarifa yako wazanzibari sio mwehu wa kukana majina ya Unguja na pemba (zanzibar)sioni Ubaya wa jina Tanganyika kwanini linawaudhi watu kutamkwa, nawaombea wale wenye uchungu na Tanganyika siku moja Mmungu awape nguvu za kulimarisha jina asili la Tanganyika.
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  We bwana mkubwa vipi? Kutaja neno Tanganyika ni ufisadi kwa vipi? Na hayo ya kuvunja muungano ni yako .. sijui yanakujaje hapa! Nadhani unafahamu fika kwamba December 9 huwa tunafunga ma osifi na tunasherehekea uhuru wa Tanganyika kwa magwaride rasmi ya majeshi ya ulinzi na usalama na viongozi wote wa kitaifa huwa wanaudhuria.
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Tanganyika ipo, kuna ziwa, kuna wilaya huko DRC.

  Ila nchi iliuawa katika muungano na Zanzibar katika mazingira ya kutatanisha na hesabu mpya za federation ambazo hazijawahi kuonekana tena dunia nzima.
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Tanganyika will prevail forever!
  Time talks,...and in no tym, we gonna see our beautiful Tanganyika!
   
 12. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #12
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  SWALI: Hivi timu ya taifa ya Zanzibar inapocheza mpira dhidi ya timu ya taifa ya bara kwenye Challenge inakuwa ni Zanzibar dhini ya Tanzania au Tanganyika? Mimi nadhani ni Zanzibar dhidi ya Tanganyika ila hawataki hilo jina litamkwe. Lakini nchi ipo.
   
 13. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #13
  Dec 7, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  mkisikika na wenye nchi mnasema Tanganyika mtakiona........

  Moja ya laana inayowapata Wadanganyika ni kukataa asli yao na kulikana jina la nchi yao ya asli.

  Poleni sana
   
 14. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #14
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Je wewe unayesema Tanganyika Itarudi umezaliwa lini? Nafikiri wewe ni Enzi ya Ruksa ndo maana hujui usemalo.........Asante
   
 15. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #15
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  tanganyika is the invisible power,
  ilikuwepo,ipo, na itaendelea kuwepo hata kama haionekani,
   
 16. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #16
  Dec 7, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Naona tumekosa mambo ya kujadili! Kama kuna mtu atajisikia kuita Tanganyika au Tanzania Bara sioni kama kuna ubaya wowote, isipokuwa ijulikane nia yake ni nini! Dhambi ya ubaguzi itaendelea kuwatafuna, na mnastahili iwatafune vilivyo! Mkishamaliza kusema SISI WATANGANYIKA na kujitenga mtakuta hakuna mtu anayeitwa MTANGANYIKA! Kutakuwa na SISI WANYAMWEZI, WAO WASUKUMA! SISI WAPEMBA, WAO WAUNGUJA,.........Historia ndivyo ilivyo!
   
Loading...