Kishaju
Senior Member
- Feb 23, 2008
- 106
- 62
Ndugu zangu, kulingana na HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA TAKURU, MBEYA, 20 FEBRUARI, 2006 ilikuwa inawapa mwanya TAKUKURU kuuchunguza mkataba wa Richmond kwa undani si mazingira ya Rushwa tu....yaani hata mchakato mzima...ebu angalieni hapa chini sehemu ya hiyo hotuba na tumuulize Hosea je anapingana na kauli ya mkubwa wake aliyemsimika kazini....
"....Naomba nitaje maeneo kadhaa ambayo nadhani itakuwa busara kuyatilia mkazo katika mipango yenu.
Tayari nimetaja rushwa katika mikataba. Kadhalika nimeshaelezea, Bungeni, nia yangu ya kutaka kuangalia upya taratibu za kuingia mikataba zinazotumiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kubaini mianya ya rushwa na kuongeza uwazi na uwajibikaji ili kulinda maslahi ya umma. Naomba TAKURU isaidie katika zoezi hili na kuishauri Serikali juu ya mapungufu yaliyopo katika taratibu zilizopo sasa ili yarekebishwe.
Katika zoezi hili, msisahau kuangalia pia michakato ya majadiliano, viwango vya utekelezaji, muda wa utekelezaji, kuhusika au vinginevyo kwa mamlaka za udhibiti wa utekelezaji (regulatory agencies) na hatua sahihi za kuchukua endapo masharti ya mikataba yatavunjwa.
Ni jukumu lenu TAKURU kutumia ujuzi wenu kubaini mapema mikataba batili au ile isiyokuwa na manufaa kwa taifa na kuishauri serikali ili ichukue hatua zinazostahili kabla fedha na mali havijapotea. Kinga ni bora kuliko tiba.
Eneo la pili lenye tuhuma ya kuwa na mianya ya rushwa kubwa kubwa ni la manunuzi/ununuzi (procurement/purchases) Serikalini. Sina budi kukiri kuwa Sheria ya Manunuzi na taratibu nzuri na rahisi za ununuzi zilizowekwa zimesaidia sana kupunguza ukubwa wa kipenyo cha mwanya wa rushwa katika eneo hili. Hata hivyo bado kuna maneno yahusuyo upendeleo, mgawanyo usio sawa, kutokuwepo uwazi wa kutosha wala ushindani halisi kwa kuwa washindani wengine hupewa habari za viwango vya gharama mapema. Kadhalika kuna madai kuwa ununuzi hauzingatii gharama na ubora wa bidhaa. Kwa ajili hiyo yapo madai kuwa wakati mwingine bidhaa zinapewa gharama za juu zaidi na kama gharama ni za kawaida basi baadhi ya bidhaa hazifikishwi kwa mnunuzi kwa maelewano baina ya wanunuzi na wauzaji. Fedha nyingi za serikali hupotea kupitia mwanya huu wa rushwa. Fuatilieni taratibu za manunuzi na ununuzi serikalini kubaini na kuziba mianya ya rushwa katika eneo hili nalo. Nia yangu ni kutaka kuona pesa kidogo tulizo nazo zinatumika kwa manufaa ya umma na watu walio wengi na siyo kuendeleza maslahi binafsi ya watu wachache"
Sasa Hosea kwa nini asiachie ngazi jamani....