Kumbe Hosea wa TAKUKURU anapingana na Rais JK

Kishaju

Senior Member
Feb 23, 2008
106
62
Ndugu zangu, kulingana na HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA TAKURU, MBEYA, 20 FEBRUARI, 2006 ilikuwa inawapa mwanya TAKUKURU kuuchunguza mkataba wa Richmond kwa undani si mazingira ya Rushwa tu....yaani hata mchakato mzima...ebu angalieni hapa chini sehemu ya hiyo hotuba na tumuulize Hosea je anapingana na kauli ya mkubwa wake aliyemsimika kazini....

"....Naomba nitaje maeneo kadhaa ambayo nadhani itakuwa busara kuyatilia mkazo katika mipango yenu.

Tayari nimetaja rushwa katika mikataba. Kadhalika nimeshaelezea, Bungeni, nia yangu ya kutaka kuangalia upya taratibu za kuingia mikataba zinazotumiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kubaini mianya ya rushwa na kuongeza uwazi na uwajibikaji ili kulinda maslahi ya umma. Naomba TAKURU isaidie katika zoezi hili na kuishauri Serikali juu ya mapungufu yaliyopo katika taratibu zilizopo sasa ili yarekebishwe.

Katika zoezi hili, msisahau kuangalia pia michakato ya majadiliano, viwango vya utekelezaji, muda wa utekelezaji, kuhusika au vinginevyo kwa mamlaka za udhibiti wa utekelezaji (regulatory agencies) na hatua sahihi za kuchukua endapo masharti ya mikataba yatavunjwa.

Ni jukumu lenu TAKURU kutumia ujuzi wenu kubaini mapema mikataba batili au ile isiyokuwa na manufaa kwa taifa na kuishauri serikali ili ichukue hatua zinazostahili kabla fedha na mali havijapotea. Kinga ni bora kuliko tiba.

Eneo la pili lenye tuhuma ya kuwa na mianya ya rushwa kubwa kubwa ni la manunuzi/ununuzi (procurement/purchases) Serikalini. Sina budi kukiri kuwa Sheria ya Manunuzi na taratibu nzuri na rahisi za ununuzi zilizowekwa zimesaidia sana kupunguza ukubwa wa kipenyo cha mwanya wa rushwa katika eneo hili. Hata hivyo bado kuna maneno yahusuyo upendeleo, mgawanyo usio sawa, kutokuwepo uwazi wa kutosha wala ushindani halisi kwa kuwa washindani wengine hupewa habari za viwango vya gharama mapema. Kadhalika kuna madai kuwa ununuzi hauzingatii gharama na ubora wa bidhaa. Kwa ajili hiyo yapo madai kuwa wakati mwingine bidhaa zinapewa gharama za juu zaidi na kama gharama ni za kawaida basi baadhi ya bidhaa hazifikishwi kwa mnunuzi kwa maelewano baina ya wanunuzi na wauzaji. Fedha nyingi za serikali hupotea kupitia mwanya huu wa rushwa. Fuatilieni taratibu za manunuzi na ununuzi serikalini kubaini na kuziba mianya ya rushwa katika eneo hili nalo. Nia yangu ni kutaka kuona pesa kidogo tulizo nazo zinatumika kwa manufaa ya umma na watu walio wengi na siyo kuendeleza maslahi binafsi ya watu wachache"

Sasa Hosea kwa nini asiachie ngazi jamani....
 
Kishaju kula tano mwanangu,

Hii speech anatakiwa kupewa Hosea, halafu aulizwe kuhusu kauli yake juu ya mikataba.

I don't care if this is internal bickering or not (as has proved to be the case recently).The entire TAKUKURU needs to be reformed.We do not have any faith in not only Hosea, but also the entire top echelon of TAKUKURU.
 
Ndo hivyo...sasa ni vizuri wawe wanakumbuka wanayoyasema....kwa hiyo TAKUKURU ina nafasi kubwa ya kuzuia UFISADI kama ikifanya kazi inavyotakiwa....
 
Ndo hivyo...sasa ni vizuri wawe wanakumbuka wanayoyasema....kwa hiyo TAKUKURU ina nafasi kubwa ya kuzuia UFISADI kama ikifanya kazi inavyotakiwa....

Kweli kabisa nadhani na hosea alitaka marekebisho ya sheria, na yakapita bungeni, au sio?
 
Ndo hivyo...sasa ni vizuri wawe wanakumbuka wanayoyasema....kwa hiyo TAKUKURU ina nafasi kubwa ya kuzuia UFISADI kama ikifanya kazi inavyotakiwa....

Nadhani sentensi yako ingekuwa na raha zaidi ingesema: sasa ni vizuri wawe wanakumbuka wanayoambiwa na JK (Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Tanzania)...
 
I have a strong feeling he is going within or before the next bunge session.

