Nyerere alikua na malengo mazuri sana kuwafanya watu wote/vijana wote wapitie JKT lakini baadaye ilikuja kushindikana kwa sababu za kiuendeshaji, ingawa sasa naona hali imeanza kurudi taratibu.
Mkuu, siyo magereza tu, askari yeyote wa jeshi lolote, liwe la police, magereza, uhamiaji, JWTZ, humpigia salute askari aliyejuu yake ktk maana ya Rank za kijeshi.
Kwa maana hiyo, hata wa JWTZ humpigia salute askari wa jeshi lingine lolote liwe police, magereza nk, kinacho matter ni kuzidiana RANKS za kijeshi.