Kumbe kuna jeneza Self na hamsemi!

Kumbe kuna jeneza Self na hamsemi!

Naamini tuko pamoja na tunaendelea kupambana.

Ukistaajabu ya musa utaona ya filauni.

Wiki hii jumatatu nilikuwa nasafiri kwenda eneo fulani, Siti niliyokaa nilikuwa nimekaa na kaka mmoja hivi age 23 hadi 30yrs

Kutokana na maongezi yake kwenye simu ilionesha wazi anakwenda msibani na muda huo alikuwa anaongea na MUUZA MAJENEZA KWA SIMU.

Kitu kilichonishangaza ni majeneza aliyokuwa anaulizia na muuzaji akimjibu kutokana na bei na hadhi ya jeneza.

Kitu kilichonishangaza ni KUULIZA JENEZA AMBALO NI SELFCONTAINER NA MUUZAJI KWELI AKAMWAMBIA BEI YAKE NAYE PIA AKAWAPA MREJESHO WAFIWA.

Baadhi ya majeneza yaliyoulizwa na kupewa bei ilikuwa

1. Jeneza la kawaida la kufungua.

2. Jeneza lenye switch

3. Jeneza ambalo ni Self
Na yote aliambiwa yapo na bei zake pia.

Pia hivi karibuni nilisikia RC CHALAMILA akiongea clip moja kuwa tupunguze mbwembwe kwa marehemu NA AKISEMA JENEZA MPAKA UNAWEZA PASSWORD

Nikabakia na maswali hili jeneza Self kumbe marehemu tunachimba dawa na kukata gogo humo humo.

ISHI UONE MENGI.

Wajuzi wa mambo haya karibuni.
Hahaha hawataki marehemu atoroke kaburi
 
Na hii unakuta ni kikundi kabisa na hiyo ndo kazi inayowaweka mjini.

Huwa kuna saa najisemea vya kushangaza haviwezi kuisha ndani ya hii dunia. Yaani unaeza ona hiki ukashangaa baadae unakutana na kingine kinakushangaza zaidi.
yani kama ni pesa basi inatafutwa kwakweli,dah,,!
 
Mimi hata wakinitupa porini ntakuwa nipo zangu another realm navuta zangu tu ndumu.
 
Kama kuna siku itatokea nikaachana na Ugalatia ni kwa sababu kuu zifuatazo:

1. Zile raha ambazo Sheikh Kipozeo huwa anazifafanua kuwa zipo zinasubiri kule akhera.

2. Simplicity ya mambo likiwemo la mazishi. Unakata moto leo unazikwa leo hii hii bila mbwembwe wala nini...ni Sanda na mkeka tu kwisha. Safi sana hii!

3. Ishu ya ndoa...rahisiiiii!

Misiba ya Kigalatia siku hizi imegeuka ni sehemu ya show off na kama wewe ni masikini watu wala hawaji au utazikwa haraka haraka na kwa dharau. Watu wanalipa pesa mpaka kwa viongozi wa serikali ili waweze kuhudhuria ili eti kuupa uzito msiba. Utafikiri haya yanasaidia lo lote kwa marehemu. Kumbe hata ungezikwa na dunia nzima kama alivyozikwa Mandela au Papa Paulo wa Pili ni kazi bure!
Namkubal sana kwa kitendo cha kuwa muwazi kuhusu mizigo licha ya statas yake ya Usheikh
 
Namkubal sana kwa kitendo cha kuwa muwazi kuhusu mizigo licha ya statas yake ya Usheikh
Mizigo sheikh!

Screenshot_20230624_212148_Instagram Lite.jpg
 
Back
Top Bottom