Ikichukuliwa kuwa TAKUKURU ilipaswa kuwa mstari wa mbele kuainisha mianya ya rushwa lakini haikutoa hata dalili ya kuwa kuna uozo ktk mkataba wa Richmond. Hii ni sawa na kumuabisha Mkuu wa nchi na wananchi kwa ujumla. Kama Hosea angekuwa anasoma alama za nyakati angeomba kujiuzulu maana Pinda amesema kuwa maazimio ya Bunge yamepokelewa na yatatekelezwa.
Au asubiri kuona uteuzi mpya wa mkurugenzi wa Takukuru.
 
Si unajuwa hapa kwetu ustaarabu wa kuwajibika hatuna na ikitokea inakuwa ni very rare case kama mzee ruksa na wengine wachache sana, la sivyo mpaka ulazimishwe.
 
Naomba mwenye majibu mazuri ya swali hili;

Kwanini Hosea mpaka leo haja jiuzulu ndugu zangu?
 
Naomba mwenye majibu mazuri ya swali hili;

Kwanini Hosea mpaka leo haja jiuzulu ndugu zangu?

Nikisema ni kiburi cha madaraka sidhani nitakuwa nimekosea.
Pia ni ile kuona Muungwana kakaa kimya anadhani bado anahitajika sana ila hajui kuwa Kobe akiinama........
 
Hivi mwadhani kina lowasa, karamagi na bangushiro walijiuzulu kwa hiari au wamefukuzwa? Hosea akijiuzulu kwa hiari nanyoa ndevu!!! Kinachotakiwa ni JK kumtimua!!! Vinginevyo ni danganya toto!!!!
 
Msishangae akiulizwa huyo Hosea kuhusu hii hotuba huenda akajibu "siikumbuki!" Na labda hayo maswali ataulizwa akiwa balozi wa Tanzania huko wapisijui, na atakuwa amepewa wito wa kuja kuyajibu wiki mbili kabla lakini atasema ameshtukizwa, hii inaitwa "Lumbanga style"!
 
Kwa maelezo ya hosea aliyoyatoa juzijuzi ni kama vile kwake rushwa ni bribe na ndio maana anasahau kwamba taasisi hiyo kwa jina la kiingereza ina zungumzia Corruption na si bribe.

TAKUKURU - Taasisi ya Kuzuia Na Kupambana na Rushwa

PCCB - Prevention and Control of Corruption Bureau

Ikumbukwe kwamba bribe ni kasehemu kadogo tu ndani ya lijimonster corruption. Siamini kama Dr. Hosea halitambui hili. Cha ajabu ambacho nashindwa kabisa kumuelewa Dr. Hosea ni pale anaposema Richmond kulikuwa hakuna rushwa akimaanisha bribe, Yes bribe kwa sababu hiyo iko kidogo tangible lakini corruption siku zote lazima ihusishe mazingira na mchakato au michakato. Huwezi kusema This buddy is corrupt na ikadhaniwa moja kwa moja eti ni mtoa au mpokea rushwa.

Corruption may be defined as any conduct which amounts to
• influencing the decision-making process of a public officer or authority, or influence peddling;
• dishonesty or breach of trust, by a public officer, in the exercise of his duty;
• insider dealing/conflicts of interests; [and]
• influence peddling by the use of fraudulent means such as bribery, blackmail, which includes the use of election fraud.
• Any person who directly or indirectly accepts, agrees or offers to accept any gratification from any other person to benefit him-/herself or any other person is guilty of the crime of corruption. The person who makes the offer or inducement to another to commit a corrupt practice is also guilty of the crime of corruption. Although there is an active and a passive side to the crime, both parties are equally guilty of corruption.

Ilikuwaje Hosea hakuona hayo, wakati kamati ya Bunge imeyaona na kuchambua moja baada ya lingine.

Bro Hosea wajibika mkuu!!!!!!!!!!!!
 
Kishaju, asante sana Mkuu.... Unajua hili limejibu mengi ambayo tulikuwa tunayaongelea kuhusu TAKUKURU kwenye thread flani hapo nyuma kidogo....

Aisee jamaa hili limemgusa pabaya manake hotuba/risala wengi tumezoea kusikiliza part and forget the next day!!!

Haya yetu macho na masikio!!!
 
