Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 15,328
- 11,192
Hawa Ngulume aitwa Korti Kuu, adaiwa sh. milioni 500/-
Habari Zinazoshabihiana
RC azuia madiwani kuzuru Bunge 14.11.2006 [Soma]
Korti Kuu yaamuru mfanyabiashara akamatwe 06.04.2006 [Soma]
Mgambo walazwa kwa kuchapwa fimbo, kucharangwa mapanga 07.01.2007 [Soma]
Na Grace Michael
MAHAKAMA Kuu ya Tanzania imemwamuru Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Bibi Hawa Ngulume, kufika mahakamani hapo Novemba 30, mwaka huu katika kesi ya madai ya sh. milioni 500 kama fidia ya kumpiga mtu na kumsababishia maumivu.
Amri hiyo ilitolewa jana mahakamani hapo na Jaji Robert Makaramba ikiwa ni ya pili ambapo ya kwanza haikumfikia mlalamikiwa.
Jaji Makaramba alisema amri hii itapelekwa na mtu ili imfikie malalamikiwa na sio kwa njia nyingine kama ilivyokuwa mara ya kwanza.
Upande wa wadaiwa walitakiwa kuwasilisha utetezi wao mahakamani hapo kabla ya Novemba 14 mwaka huu na mdai anatakiwa kutoa maelezo mengine kama yatakuwepo kabla ya Novemba 21, mwaka huu.
Bi. Hawa anadaiwa fidia hiyo kutokana na tuhuma za kumpiga kibao mkazi wa Kijiji cha Kapunga, Bw. Ofredy Mkemwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Ardhi na Kilimo ilipotembelea kijiji hicho.
Inadaiwa kuwa wanakijiji wa Kapunga walikuwa wamekusanyika kwa lengo la kutoa malalamiko yao kwa kamati hiyo ya Bunge ilipokuwa inapita kijijini hapo ambapo waliuzuia msafara wa kamati hiyo na kutaka kutoa malalamiko ya manyanyaso wanayopata.
Kwa mujibu wa hati ilivyowasilishwa mahakamani katika kesi hiyo inadaiwa Mkuu huyo wa Wilaya alimchapa kibao usoni, Bw. Mkemwa kutokana na kuwa mstari wa mbele kuwasemea wanakijiji malalamiko yao.
Wanakijiji hao walitaka kupatiwa ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili kutokana na mwekezaji katika mashamba ya mpunga anayedaiwa kuwanyanyasa.
Washtakiwa katika kesi hiyo ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali na Bi. Hawa ambao wanatakiwa kufika mahakamani hapo Novemba 30, mwaka huu.
Mwisho.
Niwe wazi kuwa sina ubaya na huyu mkuu wa wilaya mtukuka, ila nitasimulia ubabe wake kwa ufupi tu. Akiwa mkuu wa wilaya ya Konondoni, mnamo mwaka 2002, aligoma kabisa kusaini fomu zetu za kuombea mikopo kwa ajili ya masomo ya chuo kikuu. Nakumbuka wanafunzi wengi wa vyuo vikuu tuliokuwa wakazi wa wilaya hii tulipata shida sana kupata huuma hii, na kuna wengine walilambwa vibao walipomlazimisha awasainie fomu zao. Ikabidi sisi waoga tuene mikoani kwenda kusainiwa fomu hizi.
Sasa niliposikia kituko hiki cha kumpiga mkulima wa Mbarali nikakumbuka yale aliyoyafanya alipokuwa mkuu wa wilaya ya Kinondoni, nikajisemea kimoyomoyo kuwa, alaaas! Kumbe Mama bado mbabe sio? Hajaacha tu?