Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Great...but don't you think perhaps we learned something from the Americans (in terms of what was wrong with their declaration) being that we gained independence nearly 200 years after it (the declaration) was written?
kwanini Afrika ya Kusini hawakujifunza hilo? Kwanini Ureno hawakujifunza hilo? Kwanini Rhodesia hawakujifunza hilo? Kwanini Tanzania iliweza kujifunza hilo na kuliweka kuwa ni Azimio lao? Ni nchi gani nyingine ya Kiafrika ambayo ilipata nafasi ya kusoma Azimio la marekani na wakaamua kujenga kwa namna yao wao wenyew kama kanuni ya kuwaongoza na kuchukua hatua za kufanya hivyo?
Ghana wao walichukua "Motto" yao na kusema "Uhuru na Haki". Sisi tulichukua ya kwetu na kusema "Uhuru na Usawa" na baadaye pia "Uhuru na Umoja". Kwanini tulichukulia mambo hayo very serious na si nchi nyingine? siyo Kenya, Uganda, Congo, n.k ikawa ni Tanzania?
Wakati Ghana walikubali kutambua vyeo vya kijadi, sisi Katiba yetu ilivikataa tangu mwanzo kwa misingi ya usawa. kwanini Tanzania?
Leo hii tunaishi katika taifa ambalo watu wake hawaelewi inakuwaje mataifa mengine yanayotuzunguka yamegubikwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe na vurugu za kisiasa lakini siyo Tanzania? Je yawezekana kuwa ni bahati tu kuwa tuna Taifa leo ambao watu wake wanafurahia utajiri wa kila namna lakini bado wanatambua ya kuwa katika utajiri huo bado ni kikundi cha watu watu wachache kinaonekana kikinufaika?
Je ni kwa bahati tu kwamba Tanzania ilikuwa inaheshimika duniani katika kutetea haki na hadhi ya mtu mweusi na kupinga ubeberu na unyonyaji wa mtu mmoja na mwingine?
Je yawezekana Mungu alitupendelea sana na kutupa taifa kama hili na kuwanyima Kenya, Uganda, Congo, Zimbabwe, Afrika ya Kusini n.k?