Zogwale
JF-Expert Member
- Jul 10, 2008
- 15,287
- 10,842
Akiwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, JK aliwahi kuzidiwa ghafla uwanja wa ndege wa Brussels nchini Ubelgiji akiwa njiani kuelekea nchini Cuba, hali iliyosababisha alazwe kwa saa kadhaa kabla ya kuruhusiwa kuendelea na safari.
Source: Tanzania Daima: 25th August 2010.
My take:
Kama habari hii ni ya kweli, Ni vema wanaoangalia afya ya Rais wakatafuta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo hili, la sivyo litazidi kujirudia.
Kuna habari pia JK ana maumivu kidogo ya shingoni ambayo huenda aliyapata akiwa kijana kutokana na tukio kwenye Michezo au Mafunzo ya Kijeshi (Mwanahalisi; 25-31 August 2010). Ni vema wahusika waweke bayana pia ili wananchi wake wajue.
Kwa hiyo ana kifafa cha msimu au ni nini? Pole presidaaaa!!