Kuna watu tulibishana sana humu siku chache kabla ya jf kufungwa kuhusu hasa nini ilikuwa kazi ya uchunguzi wa TAKUKURU katika ile thread iliyokuwa na kichwa hiki "HOSEA ATAKWEPA DHAMBI HII?" nachofahamu mimi ule mjadala haukwisha ila matukio ya kukamatwa kwa wenzetu yaliuingilia,kama ungeunganishwa na mada hii nadhani sasa ni wakati muafaka wakati bado tunasubiri wadau mtuletee ile ripoti ya HOSEA hapa kuhusu richmond, wale waliokuwa pro-HOSEA na wale anti-HOSEA kuendelea na mjadala huu,hasa baada ya kupata hii clue muhimu ambayo ni agizo la rais. Wahenga wanasema kwamba? "MAOMBI YA MKUBWA NI MAAGIZO"Hivyo nadhani ni kwa hotuba hii ndio maaana hosea alianza uchunguzi,sidhani kama Rais alitoa agizo jingine zaidi ya hotuba yake hii,kama hotuba hii ndio ulikuwa msingi wa uchunguzi basi kwa yenyewe tayari inatupa japo kwa ufupi tu,nini zilikuwa hadidu za rejea za HOSEA.Na hata kama atasema hakuchunguza kwa mujibu wa hotuba hii,basi atatueleza jee haya maagizo ya Rais yaliyomo katika hotuba hii hadi leo kayatekeleza vipi?kama bado badi kashindwa kuwajibika.

Haya wadau kazi kwenu,Kazi kwako mkuu wa TAKUKURU.
 
Ndugu zangu, kulingana na HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWENYE UFUNGUZI WA MKUTANO WA TAKURU, MBEYA, 20 FEBRUARI, 2006 ilikuwa inawapa mwanya TAKUKURU kuuchunguza mkataba wa Richmond kwa undani si mazingira ya Rushwa tu....yaani hata mchakato mzima...ebu angalieni hapa chini sehemu ya hiyo hotuba na tumuulize Hosea je anapingana na kauli ya mkubwa wake aliyemsimika kazini....

"....Naomba nitaje maeneo kadhaa ambayo nadhani itakuwa busara kuyatilia mkazo katika mipango yenu.

Tayari nimetaja rushwa katika mikataba. Kadhalika nimeshaelezea, Bungeni, nia yangu ya kutaka kuangalia upya taratibu za kuingia mikataba zinazotumiwa na serikali, mashirika ya umma na idara zinazojitegemea kwa nia ya kubaini mianya ya rushwa na kuongeza uwazi na uwajibikaji ili kulinda maslahi ya umma. Naomba TAKURU isaidie katika zoezi hili na kuishauri Serikali juu ya mapungufu yaliyopo katika taratibu zilizopo sasa ili yarekebishwe.

Katika zoezi hili, msisahau kuangalia pia michakato ya majadiliano, viwango vya utekelezaji, muda wa utekelezaji, kuhusika au vinginevyo kwa mamlaka za udhibiti wa utekelezaji (regulatory agencies) na hatua sahihi za kuchukua endapo masharti ya mikataba yatavunjwa.

Ni jukumu lenu TAKURU kutumia ujuzi wenu kubaini mapema mikataba batili au ile isiyokuwa na manufaa kwa taifa na kuishauri serikali ili ichukue hatua zinazostahili kabla fedha na mali havijapotea. Kinga ni bora kuliko tiba.

Eneo la pili lenye tuhuma ya kuwa na mianya ya rushwa kubwa kubwa ni la manunuzi/ununuzi (procurement/purchases) Serikalini. Sina budi kukiri kuwa Sheria ya Manunuzi na taratibu nzuri na rahisi za ununuzi zilizowekwa zimesaidia sana kupunguza ukubwa wa kipenyo cha mwanya wa rushwa katika eneo hili. Hata hivyo bado kuna maneno yahusuyo upendeleo, mgawanyo usio sawa, kutokuwepo uwazi wa kutosha wala ushindani halisi kwa kuwa washindani wengine hupewa habari za viwango vya gharama mapema. Kadhalika kuna madai kuwa ununuzi hauzingatii gharama na ubora wa bidhaa. Kwa ajili hiyo yapo madai kuwa wakati mwingine bidhaa zinapewa gharama za juu zaidi na kama gharama ni za kawaida basi baadhi ya bidhaa hazifikishwi kwa mnunuzi kwa maelewano baina ya wanunuzi na wauzaji. Fedha nyingi za serikali hupotea kupitia mwanya huu wa rushwa. Fuatilieni taratibu za manunuzi na ununuzi serikalini kubaini na kuziba mianya ya rushwa katika eneo hili nalo. Nia yangu ni kutaka kuona pesa kidogo tulizo nazo zinatumika kwa manufaa ya umma na watu walio wengi na siyo kuendeleza maslahi binafsi ya watu wachache"

Sasa Hosea kwa nini asiachie ngazi jamani....

Jamani wakati ule Hosea alikuwa hajapata PhD na halikuwa hajawa na vision. Ila sasa it is time PCCB kupata mtu kutoka nje kwani akitoka Hossea wale wa chini yake ni bure. Of course na Hossea ni bure and MUST GO.
 
Back
Top Bottom