Jana katika kikao cha Bunge kulikuwa na mtifuano kuwa ni nani anyeidhinisha malipo ya Serikali.
Waziri wa Fedha akajibu jibu ambalo halikumridhisha Mhe. Sendeka na Mhe. Spika akaongezea ufafanuzi kwenye majibu ya Waziri wa Fedha.
Kama ni kweli Mhe. Rais ndo anaidhinisha malipo ya Serikali basi hakuna haja ya kutumia rasilmali fedha ya Serikali kutayarisha bajeti toka ngazi za chini mpaka Bunge. Kama hilo ni kweli hakuna haja ya kuwa na vikao vya Bunge takriban mwezi mmoja na nusu.
Mimi ninavyofahamu bajeti ikiishapitishwa na Bunge kila kifungu kilichopitishwa na Bunge lazima kipate fedha iliyoidhinishwa. Pili haitakiwi kufanya matumizi nje ya bajeti iliyopitishwa na Bunge na kama kuna jambo la dharura basi jambo hilo hupelekwa tena Bungeni.
Hili la Rais kupitisha malipo ya Serikali ni jambo geni kwangu.