Kumbe Rwanda Bureeeeee!

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,538
9,197
Nimekuwa nikisia makelele meengi kuhusu hii nchi ya Rwanda kwamba ndio mfano wa kuigwa na blah blah nyingi, nikataka niijue zaidi, kumbe hamna chochote hii nchi ina watu zaidi ya
Milioni 10 na uwezo wao wa kuzalisha Umeme ni Megawatt 80 MW tu!!!! nimepigwa na Butwaaa sasa hizo kelele zote za Bw.Kagame hivi Kagame vile ni za nini?
Maendeleao gani hayo yanayoongelewa huko Rwanda kama watu milioni 10 hawawezi kutumia MW 80 za umeme?
Au labda tafsiri ya maendelo imebadilika? au kufagia barabara hapo Kigali ndio maendeleo, hakika hawa jamaa wanasifiwa bureeee tumewaacha mbali saaana, duh Megawati 80 watu milioni zaidi ya milioni 10!
 
kwa umeme sawa, vipi kwa kigezo cha GDP?

Kama umeme tu hawana hayo mengine wala hatuwezi kuanza kuyaongelea umeme ndio Mpango mzima ndio kila kitu, hakuna umeme hakuna maendeleo ni rahisi kihivyo tu!
 
Mkuu ungetofautisha kuzalisha na kutumia inawezekana wanazalisha hzo lakini wakawa wananunua umeme kutoka nje ya nchi mfano Sumbawanga wanatumia umeme kutoka Zambia nadhan kuna mikoa mingine wanatumia umeme kutoka Uganda, Zanzibar wanatumia umeme kutoka bara na wanaulipia kwahyo kipimo kizuri ingekuwa ni asilimia ngapi wa ya wananchi wa Rwanda wanatumia umeme,ila kuzalisha sio kigezo cha maendeleo hata Ulaya wanasafirisha umeme kati ya nchi na nchi.
 
Huyu mtu hajasoma uchumi, mwache! Kama RwF 630 = 1USD, na Tsh 1660= 1USD halafu mtu anasema ni bureeeee!! Hamna kitu hapo usitoke povu utajichosha bure tu!! Ukizungumzia GDP ndio unamvuruga kabisaaa!!
 
compare resources zao na zetu na matatizo waliyopitia ikiwemo genocide ya 20 years ago, halafu angalia na sisi uone nani mabwege
 
yaani hiyo MW 80 ndio matumizi ya Umeme ya Rwanda kwa watu zaidi ya milioni 10, maanake changanya kila kitu, kila Nyumba ikiwasha taa, kila kiwanda kikizalisha kwa kiwango cha juu, watu wote wakiwa kazini mchana na viyoyozi na kila kitu, wachomea welding wakifanya kazi, mafundi gereji wakiwa kazini n.k ndio wanagonga hapo kwenye MW 80, yaani siku MM steel yetu akitaka kuhamishia kiwanda chake Rwanda nchi nzima itazima kwa kukosa Umeme, yaani huo ni umeme labda wa Wazo Cement na MM steel tu!
 
Alah kumbe unatumia kigezo cha rate ya fedha kupima kiwango cha Kuichumi halafu unajisifia umesoma uchumi, na hapa Je,Dola 1 moja ya US = zaidi ya yeni 130 za Kijapani, Dola 1 Us = 120 shilingi ya Kenya, Japani ndio Nchi ya Pili kwa ukubwa wa Uchumi Duniani, sasa uwiano wako uko wapi, kama unatumia kigezo hicho? au Namibian Dola ina thamani kuliko kubwa kuliko yeni ya Japani hapo Je?, yaani ukiwa na Hela ya Namibia Dola na ukachenji kwa Yeni ya Japani unapate hela nyingi zaidi kuliko kinyume chake hapo Je, Mchumi wetu unasemaje?
 
Kwani mahitaji yao ni Mw ngapi? Tungejua kwamba kwa uzalishaji huo je kuna upungufu kiasi gani ktk nchi kwa sababu navyojua Rwanda ni nchi ndogo
 
Angalia Comment # 7 halafu rudi tujadiriane tena,
Kama umeme tu hawana hayo mengine wala hatuwezi kuanza kuyaongelea umeme ndio Mpango mzima ndio kila kitu, hakuna umeme hakuna maendeleo ni rahisi kihivyo tu!
 
Kwani mahitaji yao ni Mw ngapi? Tungejua kwamba kwa uzalishaji huo je kuna upungufu kiasi gani ktk nchi kwa sababu navyojua Rwanda ni nchi ndogo

Mahitaji yao nimeshakwambia hawagoti MW 80, na unaposema Rwanda ni ndogo ujue unaongelea kieneo lkn sio kwa idadi ya watu, ujue wana km za mraba 20,000 yaani serengeti yetu ni kubwa zaidi na wana watu Zaidi ya milioni kumi 10, na sisi tu km za Mraba karibu milioni moja tuna watu milioni 40! sasa watu milioni 10 kwa kutumia MW 80 kwa kiwango chochote kile ni ndogo sana! Wazo Cement hawawezi kuwekeza Rwanda leo hii kwa maana hamna Umeme!
 
Alah kumbe unatumia kigezo cha rate ya fedha kupima kiwango cha Kuichumi halafu unajisifia umesoma uchumi, na hapa Je,Dola 1 moja ya US = zaidi ya yeni 130 za Kijapani, Dola 1 Us = 120 shilingi ya Kenya, Japani ndio Nchi ya Pili kwa ukubwa wa Uchumi Duniani, sasa uwiano wako uko wapi, kama unatumia kigezo hicho? au Namibian Dola ina thamani kuliko kubwa kuliko yeni ya Japani hapo Je?, yaani ukiwa na Hela ya Namibia Dola na ukachenji kwa Yeni ya Japani unapate hela nyingi zaidi kuliko kinyume chake hapo Je, Mchumi wetu unasemaje?
Hiyo ni hesabu rahisi kujua nani anafanya vizuri, japan wame devalue pesa yao waweze kufanya biashara na Africa that's all! Lakini huwezi kuilinganisha Rwanda nchi iliyopitia GENOCIDE ikasambaratika kwa maana ya kusambaratika, leo walipofikia hapo uzungumzie 80 MEGAWATI kwamba hawako vizuri kiuchumi!! Daktari wa Rwanda analipwa karibu Tsh 3,000,000/- ya Tanzania nyie wa kwenu mnamlipa ngapi? Walijifunza Tanzania mambo ya Health Insurance, leo wako zaidi ya 90% coverage wakati bongo hata 20% hamjafika!! Tanzania tuna all resources ila tatizo hatuna viongozi bali tuna watawala!! Na kama umegundua kila kitu kitu kinachoanzishwa Tanzania kina collapse sijui kama umewahi kujiuliza hilo swali..!! Ndio maana kila mtu akipata upenyo anaiba!! IKULU inaiba, mwananchi wa kawaida anaiba! That is Tanzania, that is bongoland!!
 
compare resources zao na zetu na matatizo waliyopitia ikiwemo genocide ya 20 years ago, halafu angalia na sisi uone nani mabwege

Kama swala tu nani ni Ubwege, basi naweza kusema wao ndio mabwege kwa maana wameuana wao kwa wao lkn sisi hatujauana hivyo sisi ni wajanja!
Suala la rasilimali hata wao wanazo nyingi tu sana nchini mwao, Rwanda ni kijani tupu, Udongo wenye rutuba mwanzo mwisho, maji ya kutosha kzalisha umeme na zaidi, hivyo sio kisingizio!
 
Back
Top Bottom