JWTZ kuimarisha ushirikiano na Vyuo vya Sayansi

JWTZ kuimarisha ushirikiano na Vyuo vya Sayansi

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,143
Reaction score
889
👉 Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, alisema kuwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) litaendelea kushirikiana na Vyuo Vikuu vya Tanzania ili kuongeza tija na ufanisi, hasa katika nyanja za sayansi na teknolojia.

👉 Jenerali Mkunda alisema hayo alipofanya ziara katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST), iliyopo jijini Arusha, tarehe 11 Septemba 2026.

👉 Katika ziara hiyo, Jenerali Mkunda aliridhishwa na namna taasisi hiyo ilivyokuwa ikitekeleza majukumu yake, hususan katika matumizi ya sayansi, teknolojia na ubunifu.

👉 Jenerali Mkunda alipata fursa ya kufahamu shughuli mbalimbali zilizokuwa zikifanywa na taasisi hiyo, ikiwemo tafiti na ubunifu uliokuwa ukilenga kutatua changamoto mbalimbali za maendeleo.

👉 Ziara hiyo ilikuwa mwaliko kutoka kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho, Profesa Maulilio Kipanyula, kwa lengo la Jenerali Mkunda kujionea shughuli zilizokuwa zikifanywa na taasisi hiyo pamoja na fursa za ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.

👉 Naye Makamu Mkuu wa Chuo, Profesa Maulilio Kipanyula, alimshukuru Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, kwa kukubali mwaliko huo, akisema ziara hiyo ilikuwa imeimarisha uhusiano kati ya taasisi hiyo na JWTZ.

👉 Profesa Kipanyula aliahidi kuwa NM-AIST ingeendelea kutoa ushirikiano katika maeneo mbalimbali, hasa katika utafiti, teknolojia na ubunifu
HScFOaWWwAA8saZ.jpg
HScFPxfX0AAfkmc.jpg
HScFR-LXAAATfVC.jpg
HScFR-LXAAATfVC.jpg
 
Back
Top Bottom