hip hop uchwara
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 6,670
- 4,370
Aisee
NaaamGazetted officer ni ofisa wa ngazi ya juu wa serikali ambaye uteuzi wake lazima utangazwe katika gazeti la serikali. Hakuna maofisa wa aina hiyo katika jeshi lolote Tanzania. Katika majeshi yote kuna NCOs na COs.
Commissioned officer ni ofisa ambaye ameingizwa katika utumishi wa kudumu katika jeshi au serikalini. Ndomana namba hubadilika na kuanza kutumia namba nyingine P na hii ni kwa majeshi yote NCOs hutumia namba tofauti na COs baada ya kupata nyota ya kwanza.
Tafsiri nyingine au Kwanini Rais anakuwepo katika kutoa kamisheni za JWTZ? ni procedure tuliyojiwekea kama Taifa na dhana kubwa hapa ni Rais kuhusishwa na majukumu ya ulinzi wa Nchi. Yaani Rais anawapa jukumu la ulinzi wa Nchi moja kwa moja ndomana anatakiwa kuwepo. Kwasababu hilo ndo jukumu namba moja la JWTZ.
Kwahiyo kitendo cha Rais kuwepo haimaanishi ndo wamekuwa COs na asipokuwepo sio COs, hapana. Maofisa wote wa majeshi yetu ni COs as long as ni jeshi kamili kwa mujibu wa katiba. Ndio maana Rais ni amiri jeshi mkuu wa majeshi yote, ndio maana wote hula kiapo cha utii kwa Rais wakati wanapoapishwa.
Nikueleweshe kidogo kuhusu vyeo, JWTZ hutumia vyeo vya kimataifa majeshi mengine hutumia vyeo aidha vya kijumuia, kikanda, au locally lakini vyeo hivi huwa ni equivalent inayotambulika nchini au katika kanda husika. Hivyo kwetu hapa vyeo hivi vina equivalent yake hata kama majina yanapishana. Ukitaka kujua anza kuvihesabu anzia na Private wa JWTZ, Constable wa Polisi, au Warder wa Magereza etc mpaka ukife cheo cha mwisho kwa Generali, IGP au CGP utagundua ngazi zinaendana. Kwa ufupi ni kwamba ni sawa na Advanced Diploma na Bachelor degree, yaani kwetu Advanced Diploma yetu tunaitambua ni sawa na degree lakini ikienda nchi nyingine haitambuliki. Lakini degree inatambulika duniani kote.
Hivyo kwa sheria zetu Luteni usu wa JWTZ ni sawa na Assistant Inspector wa Polisi, Magereza na wa Zimamoto, isipokuwa wa JWTZ ni mkubwa(senior) akifuatiwa na wa Polisi, Magereza etc. Kwahiyo Inspector yaani nyota mbili wa Polisi ni mkubwa kuliko nyota moja wa JWTZ isipokuwa nyota mbili wa Polisi atakuwa ni mdogo kwa nyota mbili wa JWTZ.
Sijui kama utakuwa umenielewa